Gari lako hatarini: uchakachuaji mpya wa mafuta umeingia

Synthesizer

JF-Expert Member
Feb 15, 2010
11,023
18,566
Makampuni ya mafuta nchini yamewaandikia EWURA kulalamika dhidi kile kinachoonekana ni uchakachuaji wa mafuta ya diesel na petrol unaofanywa na kampuni inayoagiza mafuta nchini, Augusta Energy. Uchakachuaji huo, ambao pia unaathiri magari, ni ule wa kuchanganya diesel au petroli na ethanol kwa kiwango cha juu bila hata idhini ya serikali. Mafuta yaliyochanganywa na ethanol kwa kawaida yana bei ndogo zaidi, hivyo kampuni ikiagiza mafuta yaliychanganywa na ethanol na kuyauza kama yasiyo changanywa inapata faida kubwa sana.

Kuchanganya diesel au petrol na ethanol ni kitu cha kawaida bila gari kuathirika kwa kiwango cha 90:10, 10% ikiwa ethanol. Ukichanganya zaidi ya hapo lazima ubadilishe mfumo wa mafuta wa gari.

Rwanda, ambayo inapitisha mafuta yake Tanzania, tayari imeshakataa kupokea consignments za mafuta toka Tanzania kutokana na tatizo hili la uchakachuaji na ethanol. Rwanda huko nyuma ilifanya hivi pia kwa uchakachuaji wa kutumia mafuta ya taa, na hata kuwaweka ndani madereva wa Kitanzania waliobeba mafuta yaliyochakachuliwa.

Kisichoeleweka ni jinsi gani TBS wamekuwa wakiruhusu shehena ya mafuta yaliyochanganywa na ethanol iingie nchini wakati Tanzania haina utaratibu wa kutumia "blended fuel". Zaidi ya hapo, swali la kujiuliza ni kwa nini TBS waliruhusu kuingia nchini mafuta yaliyochanganywa na ethanol kwa kiasi cha juu sana cha kuharibu magari ya watu.

Original source: IPP media
 
Kwa serikali hii ya waenda misibani kila kukicha unadhani nani yupo kazini kusimamia Nchi?!! Underperformance has become our way of life!!
 
Ngoja ya mkuu wa kaya yakizimikia kwenye msafara atapata somo kama yaliyomkumba moshi.
 
Hao wanaoingiza mafuta ni wahuni wa pale magogoni unategemea nini?
Ela feki wao.
Madawa ya kulevya wao.
Wachakachua mafuta wao.
Mafisadi wao.
Watoroshaji wanyama pori wao.
Wenye hisa kwenye migodi ya dhahabu wao.
Yani ikulu pamekuwa pango la walanguzi.
 
dah......this country bwana..!!!
 
sijui mpaka hiyo siku nchi hii itakapowekwa sawa tutakuwa tumeshapata madhara kiasi gani kwa kweli!
 
Nasikia kuna kampeini inayolenga kuhakikisha kuwa mafuta hayaagizwi kwa pamoja inayoendeshwa na wafanya biashara mbali mbali wa mafuta wakishirikiana, EWURA na pamoja wanasiasa. Hata upandaji wa bei na matatizo yaliyotekea hapo nyuma ilikuwa ni juu ya hii. Hivyo tuwe makini na hili tusije kutumiwa
 
Sidhani kama ni kampuni za mafuta zinazohusika, maana, hii inahusianaje na mafuta yanayokwenda Rwanda? Kuna mawili;

1. Augusta Energy wanaagiza mafuta yaliyachakachuliwa makusudi ili watengeneze faida kubwa kwa kuwa wanayauza kwa bei ya "unblended fuel"

2. Uchakachuaji unafanywa hapa nchini na mtandao ule ule uliokuwa unahusika na uchakachuaji kutumia mafuta ya taa.

Ikiwa namba (1) hapo juu ni kweli ina maana Augusta Energy wanafanya hivyo eidha kwa shinikizo au kushirikiana na vigogo wakubwa serikalini, Ikulu au CCM, ndio maana hata TBS inabidi wapitishe mafuta ambayo wanajua hayafai.

Ikiwa namba (2) hapo juu ni kweli ina maana katika kipindi hiki cha bulk oil procurement kutakuwa na uingizaji mkubwa sana wa "ethanol" nchini, na kinachotakiwa ni kutafiti nani amekuwa akiagiza "ethanol" kwa wingi nchini ili ajieleze hiyo ethanol inatumika wapi.

Hili ni suala ambalo linabidi lichunguzwe na kamati ya Bunge, si EWURA. Ni jambo ambalo tunapaswa tuwasihi wabunge wetu wafuatilie. Inatia aibu sana kwamba kila siku Tanzania tunakuwa chanzo cha matatizo kwa nchi zinazotumia bandari yetu kupitisha bidhaa zao, hasa hili suala la mafuta. Mtu kama Kagame pale Rwanda hana hamu na Tanzania, nadhani kila siku anawaza njia mbadala ya kupeleka mafuta Rwanda. Kwa nini tuwafanyie hivi watu wanaotegemea bandari yetu na kutulipa pesa ya kigeni?
 
Nasikia kuna kampeini inayolenga kuhakikisha kuwa mafuta hayaagizwi kwa pamoja inayoendeshwa na wafanya biashara mbali mbali wa mafuta wakishirikiana, EWURA na pamoja wanasiasa. Hata upandaji wa bei na matatizo yaliyotekea hapo nyuma ilikuwa ni juu ya hii. Hivyo tuwe makini na hili tusije kutumiwa

Ndugu yetu kama hujafanya utafiti afali usiseme kwani, mfumo huh ulianzishwa NA ewura how comes Auhujumu? Pia issue ya kuchakachua Huko nyuma hamkusikia kwa kuwa hii term was introduced by EWURA amabye alia za masks 2006 NA ndoo maana Huko nyuma hukuwa unasikia
 
wajameni huu uzi umikaa kiudaku hivi. Dizeli ichanganywe na ethanol! Hilo mbona ni sawa na kuchanganya dizeli na petrol?
 
Hao wanaoingiza mafuta ni wahuni wa pale magogoni unategemea nini?
Ela feki wao.
Madawa ya kulevya wao.
Wachakachua mafuta wao.
Mafisadi wao.
Watoroshaji wanyama pori wao.

Wenye hisa kwenye migodi ya dhahabu wao.
Yani ikulu pamekuwa pango la walanguzi.

Your vote has the final say!!!
We are so divided when it comes to the National matter! Every individual is poor to think even for 2 year to come!
 
wajameni huu uzi umikaa kiudaku hivi. Dizeli ichanganywe na ethanol! Hilo mbona ni sawa na kuchanganya dizeli na petrol?

Nachukia kuita udaku jambo usilolielewa, ni bora uulize ufahamishwe. Ethanol-diesel fuels zinaitwa E-Diesel. In fact, ni hatari sana ku-blend bila utalaamu wa haya mambo. Soma hii document;

http://www.ornl.gov/sci/eere/PDFs/sci_tech_hilights/No_1_2001p9.pdf

inaongelea "Ethanol blending to reduce emissions from heavy duty diesel engines"

Pia soma hii document;

http://www.nrel.gov/docs/fy03osti/34817.pdf

inaongelea "Safety and Performance Assessment of Ethanol/Diesel Blends (E-Diesel)
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom