Gari haikunisaidia katika kutongoza

Gari haikunisaidia katika kutongoza

Jindal Singh

JF-Expert Member
Joined
Sep 9, 2015
Posts
1,857
Reaction score
1,543
Jamani leo nimeamua kuleta huu uzi, lakini hauna style ya ki-beira baby boy ki-beira baby boy. Unajua ukiwa mtu mzima then ukawa unafanya mambo ya kitoto inakuwa ni kituko sana katika jamii inayokuzunguka hasa ukiwa umebeba dhamana ya ukubwa.

Kuna kabinti kamoja hivi naona moyo wangu ushaanza kupiga kwa ajili yake ila sasa haka kabinti huwa kapobize sana kwanza hakina muda kabisa yaani yeye na kazi kazi na yeye, inafika kipindi inabidi ilikumpata nitumie ma massanger, hadi muda huu nishatumia watu kama 3 hivi ili kunitafutia mawasiliano yake kwa bei yoyote ile cha ajabu hakuna hata aliyefanikisha kuna mmoja nikampa namba zangu katika karatasi lakini kwa taarifa za chini chini nasikia alizichana.

Tatizo huyu binti nasikia huwa hana shobo na watu wenye nafuu ya kimaisha, na ukitazama ni kweli kuna siku nilikuwa katika gari nikajifanya mashauzi ya mkoko nikamsalimia kisha nikamwambia njoo kidogo dah! basi kama nimejitia nuksi kila nikipishana nae njiani nikiwa nipo ndani ya gari hunipitia mita za uchaguzi.

Sasa hapa issue ni kukutana nae au nipate mawasiliano yake na option zilizo baki ni mbili tu! ya kwanza ni kumtumia rafiki yake ilianiunganishe nae au anipe mawasiliano yake nipo tayari hata kumpa pesa akifanikisha, katika upande wa kumtumia rafiki yake hapa kuna changamoto moja, kwanza huyu rafiki yake sina mazoea nae nahisi nikimfuata atadhani namtaka kimausiano hivyo akisikia namtaka rafiki yake itakuwavigumu kuniunganisha nae sababu ataona wivu.
Na option nyengine iliyobaki ni kwenda kwao mpaka home, lakini kwenda huku kwa sio direct kujitambulisha ila ni kumtuma msichana akaniombee namba zake kwa dada zake kwa njia yoyote ile.Niliwahi kupata bahati ya kukutana nae siku moja tu du! huwezi amini alinipa 7 second yaani nilimsalimia to na kisha akaondoka akasema nachelewa.

Tatizo linalonifanya nimng'ang'anie huyu mtoto kwanza ni uzuri wake, yaani unanifanya ni date na ukija na kijitabia chake kidogo kana ridhisha, then isitoshe kila mwanaume anamsifia kuwa yeye ni mzuri, basi hapo ndipo napoona kwanini nimkose wakati nafuu ya maisha ninayo.

Sasa nimeleta hapa ilimnipatie mikakati ya kumnasa huyu mtoto ikiwemo kupata mawasiliano yake. Kama nitafanikisha basi moyo wangu utafurahi sana na akinikataa moyo wangu utaumia sana.

Pale unapompenda mwanamke kisha ukamtongoza na akakukataa kisha ukawa kila siku unamuona katika macho yako huwa inauma sana afadhali awe mtu wa mbali.
 
Summarize kwanza story yako ndo nikuitie wakali wa hizo kazi wakupe maujuzi
 
Sasa nimeleta hapa ilimnipatie mikakati ya kumnasa huyu mtoto ikiwemo kupata mawasiliano yake. Kama nitafanikisha basi moyo wangu utafurahi sana na akinikataa moyo wangu utaumia sana.
😀😀😀
Ngoja wazee wa hat trick waje...
 
😀😀😀
Ngoja wazee wa hat trick waje...
By the way, ungeanza kumtafuta kwenye mitandao ya kijamii kama fb na insta. Basi kule ni mwendo wa ku like kila kitu anachopost. Hii itakufanya upate attention yake. Then the rest is the history...
 
Mkuu yote hiyo unataka kibwenye tu,si vibwenye naviona vingi tu!!!!
Achana na hizo option Mimi nakupa option namba 3-tafuta kibwenye kingine
 
By the way, ungeanza kumtafuta kwenye mitandao ya kijamii kama fb na insta. Basi kule ni mwendo wa ku like kila kitu anachopost. Hii itakufanya upate attention yake. Then the rest is the history...
Hata jina sifahamu.
 
Watu tunamiliki mvi kichwani na baiskeli tu, ila watoto wakali tunang'oa kama kawaida wallah....[emoji13] [emoji13]
 
Nenda kwa mganga...
au acha kutembelea gari yako hiyo!!
 
Enzi hizo bado kijana mambo kama haya yalikuwa hayanipi taabu, nilikuwa naingia mawindoni mstari wa mbele mimi mwenyewe nafanikisha nagonga ngozi nasonga mbele, sasa uhengani huku ndio mteremko tu ka kumsukuma mlevi vile, ni mwendo wa three some kwa kwenda mbele tu
 
Mkuu yote hiyo unataka kibwenye tu,si vibwenye naviona vingi tu!!!!
Achana na hizo option Mimi nakupa option namba 3-tafuta kibwenye kingine
Katika mapenzi inatakiwa uusikilize moyo kwanza, istoshe mimi sio mtu wa wanawake wengi.
 
Option zote zikifeli jitoe muhanga mkuu,jaribu trick yangu hii,imefanya kazi kwangu twice....nenda kwao ukiwa umevaa kiheshima,gonga mlango wa mbele tena akifungua mzazi wake itapendeza zaidi,salimia kisha uombe kuitiwa huyo binti hakika atashtuka sana na ataona kweli wewe mwanaume na ukimuomba mawasiliano hapo hawezi kukataa.
NB:Uwe mtu mzima,kama mtoto usijaribu..utakamatwa na kuchapwa fimbo zisizo idadi.
 
[emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] [emoji3] usimdanganye mkuu
 
Chezea Kipochi manyoya... hakijawahi kumwacha kidume salama...

'Kwani ukinywa MAJI unamuona kwenye glass au unajiona mwenyewe!?
 
Back
Top Bottom