Naamini hata nyie hamna rukhsa ya kutumia lugha chafu na kukera msiokuwa nyie. Heshima kitu cha bure, ukijiheshimu utaheshimiwa.
Kuwa homeless au kuwa Raia wa Romania hailivui lile jina la Jumla tulilowapa la kuwa wazungu. Uwepo wao hao uliowaita wazungu homeless na Waromania ni kheri nyingine kuwa kwetu sie hawabaguliwi watu kutokana na utaifa, rangi na uwezo. Licha ya hayo, bado hauna ushahidi kuwa wazungu wasiokuwa homeless na Waromania hawakuhudhuria. Tupe ushahidi kutetea hoja yako kama u miongoni mwa wasemao ukweli.
Mmmh!! Sijui!! Kuna sheria za kiislamu UK? Kwa maana nyingine UK inatekeleza Sharia kipindi cha ramadhani  tu? na je kufuturisha hadharani ni kutekeleza sharia ipi ya kiislamu?
Nikushauri tu kuwa, isikupelekee chuki ikawa ni kikwazo kuwafanyia wenzio wasio wewe au jamii yako UADILIFU. Tekeleza uadilifu, kwani itakukurubisha kwenye UchaMungu.
#Peace