Fursa za biashara kwa kila mkoa hapa nchini

Fursa za biashara kwa kila mkoa hapa nchini

Kivip bro?

inakua vema kama ukiweka ni biashara gani
Kwanza ulitakiwa useme aina ya biashara ambayo unafikiria kuifanya. Baada ya hapo ndipo nitakushauri kwa kuanzia kwenye pendekezo lako
 
Naipendelea simiyu zamani(bariadi)ni mji unaoanza kuwa.naona watu wengi wanafanya biashara hasa za nguo,mazao na mengineyo.ila biashara za pale ni za msimu.

Kwa kua ni mji unaokua na kuona wajenzi wengi wanapenda tofali za kuchoma nikajaribu kwa mtaji mdogo tu
Tofali bichi sh.7@1
Kuni sh 50000 mapori mengi
Usafiri 20000 wa tela la ngombe. kuleta maji 10000.
Eneo nilipewa bure bada ya biashara niliwapa 20000 ya shukrani tu.
Wa kuchoma na kupanga niliwapa lak 1.
Nilichoma tofali 10000.
Mahesabu ni
7×10000+50000+20000+20000+100000+10000=370000
Mtaji ni 370000 fanya kuna tofal zitaharibika so weka 30000.pesa yote ya mtaji ni lak 4 mpaka tofali kuiva teyar kwa kuuzwa.

TWENDE KWENYE BIASHARA SASA

minimum tofali moja 120tsh
120×10000=1200000tsh

Kama bei ya kawaida 150 tsh
150×10000=1500000tsh

Ukitoa mtaji jibu utakua nalo umebaki na faida ya sh. Ngap

MUHIMU
hii biashara ni ya wakati wote ila bei zinapanda tokana na msimu.msimu wa mvua ndo tofali haikamatiki.msimu wa kiangazi bei inakua chini mana wapiga tofali ni wengi sana.

CHANGAMOTO
biashara hii siyo ya hapo kwa papo wakati mwingine inachukua mda mpaka kuja kuuza so kama huna shughuli ingine utataabika mzee.

Kama biashara yako itakua ni ya huakika na kuaminika utakula tenda nyingi mkuu na hizo ndo zinalipa hakuna mfano.sababu ukiweka mtaji mkubwa na faida inakua kubwa mfano ukiweka tofali laki moja faida utaipenda zaidi.
Pia kuna wale wanunuzi watofal chache chache hawanunui tanuru nzima waepuke wanavuruga malengo

Note:hii biashara nilifanya 2014 sijui kwa sasa bei zikoje
Wapendwa ni muda sasa nawaza wapi panafaa kwa biashara na mzunguko wake wa pesa ni mkubwa kulinganisha na mahala pengine.
Toa mji wa mamwinyi TANGA
KOKOTO ulipo pana faa ila jielekeze kwenye Biashara ya hisa za Vodacom kwa mwaka huu ndio habari ya mjini
 
Biashara ni kokote ila kwa mwaka huu biashara za Hisa za kampuni za simu zitafanya vizuri. Njia ya mtandao ita kusaidia kununua na kuuza. Barikiwa
 
KOKOTO ulipo pana faa ila jielekeze kwenye Biashara ya hisa za Vodacom kwa mwaka huu ndio habari ya mjini
Kununua hisa ni uwezaji mzuri, lakini lazima uchukue tahadhari sana kwani ikitokea jamaa wakatangaza loss ,either kwa kukwepa kodi au iwe imetokea na wewe unaingia loss lakini ujue ukiweka hisa kidogo saba let say 0.000000018% tarajia kupata faida ndogo sana tofauti na ungewekeza kwenye ujasiriamali
 
Wapendwa ni muda sasa nawaza wapi panafaa kwa biashara na mzunguko wake wa pesa ni mkubwa kulinganisha na mahala pengine.
Toa mji wa mamwinyi TANGA
Mm sijatembea mikoa mingi lkn Mtwara na wilaya zake Masasi, Newala ni sehemu yenye fursa, na biashara nzur huko ni ya vyakula kwakuwa wakaazi wa huko wao wamejikita sana kuzalisha korosho, Ufuta, karanga na Mbaazi mazao ambayo sio wanayokula. Hivyo huendesha maisha kwa kununua... mfano wilaya ya Newala vitu kama nyanya karoti (mbogamboga) ni adimu na ghali... Hivyo mtu ukijitoa ufahamu ukatoka nje kidogo ya mji ukazalisha ivyo vitu sambamba na kujumua... ninaamini matokeo njenje...

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Biashara ya mazao ni nzuri sana em tafuta mkoa ambapo mazao yapo juu sana kwa kuuza uwe unapoiga root unaendea mazao katavi then unauza huo mkoa.
 
Wapendwa ni muda sasa nawaza wapi panafaa kwa biashara na mzunguko wake wa pesa ni mkubwa kulinganisha na mahala pengine.
Toa mji wa mamwinyi TANGA
kwa nn tutoe jiji la tanga ambalo ni jiji la pili kwa viwanda vikubwa nchini na pua ni miongoni mwa majiji manne yanayochangia pato kubwa kwenye uchumi wa taifa letu?
 
Back
Top Bottom