Fursa ya kupeleka mchele nchini Rwanda

@UNSPECIFIED,sijui kwa awamu hii,lakini miaka ya nyuma hata tani kumi unakodi fuso unaingia zako kigali unauza
 
Sawa bana,afu usinitoe kwenye reli nia yangu ni kula madini ya Biz ya Wali huko Chigali, kwanini iwe inalipa kushinda DRC wewe tukana na utembee kifua nyuma ka unataka.
 
hii biashara inafaa upeleke mchele wa Kyela ambao ukipikwa mpaka mtaa wa pili wananusa harufu....
 
Huwezi kufanya biashara hiyo kama huna pesa ,namaanisha pesa sio una tani 60, unataka kupeleka mchele ng'ambo
Usipotoshe mkuu!! Watu hadi tani 30 wanapeleka sembuse tani 60!!!unapozungumzia tani sitini sio mchezo kama ni mchele hapo unazungumzia sio mtaji wa kitoto ni kama milioni 80!!!
 
Hawajata kuweka wazi..huenda wananihofia pia...ila nadhan ni mtaji mnene kias..wanapelela tons nyingi wanadai (hawajasema zaidi) ngoja nijidangishe wafunguke😂😂🙌
pia uwe makini dada. Mana wasanii n wengi mjini hapa
 
hii biashara inafaa upeleke mchele wa Kyela ambao ukipikwa mpaka mtaa wa pili wananusa harufu....
Biashara za huko huwezi peleka mchele wa kyela, uuzaji wake ni mgumu sana, kwani bei itakuwa kikwazo!! Kule unapeleka wa kawaida, labda uwe na order maalum!! Huo wa kyela mfano uununue tsh. 1800!!hujaweka ushuru, usafiri, utauuza bei gani?
 
😁😁😁haya...na trauza naona karibu kila siki usk unaona mtu ananunua anavaa hapo hapo anasepa..zile kadeti

Mkuu nauza nguo za watoto minadani, hasa ya mkoa wa morogoro vipi hizo cadeti au hayo mashati naweza kupata wateja huku?
 
Biashara za huko huwezi peleka mchele wa kyela, uuzaji wake ni mgumu sana, kwani bei itakuwa kikwazo!! Kule unapeleka wa kawaida, labda uwe na order maalum!! Huo wa kyela mfano uununue tsh. 1800!!hujaweka ushuru, usafiri, utauuza bei gani?
Mkuu mchele wa kyela unafaa upelekwe kipindi kama hiki cha mavuno unakuwa very cheap coz debe la mchele linashuka mpk 25000/-.
 
Mimi nimeshawahi kupeleka mchele kule. Nilikua nachukulia Nzega kwa sababu ya bei nk.. Na kigali nilikua nauzia sehemu moja inaitwa Gikondo. Watu wengi hupenda kuchukulia kahama wana sababu zao. Ukitaka ufanye biashara kwa raha kodisha store yako kule.
Bei mimi nklikua nauza 50kg kwa Rwf 55,000 ni kama Tsh 138,000 hivi. Kwenye gari ilikua inaingia mifuko 660 ya 50kg. Gari moja unaweza kuiuza kwa muda usiozidi wiki kwa vile kule sio walaji sana wa mchele kama sisi.
NB: usiuze rejareja. Na biashara ya dagaa ni nzuri kule lakini kwa wanawake
 
Ukishindwa kule jaribu Bujumbura ila mchele uchukulie Mpanda.
Jaribuni na viazi, vitunguu na ndizi kule Lusaka ni bonge la dili.
Kidogokidogo jaribuni kuvuka mipaka na Mwenyezimungu atajaalia Inshallah.
 
Money money...we dada hustler sana i can bet my money on you [emoji651]️TOP

Yaani nasema Mungu nipe pumzi..huku wananiangaliaga tu yaan..afu waniita mchaga😂😂wanasema wanawake wa kisukuma hawana mwamko kbs wa kuhustle..ila its true😉.. mie nikifika kila siku niwe naweka 200k ntakamilisha kbs my long term plans..huku ukiweza tu kujitoa kbs uhakika wa kupata even 200k@ day upo...toa ishu za madini.ntakuja pm tmr..
 
Ila wanyarwanda wamejaaje Kahana wananunua mchele
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…