Kikwete na Porojo za CCM Kujivua Gamba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete na Porojo za CCM Kujivua Gamba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by OgwaluMapesa, Jun 2, 2011.

 1. O

  OgwaluMapesa JF-Expert Member

  #1
  Jun 2, 2011
  Joined: May 24, 2008
  Messages: 10,948
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  NI vigumu kuamini kwamba rais wa nchi anaweza kuhusika na mchezo mchafu kama huu wa kuwabagua wananchi wake kwa misingi ya dini zao, lakini matukio ya hivi karibuni yanathibitisha hilo.

  Baada ya uchaguzi mwaka jana na hasa tukio la Arusha la Watanzania kupigwa na polisi kwenye maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), na kisha harufu ya udini kuibuka, baadhi ya Waislamu wachache wenye mtazamo mkali walianza kuzunguka nchi nzima wakitoa mahubiri ya chuki.

  Mkutano mmoja ulifanyika kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam na inadaiwa ulipata baraka za Kikwete. Baadhi ya mikutano hiyo ilijadili masuala tata, na baadhi ikaibuka hata na mapendekezo ya ajabu ukiachilia yale ya muda mrefu kama vile kudai Mahakama ya Kadhi na Tanzania kuingia kwenye Jumuiya ya Kiislamu Duniani (OIC).

  Madai mengine yalihusu malalamiko kwamba Wakristo wamekuwa wakipendelewa tangu enzi za ukoloni na kwamba ingawa Waislamu ni wengi zaidi Tanzania, lakini hawana nafasi nyingi za madaraka. Madai mengine yaliyotolewa ni kwamba Wakristo wana shule na mahospitali lakini Waislamu hawana, na kwamba serikali hutoa fedha kuzisaidia hospitali za Wakristo na walimu wa kufundisha shule za Wakristo, lakini Waislamu wanaachwa hivi hivi tu.

  Baadhi walifikia hata hatua ya kumlaani Mwalimu Nyerere na kusema kwamba hastahili kuitwa Baba wa Taifa; bali anastahili kuitwa Baba wa Kanisa Katoliki. Baadhi yao, akiwemo kigogo wetu, hawamwiti Mwalimu Nyerere kwa hadhi yake iliyozoeleka ya Baba wa Taifa, na badala yake humwita Mzee Nyerere.

  Kwa ufupi, kuna imani kubwa miongoni mwa Watanzania kwamba utawala wa Rais Kikwete unalea udini, na asipokuwa makini nyufa hii yenye msingi wa kidini inaweza kupanuka na kuutia dosari umoja wa kitaifa tulionao ambao misingi yake si udini.

  Geresha ya kujivua gamba

  Pamoja na kubadili safu ya uongozi mjini Dodoma, CCM pia ilitangaza kwamba wanachama wake watatu wanaotuhumiwa kwa ufisadi wajiondoe wenyewe; la sivyo wataondolewa kwa nguvu. Wanachama hao wanatajwa kuwa ni Waziri Mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa, na wabunge wawili, Andrew Chenge na Rostam Aziz. Ni kweli matajiri hawa hawapendwi na Watanzania wengi isipokuwa pengine wa majimboni mwao tu.

  Lakini pia watu hawa watatu wana sifa nyingine: Kwamba ndio tishio pekee na la kweli dhidi ya mpango wa Kikwete wa kusaka mgombea urais wa mwaka 2015 ambaye ni Mwislamu. Wanaotaka kumweka Lowassa kwenye urais mwaka 2015, si tu wanakwamishwa na tuhuma hizi zinazomwandama na hatihati hii ya kung'olewa CCM, lakini pia wanakwazwa na Kikwete mwenyewe. Inadaiwa kwamba, kwenye mbio za urais za 2015, tatizo la Kikwete kuhusu Lowassa si kwamba anakabiliwa na tuhuma za ufisadi; bali kwamba si Mwislamu.

