Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,330
- 33,139
Kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi Saturday, September 05, 2009 2:58 AM
Kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi anajiandaa kuliomba baraza la umoja wa mataifa liifute kwenye ramani ya dunia nchi ya Uswizi na ardhi yake igawanywe na kupewa majirani zake. Kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi amesisitiza msimamo wake wa kulitaka baraza la Umoja wa mataifa liifute kwenye ramani ya dunia nchi ya Uswizi na kisha ardhi yake igawanywe na kupewa majirani zake nchi za Italia, Ufaransa na Ujerumani.
Gaddafi anajiandaa kuwakilisha wazo lake hilo wakati Libya itakapoanza zamu yake ya urais wa baraza la umoja wa mataifa kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia septemba 15 mwaka huu, liliripoti gazeti la Daily Mail la Uingereza.
Gaddafi aliwahi kuliwakilisha wazo lake hilo kwenye kikao cha mataifa manane makubwa G8 kilichofanyika nchini Italia mwezi julai mwaka huu.
"Uswizi ni mafia wa dunia na haiwezi kuhesabika kama nchi" alisema Gaddafi kwenye kikao hicho.
"Uswizi inaundwa na jumuiya ya kiitaliano ambayo inabidi irudi Italia, jumuiya nyingine ya kijerumani inabidi irudi Ujerumani na jumuiya ya tatu inatoka Ufaransa inabidi irudi Ufaransa" alisema Gaddafi.
Waziri wa mambo ya nje wa Uswizi alisema kwamba mawazo hayo ya Gaddafi ni mawazo yake binafsi katika kampeni yake ya kupingana na Uswizi.
Uhusiano wa Uswizi na Libya ulitetereka baada ya mtoto wa kiume wa Gaddafi, Hannibal, 33, na mke wake mjazito walipokamatwa na kushikiliwa kwa muda na polisi wa Uswizi mwaka jana baada ya kumshambulia mfanyakazi wa hoteli waliyokuwa wamefikia.
Waliachiwa baada ya siku mbili baada ya kesi yao kufutwa lakini Gaddafi aliamua kulipa kisasi kwa kuondoa kiasi cha dola bilioni tano kutoka kwenye benki za Uswizi pamoja na kuvunja mikataba ya biashara na Uswizi.
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=3000934&&Cat=2
Huwezi kuchanganya personal issues na business. Sasa kama mtoto wake alimpiga mhudumu wa Hotel alitakiwa afikishwe kwenye vyombo vya sheria. Waafrika tunapenda kujikuza sana pale tunapokuwa tuna madaraka. Huyo mhudumu naye ana haki zake ambazo zinatakiwa zilindwe. Kama hizo bilioni 5 alizoondoa kwenye akaunti Uswizi zilikuwa ni zake na familia yake siwezi kumlaumu, lakini kama zilikuwa ni za serikali yake nitamuona mpumbavu tu.
Jamani naona hapa ni kwa sababu tu amezungumza Ghadafi ambaye baadhi yetu hatumpendi kwa sababu fulani fulani, lakini kwa kifupi Uswis ni nchi ambayo imekuwa chaka la mafisadi duniani kwa miaka mingi sasa. Mafisadi wa dunia wanaishi maisha bora sana wanapokuwa huko. Wengine wanaishi milimani wakipata ulinzi bora kabisa wa serikali ya Uswisi. Nchi hiyo imepata utajiri na itaendelea kutajirika kwa mitaji ya fedha zetu kutoka nchi masikini. Hawawezi kubadilika, maana wanahubiri demokrasia na utawala bora kwetu huku wao wakikumbatia wahalifu kutoka kwetu. Jamani kama wakigawanywa itakuwa afadhali maana kuna afadhali kubwa sana kati ya Uswisi na nchi jirani kama Ujerumani na Ufaransa ambako mhalifu anajishauri mara mbilimbili kwenda huko. Jiulizeni Vithlani yuko wapi, ziko wapi fedha zetu za rada na kadhalika

wewe, wacha hizo. shida zenu mnataka kumsingizia jirani? Kwani Uswiss haitoi account za mafisadi wakikamatwa? itabidi uondoe hadi visiwa vya Cayman Island, nk basi kama ni hivyo!! Kila nchi ina uhuru wa kutafuta ulaji wake kwa njia zake za kubuni. Kama anakamua mafisadi wenu, basi nyie pambaneni na mafisadi, sio mmsingizie yeye.
