Mkuu hapo umenena vyema haswa!Himizeni mji huo upangiliwe vizuri uwe mji mzuri na mkubwa.
Migahawa ya kisasa iko mingi Geita mjini,hapo katoro kuna virestaurant vidogo vidogo tu kama hako ka karibu na bank ya nmb wanakaita NtineKatoro je Biashara ya restaurant ipoje kwa sisi wapishi wazuri wa vyakula vitamu na vyenye taste ya vip wapo clients wa kuweza nunua sahani elf sita? Na elfu mbili glasi moja ya juice ya matunda . I need to invest in such kind of business
Tumezoea. Bora faida ya Tsh 100 kwenye mzunguko mkubwa.Biashara za Katoro ni za kukomoana,wafanyabiashara wanauza bidhaa kwa bei za karibu na hasara ili kuwakomoa wenzao
Wanaoifaidi katoro ni wanaokwenda kulangua mzigo hapo ila wafanyabiashara wengi wa hapo wako chali
KATORO
(Mji) ni mkusanyiko wa kata tano (5) ndo zinaunda mji tunaoita katoro. Kata hizo ni kata ya Katoro, kata ya Buseresere, kata ya Ludete, kata ya Butengolumasa na kata ya Ibondo. Huku mji unaendelea kupanuka mpaka umeungana na kata ya sita ambayo ni kata ya Nyamigota.
Mji wa katoro, umejengwa 100% na makazi ya watu na biashara zao, hakuna ofisi kubwa ya umma isipokuwa Hospital, vituo vya afya na shule za msingi na secondary.
Mji wa katoro unafanya vizuri sana kibiashara, kwasababu mbalimbali zikiwemo, umati mkubwa wa watu, makutano ya barabara za Geita-Chato na Katoro-Ushilombo. Pia, barabara za kwenda ziwa Victoria na Migodi mingi (Midogo midogo) ya dhahabu inayozungua eneo hilo.
ULINZI NA USALAMA.
Mji wa katoro asilimia kubwa kuna ulinzi binafsi (Private security companies) kwajili ya ulinzi wa maduka makubwa na maeneo ya masoko. Hii ilitokea baada ya miaka ya nyuma uvamizi (kwa kutumia bunduki) kuongezeka. Kuhusu usalama wa raia katoro ni sehem salama sana.
BIASHARA ZINAZOFANYA VIZURI KWA SASA.
Kwasasa Katoro, biashara nyingi zinafanya vizuri sana japo inategemea na ukubwa wa mtaji wako. Kwamfano:
1. Wenye mtaji mikubwa. Biashara za Vituo vya mafuta (Shell) zinajengwa kwa kasi sana. Kila leo zinafunguliwa mpya maeno mbalimbali ya barabara ya Chato, Ushilombo, Geita....
2. Masoko binafsi. Katoro watu wanajenga masoko binafsi yenye frem za kupangisha maduka, na chanja za mama mboga. Mfano, soko la kishimba...
3. Shule private/Chekechea zinafunguliwa sana. Japo sikuizi shule binafsi hazilipi sana.
4. Kafaka. Katoro uhitaji wa nafaka ni mkubwa sana. Mwaka mzima nafaka zinaingia kutoka sehem mbalimbali mwa Tanzania, mfano (maharage kutoka kigoma, mahindi kutoka sumbawanga, karanga za Tabora......). Sababu kubwa inaweza kuwa ni idadi kubwa sana ya watu na migodi ya dhahabu around katoro.
5. Maduka ya nguo. Katoro inaongoza almost kanda ya ziwa (ukitoa Mwanza) kwa kuuza nguo. Ukifika Katoro madukani, utakutana na wafanyabiashara wa nguo kutoka bukoba, ngara, karagwe, chato, Geita, biharamulo, etc wamekuja kununua nguo. Hii inaonyesha soko la nguo ni kubwa sana katoro.
