Gari la Zitto lapata ajali?

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,802
613
Kuna habari kwamba, gari la Zitto Kabwe,limepata ajali baada ya watu wanaodhaniwa kuwa walikua na malengo ya kulipora kugonga nyumba moja huko wilayani Temeke. Gari hilo kwa sasa liko kituo cha polisi, Chang'ombe... Kama kuna mwenye taarifa za ziada atuwekee humu ama kama kuna mtu ambaye ameweka taarifa hizi katika thread ambayo sijaiona naomba anisaidie kuhamisha maana tukio hili linaelezwa kutokea kati ya usiku wa kuamkia leo na leo asubuhi kwa hiyo upo uwezekano wa ama kuwa tayari limeripotiwa ama kuwapo taarifa mpya
 
CCM hao nini?
lakini tusubiri taarifa zaidi isije ikawa leo ni siku ya wajinga!!!

Zitto alikuwa na mkutano leo DDC
 
Ni kweli na nimeongea na zitto leo wakati akiwa kwenye kongamano na wanafunzi wa vyuo vikuu pale DDC aliweza kutudokeza waandishi tuliokuwa pale na hakika kwa maelezo yake na kama igizo fulani .

Hii inatokana na dereva wake jana usiku kuchelewa sana kuondoka kutokana na vikao vya zitto hivyo akaamua kumwachia gari lake ili aweze kuondoka nalo na dereva alipofika karibu na kwao alienda kulilaza maeneo ya kulaza magari na ,ilipofika jana saa saba usiku alifutwa nyumbani (dereva)na kuambiwa kuwa gari alilokuwa ameliacha sehemu za kulaza magari limegonga nyumba ya watu na limeharibika vibaya.

Haijulikani kuwa gari hilo lilikuwa linakwenda wapi, na ni kweli kuwa lipo polisi changombe na polisi wamewashikilia walinzi wawili wa eneo hilo la kulaza magari japo haijajulikana kuwa nini kilitokea uchunguzi unaendelea.

Dereva wake bado anaisaidia polisi ,kuna habari kuwa wakati linagonga nyumba lilikuwa limebeba watu wanne hii ni kwa mujibu wa mashuhuda wa ajali waliohojiwa na polisi.
Nimeongea na rpc wa temeke na kadhibitisha tukio hilo na bado wanaendelea na uchunguzi.
 
Gari hakua nayo yeye, gari ilikua na dereva, katika parking ikachukuliwa, hadi sasa walinzi wamekimbia hawajulikani walipo na dereva wa Zitto alikua polisi anaandika maelezo hadi sasa ndio anajiandaa kuachana na polisi. Gari liko polisi Chang'ombe
 
Kada huwa una kazi nyingine ya kufanya ama upo ni mwajiriwa wa hapa jf?

Nauliza maana kila wakati mchana na usiku huwa uko hapa ama mko wengi lakini mna mawazo yanayofanana?

Hata week end jamani?sijui wewe ni mkaka ama ni mdada ,naomba kuuliza usinielewe vibaya, mimi ni mwandishi wa habari.
 
Re: Breaking News: Gari la Zitto lapata ajali???

--------------------------------------------------------------------------------

Quote: UFUNUO WA YOHANA
CCM hao nini?
lakini tusubiri taarifa zaidi isije ikawa leo ni siku ya wajinga!!!

Zitto alikuwa na mkutano leo DDC

chadema oyeeeeeeeeeeeeeee !

Kada hata mambo serious unaweka mambo ya masihara, ama kati ya wanne waliokuwamo katika gari ulikuwamo na ww? Maana huwezi kusema Chadema oyeee kwa ajali. Acha nijipumzikie niachane na kero zisizo maana weekend hii
 
Kada huwa una kazi nyingine ya kufanya ama upo ni mwajiriwa wa hapa jf?

Nauliza maana kila wakati mchana na usiku huwa uko hapa ama mko wengi lakini mna mawazo yanayofanana?

Hata week end jamani?sijui wewe ni mkaka ama ni mdada ,naomba kuuliza usinielewe vibaya, mimi ni mwandishi wa habari.

hii kitu yangu nikitaka kulog out INAKATAA KATA KATA, sijui kwa nini !