Gaddafi hajasema nchi ifutwe kwa sababu ya ufisadi maana kama ni hivyo itabidi Libya nako ifutwe! Sababu yake ni kwa kuwa mtoto wake kafanyiwa mabaya, wala sio Libya iliyofanyiwa mabaya!
Jamani naona hapa ni kwa sababu tu amezungumza Ghadafi ambaye baadhi yetu hatumpendi kwa sababu fulani fulani, lakini kwa kifupi Uswis ni nchi ambayo imekuwa chaka la mafisadi duniani kwa miaka mingi sasa. Mafisadi wa dunia wanaishi maisha bora sana wanapokuwa huko. Wengine wanaishi milimani wakipata ulinzi bora kabisa wa serikali ya Uswisi. Nchi hiyo imepata utajiri na itaendelea kutajirika kwa mitaji ya fedha zetu kutoka nchi masikini. Hawawezi kubadilika, maana wanahubiri demokrasia na utawala bora kwetu huku wao wakikumbatia wahalifu kutoka kwetu. Jamani kama wakigawanywa itakuwa afadhali maana kuna afadhali kubwa sana kati ya Uswisi na nchi jirani kama Ujerumani na Ufaransa ambako mhalifu anajishauri mara mbilimbili kwenda huko. Jiulizeni Vithlani yuko wapi, ziko wapi fedha zetu za rada na kadhalika
Jamani naona hapa ni kwa sababu tu amezungumza Ghadafi ambaye baadhi yetu hatumpendi kwa sababu fulani fulani, lakini kwa kifupi Uswis ni nchi ambayo imekuwa chaka la mafisadi duniani kwa miaka mingi sasa. Mafisadi wa dunia wanaishi maisha bora sana wanapokuwa huko. Wengine wanaishi milimani wakipata ulinzi bora kabisa wa serikali ya Uswisi. Nchi hiyo imepata utajiri na itaendelea kutajirika kwa mitaji ya fedha zetu kutoka nchi masikini. Hawawezi kubadilika, maana wanahubiri demokrasia na utawala bora kwetu huku wao wakikumbatia wahalifu kutoka kwetu. Jamani kama wakigawanywa itakuwa afadhali maana kuna afadhali kubwa sana kati ya Uswisi na nchi jirani kama Ujerumani na Ufaransa ambako mhalifu anajishauri mara mbilimbili kwenda huko. Jiulizeni Vithlani yuko wapi, ziko wapi fedha zetu za rada na kadhalika
huyu jamaa atakuwa hana advisors nini? au wanamwogopa. Anadhani yeye ni nani hadi aombe taifa kuondolewa. Na Libya nayo pia ifutwe maana imechanganya raia wa misri, algeria, tunisia, chad, niger na sudan.
Mbona wapambe anao kibao tu. Hukuna sherehe yake ya 40 years ya kutawala akina nani walikuwepo??? hata jamaa yetu alikuwepo pia!!!
Una akili sana we mtoto kuliko hata wakubwa. Hongera sana.Ndio maana huwa wezi na majambazi wakifanikiwa wanaitwa "wajanja" kwa kuwa na wao "wanatafuta njia zao za ulaji za kubuni" na ule usemi wenu wa "kila mtu atakula kwenye meza yake".
Tutaendelea hivyo hivyo Watanzania kwa Wajanja kama kina..... kuendelea kupeta. Na wengine tutaambiwa hivyo hivyo "muna wivu wa kike", "mumepata wapi mitaji" "ni ugomvi wa kibiashara" na kadhalika na kadhalika lakini nchi inaendelea kuwa omba omba na kutegemea fadhila za hao hao Waswisi.