Kauli mbiu mpya ya maandamano ya cdm-tanzania kujivua gamba la ccm | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kauli mbiu mpya ya maandamano ya cdm-tanzania kujivua gamba la ccm

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Ngonini, Jul 17, 2011.

 1. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #1
  Jul 17, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Wakuu,

  Nadhani kila mtu anaona jinsi watanzania wenzetu wananvyo danganywa na wanamagamba eti wanajivua gamba kwa kuwaomba baadhi ya watu kuachia vyeo ili kukisafisha chama.

  Magamba wanatumia mafisadi kama RACHAEL kuwa ndo watakaokifanya chama kiwe safi kama wataweza kuwashawishi kuachia vyeo walivyonavyo kwenye chama. Hivi RACHEL wakiondoka Lakini mafisadi wakubwa wakabaki kuwa ndo wajumbe wa kudumu wa cc, tunawezaje kusema ccm imekuwa safi? Nani asiyejua kuwa ufisadi mkubwa ilikuwa kwa ajili ya kufanisha shughuli za chama na haikuwa wizi wa watu fulani tu? RA angekuwa na uwezo wa kuyasema yaliyoko moyoni mwake juu ya Epa,kagoda nani ndani ya chama angethubutu kuonyesha sura yake mbele ya watatnzani kwa aibu hii kubwa? Je EL akiamua kumwaga mboga nani atakubali aibu hii?


  Wananchi wenye upeo wa kupambanua mambo wananweza kuona usanii unaofanywa na hawa jamaa wa kufanya maelewano na baadhi ya watuhumiwa ili kuwagiribu watanzania kuwa sasa wameshakuwa safi na wanastaili kuendelea kuaminiwa.

  Huu ni mtandao wa ulaji ambao sasa umemeguka katika makundi madogomadogo yanayojaribu kuwavutia watu kwa giriba mbalimabli. Tumeona lile kundi lililokwenda mbeya jana likijaribu kujikosha ili waonekane wao ni safi kuliko wenzao na pengine wanajiandaa kwa 2015.


  Nina washauri CDM wavuruge sasa hii dhana ya kujivua gamba ambayo imelenga kuwalaghai watanzania ili watu walewale waendelee kututafuna. CDM kinachotakiwa sasa ni TANZANIA KUVUA GAMBA LA CCM ili nchi izaliwe upya.

  Matapishi, huwezi kuyawekea viungo na kuyafanya chakula tena. Tunahitaji mwelekeo mpya na sikung'ang'ania mfumo ambao hautupeleki tunakokwenda badala yake unatumiwa na wachache kuwafaidi walio wengi.  Mungu ibariki Tanzania na watu wake wema!
   
Loading...