Ganzi nyayoni inasababishwa na nini? Na nini tiba yake?

Nhinawe

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
1,127
1,426
Habarini za jioni Wana JF.

Humu ni sehemu ambayo nimejifunza mengi. Watu wamepata utatuzi wa yale yanayowasibu.

Kama mada inavyosema, nina tatizo la ganzi nyayoni. Hii husababishwa na nini? Nini tiba yake?

Natanguliza shukrani kwa msaada wenu.
 
Habarini za jioni Wana JF.
Humu ni sehemu ambayo nimejifunza mengi. Watu wamepata utatuzi wa yale yanayowasibu.
Kama mada inavyosema, nina tatizo la ganzi nyayoni. Hii husababishwa na nini? Nini tiba take?
Natanguliza shukrani kwa msaada wenu.
Moja ya sababu ni maungio ya mifupa ya mfumo wa uti wa mgongo kukandamiza mshipa wa fahamu, ni dalili ya mwanzo ya kiharusi
 
Habarini za jioni Wana JF.
Humu ni sehemu ambayo nimejifunza mengi. Watu wamepata utatuzi wa yale yanayowasibu.
Kama mada inavyosema, nina tatizo la ganzi nyayoni. Hii husababishwa na nini? Nini tiba take?
Natanguliza shukrani kwa msaada wenu.
Ni uchawi. Fanya Dua omba
 
Siyo mtaalamu ila kutokana na past experience yangu, unatumia kahawa kwa wingi? Kama ndiyo kahawa isiyochujwa vizuri inapelekea kuziba kwa mishipa na damu isizunguke mwilini vizuri nenda pharmacy mwelezee atakupa dawa
 
Jaribu sana ku-monitor pressure na sukari kwa ukaribu sana, pengine inaweza kuwa Moja ya sababu
 
Siyo mtaalamu ila kutokana na past experience yangu, unatumia kahawa kwa wingi? Kama ndiyo kahawa isiyochujwa vizuri inapelekea kuziba kwa mishipa na damu isizunguke mwilini vizuri nenda pharmacy mwelezee atakupa dawa
Siyo mpenzi wa kahawa hata kidogo.
Ila asante kwa ushauri.
 
Yawezekana uko pre-diabetic au diabetic tayari. Bila kupoteza muda fanya vipimo vya sukari pamoja na presha. Pima pia kiwango cha lehemu (cholesterol) kwenye damu. Hii combo ni mbaya sana aisee na usiombe ukafika kwenye full blown diabetes na hypertension.

Nenda kwa daktari ukapime hivyo vipengele haraka sana. Kama bado hali inadhibitika basi atakushauri ubadilishe kabisa mfumo wa maisha yako. Kama unakunywa pombe na kuvuta sigara itabidi uache. Kama uko mnene itakubidi upambane sana upunguze uzito. Pia itakulazimu uushughulishe mwili kwa mazoezi hata kama ni kutembea kwa angalau dakika 30 kila siku. Ulaji wa nyama nyekundu, soda na mapochopocho mengine itabidi upunguze. Ni mboga za majani sana pamoja na matunda matunda -hasa yale ambayo hayana sukari nyingi.

Labda kama ni tatizo jingine lakini kama uko pre-diabetic unaweza kabisa kureverse hiyo hali kwa kubadili tu mfumo wa maisha. Usisubiri mpaka uanze kutumia dawa maana ukianza tu mara nyingi ndiyo hakuna kuacha mpaka siku unaondoka hapa duniani.

Vipi kuhusu sita kwa sita? Bado unaweza kupiga show kama kawaida? Mara nyingi pre-diabetes huambatana na vimatatizo vya hapa na pale kwenye hiyo idara.

Fanya comprehensive physical exam ASAP. Mungu Akuponye kamanda 🙏🏿🙏🏿
 
Asante mkuu.
Pole sana kaka, Mungu akusimamie.
Nayasema haya out of experience ya bibi yangu ambaye alikuwa anapata Hali kama hii na madaktari wakashindwa kugundua kwamba chanzo ni sukari, alikuja kugundulika ni sukari too late baada ya kupatwa na kiharusi, na badae umauti ulimfika.
 
Yawezekana uko pre-diabetic. Bila kupoteza muda fanya vipimo vya sukari pamoja na presha. Pima pia kiwango cha lehemu (cholesterol) kwenye damu. Hii combo ni mbaya sana aisee na usiombe ukafika kwenye full blown diabetes na hypertension.

Nenda kwa daktari ukapime hivyo vipengele haraka sana. Kama bado hali inadhibitika basi atakushauri ubadilishe kabisa mfumo wa maisha yako. Kama unakunywa pombe na kuvuta sigara itabidi uache. Kama uko mnene itakubidi upambane sana upunguze uzito. Pia itakulazimu uushughulishe mwili kwa mazoezi hata kama ni kutembea kwa angalau dakika 30 kila siku. Ulaji wa nyama nyekundu, soda na mapochopocho mengine itabidi upunguze. Ni mboga za majani sana pamoja na matunda matunda -hasa yale ambayo hayana sukari nyingi.