Kuwepo kwangu online haimaniishi nipo JF wakati wote, hiyo sio kweli ! kama nipo online wakati wote ningekuwa walau najibu baadhi ya posts za members lakini utakuta status inaonyesha nipo online kumbe sijakanyaga JF siku kadhaa !

Kuhusu jinsia yangu, hiyo sidhani kama itakusaidia kwa njia yoyote ile au kuleta mapinduzi kwenye taifa letu !

Gud kwako wewe kuwa mwandishi wa habari angalau sipo hapa kujua nani ni nani na wanafanya nini !

AM HERE FOR AN ASSIGNMENT ! and i will do it !
 
Kada hata mambo serious unaweka mambo ya masihara, ama kati ya wanne waliokuwamo katika gari ulikuwamo na ww? Maana huwezi kusema Chadema oyeee kwa ajali. Acha nijipumzikie niachane na kero zisizo maana weekend hii

MKUU,
Hivi wewe unataka kusema huyo mtu aliyesema CCM hao alikuwa serious ? no way, kama mimi sipo serious, nadhani ungeanza na huyo aliyeanza kuishutumu CCM kwanza kabla ya kuniangukia mie !

I know i wasnt serious, hiyo nakili, simply because ya huyo member aliyesema kwamba hiyo ni ccm ! Mungu hayupo jamani ? mbona wanapopata ajali viongozi wa ccm, kamwe huwezi kusikia ccm au wanachama wao wakisema wapinzani hao ?? au nyie wapinzani ndio tabia mnazofunzwa na wenyeviti wenu wa vyama ?? well, chama tawaka hatupo hivyo !
 
Pole mzee Zitto wapo watakaokutisha lakini Mungu yupo kwa aliye ktk haki.

great !

kama zitto kapata ajali kwa nini tusiseme dreva wake alikuwa mzembe ? maana haya ndio maneno yaliyotawala katika ajali za viongozi waliopata ajali before, au kwa nini tusiseme mbowe nae kaanza kutoa kafara wanachama wake wa chadema ?
 
Watu hapa wana vituko kweli kweli, yaani kwasababu gari la Zitto limegonga nyumba basi hapo kuna mkono wa mtu?

Kwa mtu mwenye uzoefu na Tanzania hilo mimi sishangai, si ajabu dereva ndio alipata muda wa kwenda kutamba na gari la boss wake na kusababisha ajali.

Hapo mimi naona moja kwa moja ni uzembe wa dereva, atakuwa alienda kulitumia hilo gari au aliwaachia marafiki zake.

Acheni kuwa paranoid na CCM au serikali yake hata kwa mambo ambayo kwa kweli hayana maana.

Pole sana Zitto kwa gari lako kupata ajali.
 
Personally, I dont think kwamba hii ni issue muhimu ya kujadiliwa hapa JF. Gari ya zitto imegonga nyumba??? So what???
 
Watu hapa wana vituko kweli kweli, yaani kwasababu gari la Zitto limegonga nyumba basi hapo kuna mkono wa mtu?

Kwa mtu mwenye uzoefu na Tanzania hilo mimi sishangai, si ajabu dereva ndio alipata muda wa kwenda kutamba na gari la boss wake na kusababisha ajali.

Hapo mimi naona moja kwa moja ni uzembe wa dereva, atakuwa alienda kulitumia hilo gari au aliwaachia marafiki zake.

Acheni kuwa paranoid na CCM au serikali yake hata kwa mambo ambayo kwa kweli hayana maana.

Pole sana Zitto kwa gari lako kupata ajali.

si ndio maana muda wao mwingi hutumia kuondoa stress zao kwa kumuita Mheshimiwa rais Fuska, muhuni, mpenda ngono, sijui picha wanazo, mara kila anayeungana na ccm ni fisadi yaani vituko kweli kweli ili mradi wasikie raha and they are good at that !
 
Maelezo ya dereva ndiyo yatakayotoa mwanga ni mapema mno kusema lolote

lakini hujui humu kuna mapolisi washaanza kutoa majibu hata kabla ya maelezo ya dreva hayakutolewa ! watu washasema ccm hao !

ndio hapo ninapopata mwanya wa kusema CHADEMA OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEE ! maana ccm sasa imezidi bana kila baya litakalotokea kwa wapinzani ni wao tu ! teh teh teh teh !
 
Back
Top Bottom