Gamba la CCM limekwama shingoni?

Miruko

Senior Member
Feb 8, 2008
173
46

Reginald Miruko
Sekretarieti ya CCM inaendelea na kampeni mikoani kuhusu KUJIVUA GAMBA. Lakini ghafla wimbo wao umebadilika, chorus ya 'mafisadi ndani ya CCM' ikawa 'Mafisadi wa CHADEMA' wanaopimwa kwa kulipwa mshahara mkubwa.
Hivi sasa watuhumiwa wa ufisadi, hasa wale Mapacha Watatu wanachekea chooni, roho kwatuuuu! Mwisho wa siku mambo yatageuka, itakuwa ni biashara ya kuwashughulikia 'mavuvuzela, endapo watashindwa kujivua gamba na kuliacha mabegani kama picha hii www.rsmiruko.blogspot.com inavyoonesha.

Gamba.jpg
 
Mmh haya makubwa sasa. Tatizo ni kwamba ccm wameanza kupiga ngoma kabla wimbo haujatungwa matokeo yake wanaimba wimbo wowote. Walitakiwa kutunga wimbo ndio waweke beats.
 
NGWANANGWA anasema..... Tanzania: Nchi Pekee Duniani Ambayo Rais Wake Akiagiza Jambo Kila Mtu Aanajua Halitatekelezwa. Kama Hili la Kuwapa Mafisadi Siku 90. Kila Mtu Mwenye Akili Timamu Anajua Halitatekelezwa 100%..... JADILI
 
Umenikumbusha, aliagiza uzio wa mabati uliojengwa jangwani ubomolewe mara moja lakini mpaka jana ulikuwa bado kubomolewa
 
Umenikumbusha, aliagiza uzio wa mabati uliojengwa jangwani ubomolewe mara moja lakini mpaka jana ulikuwa bado kubomolewa
Wameshamsoma huyo wanajua ni kilele za purukushani za mende wala hata glasi haivunjiki, mafisadi....hatuoni wanachukuliwa hatua, barua alizosema Nape hazijatoka, magamba yamekwama shingoni hayavuliki...... wakivua ndo wamekwisha...
 
Mi ninavyojua wamejivua nguo wamebaki utupu cause kwa hali ya kawaida binadamu hatuna magamba, au kama vipi wao ni binadamu wa ajabu sana kiasi cha kuwa tofauti na wengine kwa kuwa na MAGAMBA.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom