Gari la milioni arobaini la masafa marefu

Gari la milioni arobaini la masafa marefu

GoldDhahabu

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2023
Posts
7,648
Reaction score
10,843
Ushauri wako tafadhali!

Linahitajika gari la masafa marefu linalomudu safari za mashambani. Route zake ni kama vile:
1. Mwanza - Arusha
2. Arusha - Njombe
3. Njombe - Mtwara
4. Mtwara - KASULU
5. Kasulu - Mwanza
6. N.k.

Kama nilivyoandika, safari nyingi nibza mashambani, kwa hiyo ni muhimu liwe gari la juu. Double cabin pick up inaweza kuwa bora zaidi lakini si lazima liwe double cabin pick up! Hata

Je! Gari lenye hizo sifa linaweza kupatikana kwa bei isyozidi milioni arobaini na tano?
1. Ni salama kununulia kwa mtu?
2. Milioni arobaini na tano zitatosha kuagiza kutoka Japan au Afrika Kusini?
3. Aina gani hasa linalomudu barabara za mashambani?

Asanteni🙏🙏🙏
 
Chukua D/C make ya TOYOTA hutajuta
 
Ndugu ipo mitsubishi warrior ya muingereza ni manual
 
Utapata Pick up ya China yenye engine ya 2.2 diesel ya 2010 mpaka 2012 kodi yake ni 12m kwa 2010 na 2012 ni 13m mpaka 14m na gari ya bei nafuu SA ni Nissan hard body ila ina kodi kuanzia 18m kuendelea kwa double cabin...
Gharama kutoa gari SA
Karatasi za gari pamoja na Interpol
Mipaka ya SA/Botswana
Zambia kuingia kupata bond na kufuta upande wa Tunduma.
Service ya gari kwa ajili ya safari
Diesel mpaka Tunduma.
Agent upande wa Botswana kuingia pamoja na kulipia ushuru wa bara bara kwa gari ndogo ni pula 280 agent anachukua pula 500 mpaka 600.
Toll gate upande wa Zambia Zipo 7 @ unalipia Kwatcha 20 kwa gari ndogo.
Rushwa upande wa Zambia na Botswana wakiamua wanakupeleka polisi ukalipe faini watakayoamua kazungula na Nata...
Kununua gari SA inatakiwa ukaze kweli maana hela unaiona ikiteketea ukienda na hela ndogo utapata tabu..
 
Achukue Toyota Double cabin hizo ndio ndio gari za kazi
Kodi 20m kuendelea mpaka 26m anunue bei gani na lifike kwa 40m na kumbuka hiyo pesa inabadilishwa kwa karibu Nchi tatu toka rand,pula na kwatcha kwa gharama za huko Toyota kodi zipo juu..
 
Mazda pick up nayo ina kodi ndogo iwe ya kuanzia 2010 kuja mbele ila nikipiga hesabu inataka 50m za kitanzania mpaka inafika nyumbani..
 
Ishi na HiLux
Mkuu hizo hilux chungulia kikokotoo cha TRA na mwaka wake uone TRA watachukua ngapi kwa gari zenye soko kubwa na imara wao ndio wameweka kodi kubwa ila gari mbovu mbovu kodi ipo chini..
 
Back
Top Bottom