Kikwete anataka chama kiongozwe na nani? Kwa faida ya nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Kikwete anataka chama kiongozwe na nani? Kwa faida ya nani?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by KAMBOTA, May 5, 2011.

 1. K

  KAMBOTA Senior Member

  #1
  May 5, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mwenyekiti wa CCM Jakaya Kikwete anasema anataka chama kirudi mikononi mwa wanyonge hivyo ili kufikia azma hiyo akaendesha ile operation butu inayokwenda kwa jina la "operation vua gamba"
  Kuna udhaifu mkubwa sana tena wa wazi kabisa mfano kwa takribani miaka sita ya uongozi wa Kikwete waandishi mbalimbali wa aina ya Saed Kubenea walipofunua ufisadi na kuitaka CCM iwashughulikie wajibu hoja wa CCM hawakusita kusema kuwa ufisadi ndani ya chama hiko haupo na hata ikiwa upo basi hauhusu chama bali mtu mmoja mmoja na pasipo kusoma alama za nyakati Kikwete alipita majimboni akawanadi tena kwa kuwainua mikono baadhi ya hao mafisadi huku akiwaita rafiki na wachapakazi wapenda nchi nao wakalaani mchezo huu wa kitoto lakini kama kawaida wakaibuka wapangua hoja wa CCM wakamdanganya Kikwete na kumwaminisha kuwa hakuna ubaya wa yeye kufanya hivyo.
  Lakini hofu imetanda mara baada ya chama kuendelea kuyumba na serikali kushindwa na huku vyama vya upinzani vikiendelea kuvuta hisia ya walalahoi kwa jinsi vinavyoikosoa serikali ya CCM , ndipo katika vuta nikuvute hii ikaibuka falsafa ya Kikwete ya kujivua gamba ambayo ilianza kwa mbwembwe kubwa lakini kadri muda unavyoenda kuna kila dalili kuwa nyota inazidi kufifia.
  Nayasema haya kwasababu inaelezwa kuwa kule Dodoma mwenyekiti aliwahimiza wapenda chama chao kusema ukweli bila kificho na kuahidi kuwashughulikia mafisadi hali iliyowapa moyo kina wazalendo wa chama hiko kuanza kusema ukweli bila kificho na kuwataja wanaotuhumiwa waziwazi haikutosha Kikwete alienda mbali zaidi akawapa moyo viongozi wapya hasa Nappe Nauye, kapteni Chiligati na Mukama kuwa wachape kazi pasipo woga na ni lazima maazimio yaliyofikiwa yatekelezwe bila kificho.
  Kabla msamiati wa kujivua gamba haujatoweka kwenye ndimi za watanzania tayari udhaifu mkubwa umeanza kujitokeza katika kuwashughulikia mafisadi tena badala ya mafisadi kuyumba sasa ni CCM yenyewe ndiyo inayumbishwa sana, nitaeleza kwa misingi ya hoja hata ikibidi kujibiwa pia iwe kwa misingi ya hoja;
  Kwanza makundi ndani ya chama yameongezeka sana ,hatua ya kutaka kuwatimua watuhumiwa wa ufisadi imezua makundi ya kiitikadi na kimtandao ambayo yanazidi kuitikisa CCM, kundi la kiitikadi ambalo ndiyo baya zaidi ni lile linaloamini katika chama ni mali ya wakulima na wafanyakazi hivyo ni lazima mafisadi watemwe ili kirejeshwe kwa wenyewe na kundi lingine linaamini kuwa chama ni cha wote na hivyo uwezo wa kipesa utaamua nani mwenye nguvu hivyo mtu kutuhumia ufisadi kwao sio kitu na kwa upande mwingine minyukano ya kimtandao nayo imezuka huku kukiwa na mtandao wa wmakomandoo wa operation vua gamba ambao bilashaka ni Nappe na Chiligati huku kwa upande mwingine wa wale wasiofahamu hata gamba ni nini hasa? na wengine wanaona huo ni uonevu mkubwa!
  Akinukuliwa na vyombo vya habari hapa nchini mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini alisema kuwa mafisadi ndani ya CCM sio watatu pekee bali ni wengi zaidi huku akienda mbali kwa kudai kuwa wananchi wanaamini pesa za EPA zilitumika kwenye uchaguzi wa mwaka 2005 na CCM haijawahi kukana hili je kwanini basi watu wasiamini hata serikali iliyoko madarakani ilisaidiwa na mafisadi? Hivyo alisisitiza ikiwezekana hata mwenyekiti wa CCM na yeye ang'oke lakini kuwatoa watatu ni mchezo wa kitoto.
  Watafiti wa mambo wameanza kushangaa kufuatia "lugha gongana" inayoendelea ndani ya sekretarieti mpya ya CCM huku wakisema Nappe katumwa au kajituma? Kulikuwa na haja gani ya yeye kuongea kikakamavu kuwashughulikia mafisadi kisha kushindwa kusaini barua hizo? Moja ya magazeti yaliyojizolea umaarufu nchini linalotoka siku ya jumatano linaandika kuwa sasa barua za kuwatimua watuhumiwa ni kama yai kila mtu anamrushia mwenzake hataki limpasukie mikononi naam! Mara ziko mezani kwa Msekwa, mara kwa Mukama, ooh kwa Nappe baadaye kwa Chiligati na sasa wanadai ziko kwa mwenyekiti wa chama, huku kote hazijasainiwa kwanini? Wanaogopa nini?
  Ndiyo maana watu wameanza kuhoji Nappe anapambana na nani? Kwa maslahi ya nani? Mbona kamanda mkuu haonyehi kuwa amemtuma msaidizi wake huyo kufanya operation hiyo? Ingawa anazungumza kwa maneno lakini kimatendo yupo kimya kwanini? Wengine wameenda mbali kwa kuweka wazi kuwa CCM inaandaa uadui miongoni mwa wanachama wake kwa madai kuwa watu walijikakamua mbele ya mwenyekiti kule Dodoma wakasema ukweli wakidhani kuwa kweli ipo nia ya dhati ya CCM kuwatimua watuhumiwa lakini kwa jinsi uoga mkubwa ulivyotanda ndani ya chama hiko kiasi kwamba hata kusaini barua imekuwa kazi wazalendo hao wameanza kuhofu kuwa wao sasa ndiyo wataonekana maadui wa hao watuhumiwa wa ufisadi wengine wameenda mbali kwa kudai kuwa wamechonganishwa bure na hao watuhumiwa kwani hakuna dalili za dhati za kuwashughulikia.
  Kama kweli CCM ilikuwa na nia ya ddhati hakukuwa na haja ya kina Nappe na Mukama kuanza ngonjera za kitoto za sio siku 90 bali 120 mara ooh mpaka kikao kingine, mara hatukupeana siku , mara mtu ukioga ni lazima uoge mwili mzima, haya yote ya nini? wananchi wameikinai CCM kwa kuwa wanaamini chama hiko kinalea mafisadi suluhisho ni kuwatosa bila chembe ya huruma sasa hizi lugha gongana zinatoka wapi? au walikuwa wanapima kima cha maji? Sasa wameona ni mengi watazama hivyo wameanza visingizio?
  Katika timbwili hili watu walitegemea kuona mwenyekiti wa CCM akijipambanua kwa maneno na vitendo kuwa kweli ameamua kuijenga upya CCM kwa kupambana na ufisadi lakini wapi bwana! Haonyehi kwa matendo ingwaje anazungumza kwa maneno, hii maana yake nini? je Kikwete amemwachia nani aongoze CCM? na kwa faida ya nani? Au anataka tuamini kuwa Kikwete ni mfuasi wa imani kuwa "mafisadi watajimaliza wenyewe" kama baadhi ya wachambuzi wanavyodai? Tusemaje basi ? Naam! Kwa mbali naona Kikwete ameona pale ambapo Nappe na Chiligati hawajaona, bilashaka luteni huyu wa jeshi japo hajawaambia wana CCM wenzake lakini kuna kila dalili kuwa amebaini ukweli kuwa ufisadi ndani ya CCM ni mfumo rasmi ambao umechelewa tu kutangazwa lakini siyo tatizo la watu wtatu maarufu kama mapacha watatu kama baadhi ya wanapropaganda wa CCM wanavyotaka kuwarubuni watanzania. Tungoje tuone!