  Kundi hili la kina Lowassa inaaminika lina urafiki wa karibu na Makamba ambaye inadaiwa kuwa agenda yake kubwa kwa mwaka 2015 haikuwa udini; licha ya kuwa naye amesikika mara kadhaa akilumbana na maaskofu; bali yeye (Makamba) ana ndoto ya mwanae (January) aje kuachiwa urais mwaka 2025 na kundi hili. Makamba hutamba kwamba mwanae anafaa kuwa kiongozi, na hakuna ubishi kwamba alihakikisha mwanae anapata ubunge, uenyekiti wa kamati ya Bunge, na kisha kuingia kwenye Sekretarieti ya CCM.

  Aidha, mtoto huyo wa Makamba pia anaelezwa kuwemo kwenye kundi linalowaunga mkono watuhumiwa hawa wa ufisadi ambalo lina idadi kubwa ya wabunge na viongozi wa CCM wa ngazi za wilaya, mikoa na taifa. Hii ndiyo sababu tangu CCM ilipoanza kushambulia mafisadi hadharani, yeye amepotea jukwaani!

  Kimsingi, kuna kutofautiana kati ya Makamba na Kikwete kuhusiana na nani awe rais mwaka 2015 na kuhusu nini wafanyiwe hawa watuhumiwa wa ufisadi. Hivyo; tangazo la kujivua gamba pamoja na kutajwa kwa watuhumiwa hao ambao Kikwete mwenyewe aliwapigia kampeni mwaka jana kwenye uchaguzi wa wabunge, ni geresha tu. Ukweli ni kwamba Kikwete alikuwa anaunda timu itakayomrithi mwaka 2015.

  Kimsingi, hadi sasa Kikwete ameshawaacha ‘wabaya' wake wote nje ya Kamati Kuu ambao ‘dhambi' yao kuu ni kuutaka urais wa mwaka 2015. Watu hao ni pamoja na Membe na Andrew Chenge ambaye anamtaka Lowassa.

  Kwa ufupi, janja hii ya Mwenyekiti Kikwete ya "kujivua gamba" ililenga katika kuwaengua wale wote wanaoweza kumsumbua kwenye suala la urais wa mwaka 2015; ingawa pia ni kweli kwamba ukiuangalia juujuu utaona kuwa mpango huo wa "CCM kujivua gamba" unalenga katika kupunguza nguvu za CHADEMA kwa kuirejeshea CCM mvuto wake wa zamani.

  Vyovyote vile; hakuna ushujaa wala maamuzi magumu yaliyofanyika Dodoma. Ulikuwa ni ‘usanii' tu, na ndiyo sababu hakuna kiongozi wa CCM anayepigia kelele kung'olewa chamani mafisadi zaidi ya kijana Nape na Katibu Mkuu mpya, Wilson Mukama ambao, hata hivyo, nao wamefungwa "gavana" hivi karibuni kuhusu kulipigia debe suala hilo. Hata Chiligati aliyejitokeza mwanzoni kuhubiri nia ya kuwavua uongozi wa CCM kina Lowassa, Rostam Aziz na Andrew Chenge, sasa naye ameingia mitini!

  Kauli ya Joseph Butiku

  Labda nigusie pia kidogo kuhusu malalamiko ya Joseph Butiku aliyoyatoa katika mahojiano na gazeti la Raia Mwema, hivi karibuni, kwamba viongozi wa CCM wamemwachia Mwenyekiti Kikwete mzigo wa kupambana na mafisadi.

  Mimi nadhani madai hayo ya Butiku ameyatoa bila kujua ukweli wa mambo. CCM haiko kwenye mapambano na mafisadi; bali Mwenyekiti Kikwete ndiye anapambana na maadui zake kwenye kinyang'anyiro cha kutafuta mrithi wake kwenye Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015; ila tu amepata bahati kwamba watu hao hao ndio wanaolalamikiwa kwa ufisadi. Ni bahati tu ya mtende iliyotoa fursa ya ‘usanii' huu kuchezwa!

  Aidha, kelele za CCM kupitia kwa Nape kwamba kuna vyombo vya habari, viongozi wa Upinzani na viongozi wa dini ambao wamepangwa kuwatetea mafisadi na kuishambulia familia ya Kikwete, ni janja ya kuwatangulia mbele ili wakisema jambo, wananchi waambiwe: "Si tulisema, mnaona sasa!?"

  Hata hivyo, inafahamika kuwa makundi haya matatu ndiyo yako mstari wa mbele kupinga ufisadi na udini unaosambazwa na Kikwete na watu wake, hivyo lolote litakalosemwa halitakuwa geni; bali ni muendelezo unaofahamika. Pengine CCM haijui kuwa wananchi wanajua kinachoendelea.

  Wagombea wa Kikwete 2015

  Kwa kufuatilia mambo ya kisiasa yanavyokwenda na jinsi Rais Kikwete anavyoendesha mambo yake, kuna majina mawili ya watu wanaotajwa ambao angependa wachukue urais na umakamu wa rais wa Muungano mwaka 2015. Hii inatokana pia na imani yake kwamba Katiba mpya haitabadili mfumo wa sasa.

  Sababu kubwa ni mbili: Kwanza, kutekeleza ahadi yake ya siri kwamba hawezi kuacha nchi kwa Mkristo; na pili, kuhakikisha uongozi mpya unamlinda yeye na familia yake dhidi ya misukosuko ya hapa na pale ambayo kawaida kote duniani hutokea mtu akishaacha urais. Hakika, naye hatapenda kushambuliwa kama inavyotokea kwa Mkapa.

  Baada ya kufanikiwa kuwaengua pembeni Lowassa na Membe (Prof. Mwandosya kanusurika?) ni nani, basi, ambaye Kikwete anamtaka kwa urais wa 2015 na atachezaje karata zake kuhakikisha jina la mtu huyo linapeta?

  Ili watu hao wawili anaowataka wakubalike, inaaminika kuwa Kikwete atatumia mtindo ule ule wa funika kombe mwanaharamu apite. Atawapendekeza kwa kutumia vigezo vinavyoficha ukweli. Kutokana na hali ya kisiasa itakavyokuwa, anaweza kusema: "Jamani ni zamu ya wanawake sasa, tusitawale akina baba tu, nchi yetu wote."

  Iwapo wazo hili litakwama, basi, Kikwete anaweza kusema hivi: "Jamani sasa wenzetu wa Zanzibar nao, miaka 20 imepita, tuwape nao nafasi jamani." Msemo huu, hata hivyo, hauna mashiko iwapo Katiba haitakuwa na agizo hilo; kwani upande wa Upinzani unaweza kuweka wagombea wote wa Bara.

  Mbinu hiyo Kikwete ameshawahi kuitumia kwenye kujaza nafasi ya Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana ambapo alimpendekeza kijana wa Visiwani, na pia aliitumia kwenye kupata jina la mgombea wa uspika. Anaamini kuwa mbinu hiyo itasaidia kufunika hoja yake ya udini isionekane, na hivyo kufanikisha kupata rais Mwislamu.

  Asha-Rose Migiro na Dk. Mwinyi

  Katika miaka ya karibuni Kikwete amekuwa na mahusiano ya karibu ya kikazi na mwanamama mmoja ambaye kila baada ya miezi michache hufika Ikulu, na kisha picha nyingi hupigwa kuonesha kwamba wawili hao wanaelewana na wanashirikiana kisiasa pia.

  Huyu ni mwanamama ambaye ni mmoja wa wanasiasa wachanga waliofaidika na vyeo vya uwaziri wa Kikwete mwaka 2005. Aidha, pale Tanzania ilipopewa mwanya wa kutoa jina la mwanamke wa kushika nafasi ya juu kimataifa, Kikwete hakusita kumtaja mwanamama huyu.

  Nafasi hii ilikuwa baada ya Tanzania kufanya kampeni kubwa barani Afrika kuunga mkono jina la Waziri wa Mambo ya Nje wa Korea Kusini, Ban ki-Moon, kwenye kugombea nafasi ya ukatibu mkuu wa Umoja wa Mataifa.