Labda kama ni tatizo jingine lakini kama uko pre-diabetic unaweza kabisa kureverse hiyo hali kwa kubadili tu mfumo wa maisha. Usisubiri mpaka uanze kutumia dawa maana ukianza tu mara nyingi ndiyo hakuna kuacha mpaka siku unaondoka hapa duniani.

Vipi kuhusu sita kwa sita? Bado unaweza kupiga show kama kawaida? Mara nyingi pre-diabetes huambatana na vimatatizo vya hapa na pale kwenye hiyo idara.

Fanya comprehensive physical exam ASAP. Mungu Akuponye kamanda 🙏🏿🙏🏿
Shukrani mkuu. Ushauri wote utazingatiwa.
 
Yawezekana uko pre-diabetic au diabetic tayari. Bila kupoteza muda fanya vipimo vya sukari pamoja na presha. Pima pia kiwango cha lehemu (cholesterol) kwenye damu. Hii combo ni mbaya sana aisee na usiombe ukafika kwenye full blown diabetes na hypertension.

Nenda kwa daktari ukapime hivyo vipengele haraka sana. Kama bado hali inadhibitika basi atakushauri ubadilishe kabisa mfumo wa maisha yako. Kama unakunywa pombe na kuvuta sigara itabidi uache. Kama uko mnene itakubidi upambane sana upunguze uzito. Pia itakulazimu uushughulishe mwili kwa mazoezi hata kama ni kutembea kwa angalau dakika 30 kila siku. Ulaji wa nyama nyekundu, soda na mapochopocho mengine itabidi upunguze. Ni mboga za majani sana pamoja na matunda matunda -hasa yale ambayo hayana sukari nyingi.

Labda kama ni tatizo jingine lakini kama uko pre-diabetic unaweza kabisa kureverse hiyo hali kwa kubadili tu mfumo wa maisha. Usisubiri mpaka uanze kutumia dawa maana ukianza tu mara nyingi ndiyo hakuna kuacha mpaka siku unaondoka hapa duniani.

Vipi kuhusu sita kwa sita? Bado unaweza kupiga show kama kawaida? Mara nyingi pre-diabetes huambatana na vimatatizo vya hapa na pale kwenye hiyo idara.

Fanya comprehensive physical exam ASAP. Mungu Akuponye kamanda 🙏🏿🙏🏿
Utakuwa umepiga mlemle.
Mi pia miaka zaid ya mitano nyuma niliwahi shauliwa kula matunda yenye nyuzi na mengine kama hayo.Pia dalili ya ganzi hunitokea mara kwa mara ikiwa nitakaa ktk pose moja.
Show zangu 6*6 ni mbovu japo nisipotumia pombe kwa muda flan huwa zinaongezeka!

Kinachonishtua ni pale nkikojoa ardhin wale wadudu walamba mkojo huwa hawachelew kuufata na hii ni njia ya asili wengi huitumia kujitathmini juu ya diabet!

mtoa mada kama hiyo gazi ishazidi nenda mara moja kapime utapata majibu!
 
Yawezekana uko pre-diabetic au diabetic tayari. Bila kupoteza muda fanya vipimo vya sukari pamoja na presha. Pima pia kiwango cha lehemu (cholesterol) kwenye damu. Hii combo ni mbaya sana aisee na usiombe ukafika kwenye full blown diabetes na hypertension.

Nenda kwa daktari ukapime hivyo vipengele haraka sana. Kama bado hali inadhibitika basi atakushauri ubadilishe kabisa mfumo wa maisha yako. Kama unakunywa pombe na kuvuta sigara itabidi uache. Kama uko mnene itakubidi upambane sana upunguze uzito. Pia itakulazimu uushughulishe mwili kwa mazoezi hata kama ni kutembea kwa angalau dakika 30 kila siku. Ulaji wa nyama nyekundu, soda na mapochopocho mengine itabidi upunguze. Ni mboga za majani sana pamoja na matunda matunda -hasa yale ambayo hayana sukari nyingi.

Labda kama ni tatizo jingine lakini kama uko pre-diabetic unaweza kabisa kureverse hiyo hali kwa kubadili tu mfumo wa maisha. Usisubiri mpaka uanze kutumia dawa maana ukianza tu mara nyingi ndiyo hakuna kuacha mpaka siku unaondoka hapa duniani.

Vipi kuhusu sita kwa sita? Bado unaweza kupiga show kama kawaida? Mara nyingi pre-diabetes huambatana na vimatatizo vya hapa na pale kwenye hiyo idara.

Fanya comprehensive physical exam ASAP. Mungu Akuponye kamanda
Nilitaka nimshauri hivi pia

Kikubwa tunamuomba awahi hospital iliyokaribu nae apime sukari tena ikiwezekana apime mara tatu kwa siku moja
Asubuhi akiamka kabla hajala
Akapime akitoka kula
Apime pia na masaa 6 toka mara ya mwisho kupima

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom