Daudi Mchambuzi
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 62,204
- 128,022
Kwa kweli ni bora nionekanane sina moyo wa uzalendo kwa kusikitishwa na kifo cha Baba wa Bara.Katika vita kati Tanzania na Uganda Libya ikiwa chini ya utawala Gaddafi ilitoa msaada wa kijeshi kwa nchi ya Uganda. Kutokana na msaada huo mamia ya watanzania waliokuwepo kwenye maeneo yalivamiwa na Uganda ( wakati huo ikiwa chini ya utawala wa Idi Amin Dada) walipoteza uhai wao. Hivyo leo hii mtanzania ambae anasikitishwa na kifo cha Gaddafi hana moyo wa kizalendo. Au mnasemaje wanaJF kuhusu mtazamo wangu?