Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,685
- 119,325
Wanabodi,
Msimu wa Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam, SABA SABA, umewadia, mimi mwana JF mwenzenu, Paskali Mayalla, kupitia kampuni yangu ya PPR, huwa ninarusha vipindi vya matangazo ya SABA SABA kupitia Vituo Vitano vya Televisheni kila siku kwa muda wa siku 10.
Vituo hivyo ni ...
ITV, kila siku kuanzia Saa 12:30 jioni hadi Saa 1:00 kamili.
TBC, kila siku saa 4:00 usiku hadi saa 4:30
Star TV, kila siku Saa 3:30 usiku hadi Saa 4:00 kamili.
Channel Ten kila siku Saa 2:30-3:00 usiku.
Clouds TV kila siku Saa 4:00-4:30 usiku.
Natoa fursa kwa wana JF ambao ni wajasiliamali, walioko kwenye uwanja wa Saba Saba, tuwasiliane na mimi kwa SMS 0754 270403 (Naomba usipige simu, sipokei kutokana na kuwa bize wakati wote).
Matangazo haya kwa wana JF, sio kwa ajili ya wana JF walioko Saba Saba Pekee, bali kwa wana JF wengine wowote, ambao ni wajasiliamali, popote walipo, na bidhaa zao original, wanaofanya ujasiliamali, ambapo wakipata fursa za kutangaza bidhaa zao, watafungua fursa za masoko zaidi!.
Unachotakiwa kufanya, ni
1. Kama una uwezo wa kuja saba na kumiliki banda, nakushauri njoo Saba Saba, lipia banda, leta bidhaa yako. Kisha niite nitakutangazia bure kutoka kwenye banda lako.
2. Kama huna iwezo wa kumiliki banda, lakini unayo bidhas yako, inachotakiwa kufanya ni kuibeba tuu hiyo bidhaa yako, njoo nayo kwenye uwanja wa Saba Saba, na kulipia kiingilio na bidhaa yako mkononi, ukiingia tuu viwanjani, Ofisi za PPR zilizoko Saba Saba, zipo kwenye Jengo la TANTRADE Unalotazamana nalo.
Lengo la kutoa fursa hii, ni kuwapa wana jf wenzetu wanaofanya mambo makubwa, mazuri kwa manufaa ya taifa, lakini hawana uwezo wa kulipia matangazo ya bidhaa zao. PPR itawaunganisha wazalishaji na masoko, ambapo wakipata fursa za kujulikana, wataongeza masoko, kupanuka zaidi, na kuongeza uzalishaji.
Matangazo ya Televisheni ni ghali, vituo vya televisheni vinatoza gharama kubwa kutangaza kwenye mabanda mbalimbali, mimi kupitia kampuni yangu, tayari ninao wateja wakubwa "corporate customers" wenye uwezo wa kulipia hizo gharama za TV, hivyo nami kwa upande nina obligation "to give back to the society", kwa kuwapa fursa wale wenye bidhaa zao ambazo ni muhimu, lakini hawana uwezo wa kumudu gharama za matangazo kupitia kwenye vituo vya Televisheni.
Karibuni, tuitumie fursa hii kujitangaza tukuze biashara zetu.
Masharti ni:
Bidhaa hizo zinatakiwa kuwa ni bidhaa original na sio wafanyabiashara wanaofanya trading.
Kwa vile mimi ni mzoefu, ninauwezo wa kudermine status ya bidhaa zako, kama zinalipa nitakushauri ulipie airtime ili liwe tangazo la biashara.
Kuna tofauti ya utangazaji for information dissemination na business promotional. Information dissemination ni bure, business promotion inalipiwa.
Paskali