Gari haikunisaidia katika kutongoza

Gari haikunisaidia katika kutongoza

We boya hakuna chapati mgumu mbele ya kahawa.... [emoji23] [emoji1]
 
Pesa hainunui mapenzi ya kweli.angalia namna nyingine.jishushe.siku nyingine tembea kwa miguu.ukiwa unamfatilia.
Kuwa na gari usifikiri ndo umemaliza kazi kwa mwanamke
Kuna wanawake hawapendi shobo.
Umesema vyema kabisa
 
Unaweza kuwa na unafuu wa maisha na ukamkosa msichana na akaja mtu ambae hana hata uhakika wa mlo na akamchukua kiulaini. Kosa kubwa unalolifanya ni kutumia nguvu nyingi bila kujua kuwa ni binti anayependa aina gani ya wanaume. Na kipi hapendi. Kama ungejieleza vya kutosha ningekupa mbinu na ungeleta feedback
 
Option zote zikifeli jitoe muhanga mkuu,jaribu trick yangu hii,imefanya kazi kwangu twice....nenda kwao ukiwa umevaa kiheshima,gonga mlango wa mbele tena akifungua mzazi wake itapendeza zaidi,salimia kisha uombe kuitiwa huyo binti hakika atashtuka sana na ataona kweli wewe mwanaume na ukimuomba mawasiliano hapo hawezi kukataa.
NB:Uwe mtu mzima,kama mtoto usijaribu..utakamatwa na kuchapwa fimbo zisizo idadi.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] fimbo zisizo idadi..
 
Hapo wanaokuchezea ni hao marafiki ..wanataka kuzila ela zako kwanza kabla hujafanikisha..
 
Back
Top Bottom