Gari kuweka tinted inamaanisha nini?

Gari kuweka tinted inamaanisha nini?

mzenjiboy

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2010
Posts
907
Reaction score
387
Asilimia kubwa ya wenye magari utaona vioo vyao ni black yaani huoni ndani yaani tinted. Gari iwe ndogo kubwa au hata lorry la mawe na mchanga nalo limo kundini mwa tinted, taxi nazo hazijasalimika, na wewe taja gari yoyote basi ni tinted.

Na tinted kuna kwa kiasi kama vile 30% ambayo ina uafadhali sio kali sana kuna na 50% pia. Lakini hizo za 30 au 50 hazitumiki ila wote huweka 100% yaani giza totoro. Tinted hazitumiki kwa nia njema bali hutumika kwa njia mbalimbali tena chafu na ovu.

Wewe mwenye gari ya vioo black hebu tupe sababu zenye mashiko na za uhakika kipi kilichokupeleka kuweka gari yako tinted.

Ramadhan Kareem
 
Sababu ni nyingi,wengine hawapendi michorano,wengine kwaajili ya kuficha medemu hasa wake za watu,wengine wanaficha maboksi ya magendo n,k
 
Watu wanavunja sheria sababu vioo viwili vya mbele havitakiwi kuwekwa tinted. Ila sheria za barabarani Tz who cares? Hakuna anayezifuata anyway.
 
Wamachinga kwenye foleni wanasumbua sana, macho yakielekea tu kwenye bidhaa anayo uza ni shida. Bora asikuone kama unaangalia ili kama unahitaji ufanye kumwiita na sio wote kukuvamia kama ugomvi.

Sent using Jamii Forums mobile app

Sio tu wamachinga, tinted inasaidia mengi. Mimi jana nimemuona jamaa mmoja anaenidai hela ndefu na ameshanipigia simu mara kibao nikawa napotezea. Sasa jana nimekutana nae sehemu ambayo haiepukiki jamaa kakomaa kunipungia nisimame mi nikajidai sijamuona nikanyoosha goti. Uzuri wala hawezi kujua kama ni mimi kweli nilikua na drive.
 
Tembea uone. gari zenye tinted zipo dunia nzima na kizuri zaidi ni kuwa gari nyingi zinatengenezwa na kuwekwa vioo tinted kabla ya kuuzwa
 
Wanawake hawapendi kukaa kwenye gari lisilokua na tinted maana hua wanapenda kula koni na kushikwa shikwa mapaja akiwa na jamaa yake na ikiwezekana hua wanalaza siti ili kuhitimisha game.
Nimeshawapa koni wengi sana kwa staili hii
 
Back
Top Bottom