Fursa za Mazao ya Bustani Dodoma

The Spirit of Tanzania

JF-Expert Member
Mar 7, 2020
539
930
Wakuu amani iwe kwenu.

Naomba nisaidiwe kujua fursa za mazao ya bustani mkoani dodoma, yaani je uhitaji upo wa mbogamboga kama mchicha, chainizi, spinach, majani ya kunde n.k.

Naomba pia kujua maeneo gani wanakodisha mashamba ya bustani, hasa panapopatikana maji kwa wingi, bei zake, barabara ikoje.

Nilitaka kuhamia Dodoma, nikafanye kazi hiyo sasa kabla ya kwenda ningepata taarifa hizi ingenisaidia nipango yangu.

Asanteni.
 
Lile ni jiji, lazima mahitaji yatakuwa ni makubwa.

Nakutia moyo, endelea na wazo lako. Zingatia;

  • Weka outlet point ya kuaminika, -Fungasha bidhaa zako kistaarabu zivutie watu wa aina zote.
  • Fungua kurasa za mitandao ya kijamii
  • Hakikisha una bidhaa anuai (varieties) hata ambazo hauzalishi unaweza kuzisogeza kutoka kwa wazalishaji wengine au sokoni,
  • Simamia wewe mwenyewe au mkeo/mumeo/mwanahisa mwenzio
  • Ikitokea kupata hasara mwanzoni, usikate tamaa, endelea kujenga soko, jifunze.

Hakika utatoboa na Mungu akubariki
 
Mkuu kwa ushauri Tenga muda uje hombolo u survey kwanza utakua na maamuzi mazuri juu ya bustani.
 
Mkuu kwa ushauri Tenga muda uje hombolo u survey kwanza utakua na maamuzi mazuri juu ya bustani.
Nikifika dodoma,kuja hombolo napanda gari gani?

Halafu kutoka dodoma mjini hadi hombolo ni muda gani mkuu?

Natamani soko langu liwe Dodoma mjini, nahisi kuja mahitaji mengi pale japo sina uhakika.
 
Wakuu amani iwe kwenu.

Naomba nisaidiwe kujua fursa za mazao ya bustani mkoani dodoma, yaani je uhitaji upo wa mbogamboga kama mchicha, chainizi, spinach, majani ya kunde n.k.

Naomba pia kujua maeneo gani wanakodisha mashamba ya bustani, hasa panapopatikana maji kwa wingi, bei zake, barabara ikoje.

Nilitaka kuhamia Dodoma, nikafanye kazi hiyo sasa kabla ya kwenda ningepata taarifa hizi ingenisaidia nipango yangu.

Asanteni.
Karibu sana Dodoma,vizuri ununue eneo pembezoni mwa mji na unatoboa kisima na mambo yanasonga.
 
Huku ni jukwaa serious.
Lets get serious.
Personally nliemda dodoma na the same idea.
Sehem ambapo mimi niliona panafaa ni chamwino ikulu.
Kule kuna sehem nyingi sana watu wanalima tena kwa kumwagilia.
Wenyeji wana shamba ndogo ndogo coz wengi hawana pumps.
Lakini wanatumia visima vya kuchimba wenyewe. Around 4 metres unakuta maji, so mtu unaeza kuta kachimba hata 2 around kashamba chake.
Mimi naona pale panafaa ni mwendo kama wa km 35 frm town.
Dom mjini pia kuna maeneo watu wanalima kwa mfano njia ya kwenda nanenane lakn nahisi gharama zitakua juu kidogo.
Pia kuna wale wanaolima huko swaswa lakini watu wengi hawapendi mboga kutoka huko maana wanaamini zinamwagiliwa kutumia majitaka.
All in all, tenga muda, njoo mjini ufanye survey yakutosha.
Kila la kheri
 
Nikifika dodoma,kuja hombolo napanda gari gani?

Halafu kutoka dodoma mjini hadi hombolo ni muda gani mkuu?

Natamani soko langu liwe Dodoma mjini, nahisi kuja mahitaji mengi pale japo sina uhakika.
umbali kutoka sokoni had hombolo wasatan km 26 iv barabara ipo vzur uzuri ni kwamba hombolo kuna bwawa ambalo litakusaidia katika umwagiliaji vile vile mashamba utapata kwa gharama nafuu tafauti na sehem zingine mkuu
 
Dodoma Naona Wakulima Wa Mboga Wenye Visima Vyenye Maji Muda Wote Ndiyo Wanaweza Kumudu Bustani Za Mboga. Zanka Hapo Toka Jeshini Pale Unajikatia Mapori
 
umbali kutoka sokoni had hombolo wasatan km 26 iv barabara ipo vzur uzuri ni kwamba hombolo kuna bwawa ambalo litakusaidia katika umwagiliaji vile vile mashamba utapata kwa gharama nafuu tafauti na sehem zingine mkuu
Hv gharama za kukodi eneo la nusu ekari zinaweza kucheza kwenye shilingi ngapi?
 
Back
Top Bottom