6. Store za mpunga. Kati ya biashara zinazolipa katoro ni pamoja na mashine za kukoboa mpunga na store zake.
7. Plant na Elution. Biashara hii inalipa sana. Kwasababu katoro imezungukwa na migodi mingi midogo midogo ya dhahabu, Plant na Elution nyingi zimejengwa maeneo (karibu) na katoro Kwasababu ya usalama zaidi. Kwasasa hii biashara imeajili vijana wengi sana kutoka katoro.
Kwa watu wenye mitaji midogo na ya kati. Kuna biashara ambayo mtu anaweza kufanya na ikamtoa kimaisha.
1. Kufuata samaki ziwa Victoria
2. Kufuata viazi na mihogo sehem za runzewe na kuleta katoro.
3. Nyanya, vitunguu na mboga mboga
4. Bajaji na boda boda
5. Ufundi wa ujenzi
6. Ufundi wa furniture (sofa, kabati,.... )
7. Welding na aluminium
8. ......
(KARIBU SANA MJI WA KATORO UFANYE BIASHARA)
Wateja wapo wa kununua sahani ya. Chakula elfu sita?Migahawa ya kisasa iko mingi Geita mjini,hapo katoro kuna virestaurant vidogo vidogo tu kama hako ka karibu na bank ya nmb wanakaita Ntine
Zao lolote laweza kuwa la kibiashara hata mchicha.Wakazi wa Katoro wanalima mazao gani ya biashara?
Yes, restaurant nzuri zipo japo ni chache. Wateja wa aina zote (wa kati na chini) wapo.Katoro je Biashara ya restaurant ipoje kwa sisi wapishi wazuri wa vyakula vitamu na vyenye taste ya vip wapo clients wa kuweza nunua sahani elf sita? Na elfu mbili glasi moja ya juice ya matunda . I need to invest in such kind of business
Wapo ila itategemeana na namna ya uendeshaji wa biashara yako,pia locationWateja wapo wa kununua sahani ya. Chakula elfu sita?
Mkuu huwezi kuuza mzigo kwa karibu na hasara ukaendelea kukua kibiashara. Kilichopo hapo ni kwamba wafanyabiashara wengi wanafuata mizigo Dubai, China na Kampala direct. Wanakuja kuuza mzigo bei zao zinapishana kidogo tu na zile za karakoo za Dar es salaamBiashara za Katoro ni za kukomoana,wafanyabiashara wanauza bidhaa kwa bei za karibu na hasara ili kuwakomoa wenzao
Wanaoifaidi katoro ni wanaokwenda kulangua mzigo hapo ila wafanyabiashara wengi wa hapo wako chali
Kama upo katoro naomba mawasiliano yako mkuu nahiitaji kufungua Mgahawa wa kisasa Mimi ni Mpishi mzuri Sana nikipika chakula Hadi kila lazima aseme yes so kwa hapa dar nimepika katika event tu so nahiitaji kuwa na restaurantWapo ila itategemeana na namna ya uendeshaji wa biashara yako,pia location
Sipo Katoro ila kila baada ya wiki kama 3 au2 nakuwa hapoKama upo katoro naomba mawasiliano yako mkuu nahiitaji kufungua Mgahawa wa kisasa Mimi ni Mpishi mzuri Sana nikipika chakula Hadi kila lazima aseme yes so kwa hapa dar nimepika katika event tu so nahiitaji kuwa na restaurant
Sawa Mkuu ubarikiwe sanaSipo Katoro ila kila baada ya wiki kama 3 au2 nakuwa hapo
Wafanyabiashara wengi ni wakulima,wana ming'ombe polini na pia wana nyumba za kupangisha kwahiyo biashara kwao inakuwa ni ya kutafutia hela ya mbogaMkuu huwezi kuuza mzigo kwa karibu na hasara ukaendelea kukua kibiashara. Kilichopo hapo ni kwamba wafanyabiashara wengi wanafuata mizigo Dubai, China na Kampala direct. Wanakuja kuuza mzigo bei zao zinapishana kidogo tu na zile za karakoo za Dar es salaam