Gaddafi Adaiwa Kujirusha Kisiri na Mama wa Mfalme wa Uganda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Gaddafi Adaiwa Kujirusha Kisiri na Mama wa Mfalme wa Uganda

Discussion in 'International Forum' started by MziziMkavu, Jul 7, 2009.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jul 7, 2009
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi Tuesday, July 07, 2009 7:40 AM
  Kiongozi wa Libya Kanali Muammar Gaddafi ambaye ana wake wawili na watoto wanane amedaiwa kuwa yuko kwenye mapenzi ya siri na mama wa mfalme wa Uganda. Gaddafi mwenye umri wa miaka 67 amedaiwa kuwa anajirusha kimapenzi kwa siri na Best Kemigisa, 42, ambaye ni mama wa mfalme Oyo Nyimba Kabamba Rukidi IV wa Toro.

  Toro ni miongoni mwa falme tano kubwa za kitamaduni zilizobaki nchini Uganda.

  Kwa mujibu wa gazeti linalosomwa sana nchini Uganda la Red Pepper, Gaddafi alikutana na malkia Best Kemigasa wakati wa sherehe za kuvishwa taji la ufalme mtoto wake Oyo ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 9 na nusu. Hivi sasa mfalme Oyo ana umri wa miaka 17.

  Gaddafi alionana tena na malkia Kemigasa mwaka 2001 wakati alipoalikwa nchini Uganda wakati rais Yoweri Museven alipofanya sherehe za kushinda uchaguzi wa urais.

  Taarifa ziliendelea kusema kuwa Gaddafi alimualika nchini Libya malkia Kemigasa wakati huo.

  Habari za mapenzi ya Gaddafi na malkia Kemigasa zilipamba moto hivi karibuni baada ya kugundulika kuwa karibuni familia yote ya malkia huyo imehamia nchini Libya.

  Taarifa zaidi ziliendelea kusema kuwa Gaddafi alimnunulia mpenzi wake huyo ndege ambayo malkia huyo anaitumia.

  Gazeti hilo liliendelea kusema kuwa Gaddafi alimtaka malkia Kemigasa amzalie mtoto wa kiume.

  Kutolewa kwa habari hizo kulimkasirisha sana Gaddafi na wakati huo huo wahariri wawili wa gazeti hilo walifunguliwa mashtaka na ubalozi wa Libya nchini Uganda kwa kutoa habari za kumchafulia jina Gaddafi.

  Balozi wa Libya amewafungulia mashtaka wahariri wawili wa gazeti hilo akitaka walipe fidia ya paundi milioni 245 kwa kumchafulia jina kiongozi wa Libya.
  http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsId=2436030&&Cat=2
   
 2. G

  Game Theory JF-Expert Member

  #2
  Jul 7, 2009
  Joined: Sep 5, 2006
  Messages: 8,571
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 0
  [​IMG]
   
 3. Eqlypz

  Eqlypz JF-Expert Member

  #3
  Jul 7, 2009
  Joined: May 24, 2009
  Messages: 4,069
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Old News next.
   
Loading...