TANZIA Mtangazaji wa Clouds FM, Ephraim Kibonde afariki dunia. Azikwa makaburi ya Kinondoni,Dar es Salaam

mtzmweusi

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
8,591
8,874
k (33).jpg

Habari za hivi punde ni kuwa mtangazaji maarufu wa Clouds FM, Ndugu Ephraim Kibonde amefariki dunia alfajiri ya leo tarehe 7 Machi 2019.

Kibonde alianza kusumbuliwa na presha akiwa katika msiba wa marehebu Ruge Mutahaba huko Bukoba mkoani Kagera na kuhamishiwa hospitali ya Bugando jijini Mwanza ambapo mauti yamemkuta. kifo chake kimetokana na kusumbuliwa na shinikizo la damu ambalo lilianza tangu akiwa mkoani Kagera alipokuwa akishiriki katika maziko ya aliyekuwa mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group Ruge Mutahaba.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza pamoja na Mkuu wa Vipindi wa Clouds FM, Sebastian Maganga wamethibitisha kutokea kwa kifo hicho.

Baba mzazi wa aliyekuwa mfanyakazi wa Clouds FM Ephraim Kibonde amezungumzia kuhusu kifo cha mtoto wake na kusema kuwa ni mtoto wa pili katika familia na amezaliwa mwaka 1972 Upanga jijini Dar es Salaam.

Vilevile amesema kuwa Ephaim Kibonde amesoma hapa Dar es Salam na ameacha watoto watatu ambao ni Junior, Hilda na Illaria.

Kibonde pia alikuwa MC maarufu na mahiri katika shughuli mbalimbali amefariki dunia ikiwa imepita miezi saba tangu aondokewe na mke wake aliyejulikana kwa jina la Sara Kibonde wakati anapatiwa matibabu katika hospitali ya Hindu Mandal jijini Dar es Salaam

Bwana ametoa, Bwana ametwaa

Mwaka jana Ephraim Kibonde alimpoteza mkewe mama Sara Kibonde. Zaidi soma >TANZIA: Ephraim Kibonde afiwa na Mke wake Sara Kibonde - JamiiForums

maxresdefault.jpg

Ephraim Kibonde akiwa na mkewe enzi za uhai wao​
 
Habari za hv punde kua huyu mtangazaji wa cluz media group ametutoka dunia.
Pole ndugu jamaa na familia kwa ujumla kwa kumpoteza kijana mchapa kazi.
Kama taifa na tasnia ya habari akika tumepoteza mtu makini sana.
Pumzika kwa amani mungu akupunguzie na azabu kabli.



Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Ephraim Kibonde amefariki usiku wa kuamkia Leo tarehe 7 machi 2019

Hatujapoa bado na msiba wa Ruge Leo Kibonde hatunae

Huzuni sana Mungu awape faraja watoto wake

Sent using Jamii Forums mobile app
IMG_20190307_081452_905.JPG
siri ya kifo aijuae muumba, hapa alikuwa anasimamia wekaji wa mashada ya marehemu ruge, wala hakujua siku 3 mbele zinazofuata mauti ya tamkumba, tunatembea na vifo hakika sisi si lolote wala chochote, Mungu ampe kauli thabiti amina.
 
Tukiwa bado na majeraha mabichi ya msiba wa Mkurugenzi wetu wa Vipindi na Uzalishaji #RugeMutahaba, kwa masikitiko makubwa tunatangaza kifo cha Mtangazaji wetu #EphraimKibonde kilichotokea alfajiri ya leo (Machi 7 2019)

Tunamtukuza Mungu kwa Maisha ya Kibonde, na kumuomba yeye ampokee na kumpuzisha katika makao ya amani ya milele.

Tutaendelea kuwapa taarifa zaidi kuhusiana na msiba huu. Bwana Ametoa, Bwana Ametwaa, Jina lake Lihimidiwe.
FB_IMG_1551936159776.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom