Fursa za Mji wa Kigoma

NONGWA

Senior Member
Mar 10, 2012
142
116
Wadau naomba kujua ni fursa gani zipo za kibiashara kwa nyanja zote katika Mkoa wa Kigoma. Mimi natokea Dar na kwenda Kigoma kwa shughuri za kikazi tu wadau naomba kujua.
 
Usisema Mji Sema Dubai Ya Tanzania
Fursa Lima Chikichi, Ntole, Zambagiza, Mkubi

Msimu Wa Nswa Unatafuta Kichuguu Chako Unashinda Hapo
We jamaa umenichekesha eti zembagiza, mkubi. Sasa ataelewa nini halafu mkubi apeleke wapi.

Akiwa mnyakyusa atafurahi sana kule kwao kuna mkubi, chikichi wao huita mawese au mbosa, nswa ndio kwso hapo naongezea na uyoga bila kusahau ndizi kisamunyo, kijivu na zile za kupikia kayoga.

Aisee huyo hata hama akibahatika na kupata binti kule ujiji kwao watamsahau.
 
Akipata Binti Wa Kiha Toka Kasulu Ndiyo Atasahau Yote
 
Usisema Mji Sema Dubai Ya Tanzania
Fursa Lima Chikichi, Ntole, Zambagiza, Mkubi

Msimu Wa Nswa Unatafuta Kichuguu Chako Unashinda Hapo
Na Akishalima chikichiki aje nimtengenezee mashine za kisasa za kukamua mafuta ya MAWESE na na kubangua mbosa/mise.

Karibu.
 
Kilimo cha chikichi/mawese... Kulima mwenyewe au kujiongeza kupitia kulangua na kukamua au ukihitaji basi nikutengenezee mashine ya kisasa ya mawese nikusimikie site Nzuri uendelee kunywa kuku kwa mrija.
 
Mkoa wa kigoma kuna fursa nyingi kama ilivo mikoa mingine kwa haraka haraka kutoka kigoma mjini pale utakuta bandari ukiweza tafuta connection ya kupeleka vitu kama mchele, mbuzi, nchini DRC
 
Kwa sababu inampaka na nchi pia ya Burundi basi peleka pia udaga ambao utanunua kule kibondo au maeneo ya wilaya ya kasulu, makere, kagera nkanda,
 
Au unaweza kwenda kijiji kimoja kinaitwa heru juu ukanunua mirunda ya kujengea magorofa kule ni bei rahisi kuliko njombe na mafinga ukaipeleka Dodoma ukipata soko la uhakika kwani inalipa sana
 
Lakinj utaweza kutafuta magimbi maji yale makubwa maeneo ya kibondo na kwenda kuyauza nchini Burundi ambapo kwa sasa wao kilo moja ya magimbi hununua kwa shilingi 340
 
Kama ulivoshauriwa unaweza kulima zao la mchinichi maeneo ya ukanda wa Burombora, kaseke, ilagara, kamara, simbo na kadhalika hilo ni zao la kudumu na litakupa pesa ya uhakika kama ilivo korosho lindi, mtwara au parachichi njombe na mbeya
 
Back
Top Bottom