amate
Senior Member
- Feb 23, 2017
- 157
- 378
KATORO
(Mji) ni mkusanyiko wa kata tano (5) ndo zinaunda mji tunaoita katoro. Kata hizo ni kata ya Katoro, kata ya Buseresere, kata ya Ludete, kata ya Butengolumasa na kata ya Ibondo. Huku mji unaendelea kupanuka mpaka umeungana na kata ya sita ambayo ni kata ya Nyamigota.
Mji wa katoro, umejengwa 100% na makazi ya watu na biashara zao, hakuna ofisi kubwa ya umma isipokuwa Hospital, vituo vya afya na shule za msingi na secondary.
Mji wa katoro unafanya vizuri sana kibiashara, kwasababu mbalimbali zikiwemo, umati mkubwa wa watu, makutano ya barabara za Geita-Chato na Katoro-Ushilombo. Pia, barabara za kwenda ziwa Victoria na Migodi mingi (Midogo midogo) ya dhahabu inayozungua eneo hilo.
ULINZI NA USALAMA.
Mji wa katoro asilimia kubwa kuna ulinzi binafsi (Private security companies) kwajili ya ulinzi wa maduka makubwa na maeneo ya masoko. Hii ilitokea baada ya miaka ya nyuma uvamizi (kwa kutumia bunduki) kuongezeka. Kuhusu usalama wa raia katoro ni sehem salama sana.
BIASHARA ZINAZOFANYA VIZURI KWA SASA.
Kwasasa Katoro, biashara nyingi zinafanya vizuri sana japo inategemea na ukubwa wa mtaji wako. Kwamfano:
1. Wenye mtaji mikubwa. Biashara za Vituo vya mafuta (Shell) zinajengwa kwa kasi sana. Kila leo zinafunguliwa mpya maeno mbalimbali ya barabara ya Chato, Ushilombo, Geita....
2. Masoko binafsi. Katoro watu wanajenga masoko binafsi yenye frem za kupangisha maduka, na chanja za mama mboga. Mfano, soko la kishimba...
3. Shule private/Chekechea zinafunguliwa sana. Japo sikuizi shule binafsi hazilipi sana.
4. Kafaka. Katoro uhitaji wa nafaka ni mkubwa sana. Mwaka mzima nafaka zinaingia kutoka sehem mbalimbali mwa Tanzania, mfano (maharage kutoka kigoma, mahindi kutoka sumbawanga, karanga za Tabora......). Sababu kubwa inaweza kuwa ni idadi kubwa sana ya watu na migodi ya dhahabu around katoro.
5. Maduka ya nguo. Katoro inaongoza almost kanda ya ziwa (ukitoa Mwanza) kwa kuuza nguo. Ukifika Katoro madukani, utakutana na wafanyabiashara wa nguo kutoka bukoba, ngara, karagwe, chato, Geita, biharamulo, etc wamekuja kununua nguo. Hii inaonyesha soko la nguo ni kubwa sana katoro.
6. Store za mpunga. Kati ya biashara zinazolipa katoro ni pamoja na mashine za kukoboa mpunga na store zake.
7. Plant na Elution. Biashara hii inalipa sana. Kwasababu katoro imezungukwa na migodi mingi midogo midogo ya dhahabu, Plant na Elution nyingi zimejengwa maeneo (karibu) na katoro Kwasababu ya usalama zaidi. Kwasasa hii biashara imeajili vijana wengi sana kutoka katoro.
Kwa watu wenye mitaji midogo na ya kati. Kuna biashara ambayo mtu anaweza kufanya na ikamtoa kimaisha.
1. Kufuata samaki ziwa Victoria
2. Kufuata viazi na mihogo sehem za runzewe na kuleta katoro.
3. Nyanya, vitunguu na mboga mboga
4. Bajaji na boda boda
5. Ufundi wa ujenzi
6. Ufundi wa furniture (sofa, kabati,.... )
7. Welding na aluminium
8. ......
(KARIBU SANA MJI WA KATORO UFANYE BIASHARA)