TANZIA Gardner G Habash mtangazaji wa Clouds Media afariki dunia

Mtangazaji Mahiri wa Clouds FM, Gadner G. Habash (50) amefariki Dunia Leo April 20, 2024.

Gadner maarufu kama ‘Captain’ aliejizolea Umaarufu Mkubwa kupitia Kipindi cha Jahazi, alikua amelazwa katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) Jijini Dar es Salaam kutokana na kusumbuliwa na Pressure (Shinikizo la Damu).

Wasafi Media Tunatoa Pole kwa Familia , Clouds Media Group , Ndugu Jamaa na Marafiki . Mungu ailaze Roho yake Mahali Pema Peponi Amein

Wasafi Media

View attachment 2968923

Pia soma
- Mtangazaji Captain G. Habash alazwa JKCI kwa tatizo la Shinikizo la Damu
Duh Lady Jay Dee Si ataumia sana!
 
“Who wil Cry when You die”- Robin Sharma!
Kitabu hiki ukikisoma unaweza kujifunza sana kutoka kwa watu au ujifundisha mwenyewe na kujifunza kwako mwenyewe na si kudhani na kufikiri kuwa eti kifo cha mtu ni funzo!

Wenye akili finyu ndio wanadhani wanatakiwa kujifunza kutokana na vifo… kifo ni hitimisho ya maisha lakini nafikiri tunaweza kujifunza zaidi watu wakiwa hai …..
Gadner ni mmoja wa watangazaji bora sana katika kizazi hiki na kilichopita na alikuwa na uwezo wa kwenda na wakati na alikuwa anaweza kufit kila eneo kwa hiyo kama alipokuwa hai watu wakashindwa kujifunza na wanasubiri wajifunza msibani basi hao tuwaite “misiba”

Gadner alikuwa binadamu kama wengine na kwakweli alikuwa ni kivutio kikubwa sana kwenye usikilizaji wa radio kuanzia clouds fm,times fm na Efm !

Kama binadamu wengine lazima alikuwa na mapungufu na kama kuna jambo alilifanya linapelekea matatizo yake na kuhitimisha safari yake basi ni jambo alilolichagua na alikuwa anajua fika njia aliyo ichagua!
 
The 109 years ww2 veteran alikuwa anavuta pakti kadhaa za sigara kila siku!! Na hakufa kwa kansa, Warren buffet is 94 years old na anakunywa 5 cans of coca cola daily, with junk foods hasa sweets and fried chickens.
Maisha ni bahati tu sio uhodari wala kanuni

Vyakula na vinywaji vina athari na faida zisizofanana baina ya mtu na mtu, kila mwili una reaction tofauti mkuu...

Ina wezekana kabisa pombe ikawa ina madhara kwa mtu A na isiwe kwa mtu B kwa sababu uwezo wa kuimeng'enya na kuitoa mwilini unatofautiana...

Mathalani mchicha na mboga za majani ni chakula utashauriwa ukitumie kwa wingi, lakini kuna wengine wakila wanapata shida ambazo ni fatal kwa sababu ya uwepo baadhi ya madini...
 
Back
Top Bottom