Fursa kubwa inayopatikana kata ya Kiranjeranje Wilaya ya Kilwa Mkoani Lindi

Jul 14, 2021
25
26
Habarini watanzania,. Kata ya KIRANJERANJE inapatika wilayani KILWA mkoani LINDI kata hii ina vijiji sita ambayo ni KIRANJERANJE ambayo ndo makao makuu ya kata, MTANDI, MBWEMKURU, MIRUMBA, KISWEHELE na MAKANGAGA. Katika kata hii kwenye vijiji vyake sita kijiji chake kimoja ambacho ni Makangaga kipo 30km kutoka barabara kuu ya kutoka Dar er salaam kwenda Mtwara kimebalikiwa madini aina ya gypsum, haya ni madini mfano wa mawe ambayo moja ya material ambayo yanatumika kutengezea siment.

Kwa sasa makampuni mengi ambayo yanazalisha siment Tanzania huwa wanayatumia haya madini. Hadi kiwanda kikubwa cha dangote huwa yanatumia haya madini.

Kuna fursa nyingi za kibiashara hizi ni baadhi tu.

1) USAFIRISHAJI. kunafursa kubwa ya usafilishaji wa haya madini. Kuna aina mbili za usafilishaji moja kutoa mzigo huu wa mawe kutoa migodini MAKANGAGA kuleta KIRANJERANJE au MTANDI ambayo vijiji ivyo vipo barabara kuu kutoka dar kwenda Mtwara . Usafilishaji mwengine ni kutoa KIRANJERANJE au MTANDI kwemda viwanda vya siment Kama Wazo, kimbiji, kibaha, Mtwara dangote nk.

2).VITUO VYA MAFUTA. Kuna fursa kubwa sana ya mafuta station kwani hapa Kuna mitambo mingi sana na magari mengi pia maitaji ya mafuta ni makubwa.

3)BIASHARA YA MADINI HAYA YA Gypsum. Kuna fursa ya biashara hii ya gypsum kuna watu wanamiliki migodi kazi yao ni kuu haya mawe migodin uko uko kwaiyo unaweza kununua ayo mawe kwa wamiliki wa migodi na wewe ukapeleka kwenye viwanda vya siment.

4) NYUMBA ZA WAGENi, Kuna fursa kubwa sana za nyumba za wageni mana kunamwingiliano mkubwa sana wa wageni.
5)HUDUMA ZA KIFEDHA. Kama mjuavyo watanzania sasa hivi dunia imeendele pesa zipo kwenye mfumo wa kidigitali hapa hasa miamala ya simu na mawakala wa mabenki. Kuna fursa kubwa sana ya hii biashara za kifedha.

Hizo baadhi za fursa tu ambazo zinapatikana, nawakaribisha watanzania wote.
Mobile. 0629641343.. Hamayserhamis
 
Habarini watanzania,. Kata ya KIRANJERANJE inapatika wilayani KILWA mkoani LINDI kata hii ina vijiji sita ambayo ni KIRANJERANJE ambayo ndo makao makuu ya kata, MTANDI, MBWEMKURU, MIRUMBA, KISWEHELE na MAKANGAGA. Katika kata hii kwenye vijiji vyake sita kijiji
Huko nikileta tipa langu trip moja ya kubeba gypsum napata laki ngapi?
 
Habarini watanzania,. Kata ya KIRANJERANJE inapatika wilayani KILWA mkoani LINDI kata hii ina vijiji sita ambayo ni KIRANJERANJE ambayo ndo makao makuu ya kata, MTANDI, MBWEMKURU, MIRUMBA, KISWEHELE na MAKANGAGA. Katika kata hii kwenye vijiji vyake sita kijiji
Nikiwa na mtaji wa laki tano nitafanya biashara gani?
 
Back
Top Bottom