Mkuu, nilishawahi kusema mara kadhaa kwamba kwamba ukiona nimepotoka niwashe tu usione aibu.
Sasa, hebu jiulize. Ilani ya ccm na Chadema wanaomba tuwachague ili watuboreshee huduma za jamii na uchumi. Ukimpeleka dr Slaa kwenda kugombea urais Libya, ilani yake itakuwa nini? Uchumu tulivu, huduma za jamii bure na bora kuliko hata marekani.
Hivi gaddafi na JK ni nani dikteta? Saddam na Bush nani alikuwa dikteta? Statistically, Gaddafi is an outlier, yaani, an awkward case. Usitumie theorie ambazo wengine wote wamefiti.
Kama ikitokea wakamuondoa madarakani Libyans watakuwa wameruka mkojo kukanyaga mavi
wewe bado una mawazo ya kitoto kabisa, hivi unajua maana ya dictator au unataka tu kuleta utani?
mtu umetawala miaka 42 , hata kama umeleta mazuri yapi kumbuka kuwa watu watakuchoka tu.
Na ninataka kukuhakikishia kuwa sio kweli kwamba Libya is far better than other countries ,eti unathubutu kujaribishia na USA?
are u joking?
kule hakuna kazi, maisha ni magumu?
kuna matabaka ya walio nazo na waio kuwa nazo
kuna matajiri kweli kweli
na kuna masikini wa kufa mtu
kweli huduma za afya ni za bure lakini huduma zake zinasemekana ni mbaya sana kwani hakuna madawa , madaktari na vitu vingine
hivyo ni jina tu
Kama uliona hotuba ya mtoto wake ya juzi utaamini ninalokuambia, alijaribu kuwashawishi wananchi na kuwaambia kuwa kwa sasa tumeweka 200bln dolars kwa ajiri ya miradi mbali mbali , maana yake ni kuwa miradi mingi iko chini ya mawe...
Kukosekana haki na uhuru kwa wananchi ni tatizo jingine.
Huwezi kunieleza eti kisa unanipa chakula,matibabu bure ndio unikataze kupata mawasiliano na nchi zingine, unikataze kuwa na media, unikataze uhuru wa kuongea na mengine.
Hivyo wana Libya sio vichaa wala wajinga, wanajua kila wanachofanya wala hawabahatishi.