  Nova Kambota Mwanaharakati

   
 2. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #2
  May 5, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,674
  Trophy Points: 280
  Ccm haina haki ya kuongoza nchi hii,imeshashindwa na wao wanajua hilo,muda wao unahesabika
   
 3. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #3
  May 5, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180
  Dalili ya mwisho kabisa ya dola kusambaratika ni kuanza kufitiniana yenyewe!
  Vita ya panzi hii, na itakuwa ni mbaya kuliko maelezo, maana imebuniwa na mtu akiwa kasimama jukwaani, bila kushauriana na wenzake!
   
 4. kisu

  kisu JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 802
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Chama cha Magamba!!! Chukua Chako Mapema!!!
   
 5. MANI

  MANI Platinum Member

  #5
  May 5, 2011
  Joined: Feb 22, 2010
  Messages: 6,410
  Likes Received: 1,863
  Trophy Points: 280
  Ufisadi ni mfumo ndani ya CCM na ni vigumu kubadili mfumo huo bila kuathiri uwepo wake. Na kwa hili naona CCM hawawezi kuwajibishana kama ambavyo wanatangaza, hii ilikuwa ni njia ya ku buy time ili watu wasahau na kurudisha imani lakini kwa hali halisi ya sasa hivi huu wimbo wa kujivua gamaba utawadodea !
   
 6. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Chama cha Misukule.
   
Loading...