  Mwanamama huyo pia ana kisomo kizuri kinachokubalika na kinachoweza kuwaaminisha watu wanaotaka kuuliza maswali kuhusu uwezo wake kiutendaji wa kuiongoza nchi yenye matatizo ya uchumi na yenye mipasuko kibao kama Tanzania. Mwanamama huyo ni Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Dkt. Asha-Rose Migiro ambaye anaelezwa kuanza kujiandaa kurejea nyumbani Tanzania siku si nyingi.

  Kwa upande wa Zanzibar, ni waziri mmoja kijana ambaye urafiki wake na Kikwete huwashangaza viongozi wengine wa Zanzibar; mathalani jinsi wanavyosalimiana kama watoto wa mjini. Katika mtandao wa YouTube Watanzania waliweka picha ya video ya Kikwete akisalimiana ‘kishkaji' na waziri huyu kwenye Uwanja wa Amani, Zanzibar siku ya Januari 12, mwaka huu. Picha hiyo iliibua gumzo kubwa.

  Hivi karibuni Waziri huyu alipokabiliwa na msukosuko wa kutakiwa na wananchi kwamba ajiuzulu ambao kimsingi ulisababishwa na utendaji dhaifu wa Jeshi la Wananchi uliochukua maisha ya watu kwenye milipuko ya maghala ya silaha, alikataa na Kikwete hakusema kitu. Huyu ni Waziri wa Ulinzi, Dkt. Hussein Mwinyi.

  Hitimisho langu

  Inaaminika kuwa hao wawili ndio chaguo la Kikwete katika mbio za urais za 2015, na chaguo lake hilo linachagizwa zaidi na dini zao badala ya vigezo vya jumla vya sifa ambazo Watanzania wote tunataka mtu anayetaka kuwania urais kuwa nazo.

  Hata hivyo, napenda nieleweke kwamba sina tatizo na rais ajaye kuwa Mwislamu au Mkristo; ilimradi tu awe ni kiongozi hodari, mchapakazi, mwadilifu na mwona mbali. Angalizo langu ni kwamba rais huyo ajaye asitafutwe kwa msingi wa dini yake; bali kwa vigezo hivyo vya ubora.

  Nasisitiza hivyo; maana Watanzania katika ujumla wao hawajali dini ya mtu ila uadilifu na uchapakazi tu, lakini viongozi wetu ndio wenye matatizo ya udini. Na kwa hakika, Kikwete analo tatizo hilo.

  Nihitimishe kwa kusisitiza kwamba wajibu wa wana-CCM ni kukisafisha chama chao kwa uaminifu na werevu, na kisha kuachia demokrasia iamue nani awe mgombea wa CCM mwaka 2015. CCM na Kikwete wawe waangalifu na dhana hii ya "sasa ni zamu yetu kutawala" ili Tanzania isitumbukie kwenye matatizo yanayosikika kwenye nchi zingine.
   
 2. a

  allydou JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2011
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 1,484
  Likes Received: 567
  Trophy Points: 280
  sin uhakika kama husein mwinyi ana nguvu ya kuweza kukubalika CCM, lakini huyo mama nyota yake inaonekana kun'gaa sana, isitoshe kikwete yupo karibu sana na akina mama, anapendelea sana akina mama katika shughuli zake, hapo chochote kinaweza kutokea
   
 3. A

  Akiri JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2011
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,447
  Likes Received: 62
  Trophy Points: 145
  nimemsoma huyu mwandishi tangu ile makala yake ya kwanza jamaa ameongea mambo mengi mazito rakini bado napata shida na sisi watanzania tutakuwa waoga mpaka lini? sasa mwandishi unaandika mambo magumu then unaficha jina lako? kwa nini usiwe wazi kama mpiganaji Asbert ngurumo?

  nimeisoma kwa umakini sana makala ya huyu mkuu na kila alichokisema ni kweli tupu. lakini niseme punguza jazba chama chenu kimekufa hata huwo urais wa 2015 sijui kama mtapata coz CDM wapo juu nani anataka kusikia habari za ccm leo hii ?
   
 4. MANAMBA

  MANAMBA Senior Member

  #4
  Jun 2, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 169
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Uandishi wake una kila dalili ya kutumiwa na kikundi fulani
   
 5. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #5
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  No!!! c suala la kutumiwa na kikundi, hivi kwa nn hatuamini mtu independently anaweza kuwa na fikra kama hizi? Anyway mwandishi ana logic kubwa sana katika makala yake. Mambo haya anayozungumza ni kweli, sema ni vile naamini by that time watz wote watakuwa washafunguka vichwa hawataburuzwa kihivyo. Big up! mwandishi wa makala
   
 6. mmbangifingi

  mmbangifingi JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2011
  Joined: Mar 9, 2011
  Messages: 2,855
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  ufisadi anaotajwa kuufanya lowassa hakuna jk asichojua na alifaidika nao. halikadhalika chenge na rostam. kama ni kujivua gamba kwa nn uishie tu kuwafukuza chamani badala ya kuwapeleka jela na kufilisi mali zao? its apparently issue ni urais 2015 hata kama c lowassa kuuchukua basi kuhakikisha amewapunguza/amewaondolea nguvu ya ushawishi kwa kuwaweka mbali na nec/kamati kuu.
   
 7. The Good

  The Good Senior Member

  #7
  Jun 2, 2011
  Joined: May 26, 2010
  Messages: 152
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Asha-Rose bado ni mwislamu?
   
 8. FarLeftist

  FarLeftist JF-Expert Member

  #8
  Jun 2, 2011
  Joined: Oct 20, 2010
  Messages: 362
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  udini ni nini?
  mimi kama Mtanganyika sijui lolote kuhusu udini wala sina haja ya kujua
   
 9. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Ni ukweli usio fichika tena kuwa ombwe la uongozi wake toka achaguliwe kuwa rais mwaka 2005 ndio linamfanya atumie mambo ya udini kama kichaka cha kukimbilia mara anaposhambuliwa kuwa kazi imemshinda!! Hata hivyo maadam amefanikiwa kuchakachua na kupata kipindi kingine cha miaka mitano sasa akili yake yote iko kwenye maisha yake baada ya ngwe hii na jinsi atakavyohakikisha kuwa hapati taabu kama wanazopata marais wengine wezi barani Africa ya yeye na ukoo wake kushwekwa lupango; hivyo basi kazi yake kubwa sasa ni kumtafuta mrithi atakayesitiri uchafu wake mara baada ya kutoka madarakani. Naamini mtu yeyote atakayejulikana kuwa ni chaguo la Kikwete kama ndio mrithi wa kiti chake wananchi hawatamchagua kutokana na rekodi yake mbovu ya utendaji.
   
 10. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Mkuu usifikiri sheikh Osama alikuwa hapendi kutumia simu, alikuwa na sababu. Hoja aliyoongea mwandishi ni kweli ni nzito hivyo watu kama hao wanatafutwa sana kuanzia na system yenyewe unaweza kufa hivi hivi? Jiulize yule Prof. alipigwa risasi alipotaka kuingia ndani alikuwa wakili alipenda, nakujuza tu inasadikiwa alimuona Dr. Balali ambaye yeye alikuwa classmate wake hivyo siyo rahisi kumfanananisha live USA habari zilipolink hakukawia na jamaa hawajakamatwa hadi leo, na wananchi wakipigwa changa la kuwa wauaji ni majambazi! Majambazi mara nyingi yana hunt money, lakini siasa nakuhakikishia unakupoteza muda si mrefu endapo usipokaa vizuri. Vita hii ni pana na ngumu kuliko unavyofikiri.
   
 11. mfereji maringo

  mfereji maringo JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2011
  Joined: Nov 19, 2010
  Messages: 1,003
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Nahisi umetumwa na Lowasa, sasa kamwambie kuwa hatoukosa urais kwa sababu ya dini yake, bali ataukosa uraisi kwa wizi wake, kama unabisha kamuulize nyerere.

  kisha tueleze kuhusu Asha Rose Migiro je hafai kuwa raisi kwa sababu yeye ni mwislam? hivyo si vyema waislamu wawili kufuatana kuwa marais?au anamapungufu ya kiutendaji
   
Loading...