Fursa katika kilimo cha viazi lishe, tuchangamkieni upesi

Soko lake liko wapi kama soko halijawa valid basi hii ni kik tu
 
SOKO LA UHAKIKA LA VIAZI LISHE, CHANGAMKIA UPESI, LISIKUPITE!

Katika kuwajali wakulima wetu na kutambua mahangaiko yao kwenye masoko ya mazao wanayoyazalisha, kampuni ya kinasoru East Africa Tanzania Ltd imepata soko la uhakika la kuuza viazi lishe nje ya nchi kupitia wakala wao aliyepo hapa nchini. Wakati naitambulisha kwa mara ya kwanza fursa hii mpya katika mada yangu ya “Fursa Katika Kilimo cha Viazi Lishe, Tuchangamkieni Upesi”, watu wengi walikuwa na shauku kubwa ya kutaka kujua kwa undani juu ya kilimo hiki lakini vilevile walitilia shaka uwepo wa soko la uhakika la kuuzia aina hii ya viazi.

Kwa upande wangu, nilijitahidi sana kuwatoa shaka juu ya tatizo la soko na kuwahakikishia kuwa soko la viazi lishe lipo na tena ni la uhakika, kuanzi mbegu zenyewe zile za F1 na hata viazi vyake. Nilifafanua zaidi kwa kuwaambia kuwa viazi lishe licha ya faida nyingine nyingi zinazotoa, ni chakula kitamu na chenye kupendwa sana. Na pili mwonekano wa viazi hivyo umekuwa kivutio kikubwa kwa watu wengi na kufanya visiwe na upinzani sokoni.

Mathalani, ukivuna leo tani moja ya viazi lishe vyako na ukavipeleka sokoni Jijini Dodoma kwenye soko la Maisha Plus, soko la uuzaji wa Matunda, Mbogamboga, Samaki, Ndizi na Mazao mengine jamii ya mizizi, na ikatokea kule sokoni kuna wakulima wengine wamekutangulia wenye viazi vitamu vya kawaida, pamoja na kwamba wote mna viazi vitamu, lakini wewe mwenye viazi lishe utauza mapema zaidi na kuwaacha wakulima wenzako waliyokutangulia.

Kimsingi Viazi lishe ni chakula kizuri, kitamu na chenye Vitamin A kwa wingi ambayo ni muhimu sana kwa akinamama wajawazito, wanaonyonyesha, watoto na wazee katika kusaidia uonaji wa macho, uimarishaji wa kinga ya mwili, ukuaji na kufanya maendeleo bora ya mtoto.

Watu wengi wamekuwa wakiutumia unga wa viazi lishe kama moja ya malighafi au viwambajengwa kwa ajili ya kutengenezea unga lishe wenye virutubisho mbalimbali muhimu kwa ajili ya matumizi ya makundi tofauti tofauti ya watu kama ilivyoanisha hapo juu.

Umaarufu wa unga wa viazi lishe siku za hivi karibuni umeongezeka maradufu katika jamii yetu na kusababisha watu wenye maduka makubwa kama supermarket kuutafuta unga huo kwa udi na uvumba ili kuuza kwenye maduka yao. Ndiyo maana sasa hivi siyo ajabu tena kukuta unga huu ukiuzwa kwenye aina hiyo ya maduka. Umuhimu wa viazi lishe unaoneka zaidi kutokana na kuwa na matumizi mengi.

Unga wa viazi lishe unaweza kuutumia kama ambavyo unautumia unga wa ngano kwa ajili ya mapishi mbalimbali. Unaweza kutumia unga wa viazi lishe kwa kupikia keki, maandazi, ugali, chapati na Biskuti. Aidha, viazi vyake unaweza kutumia kwa ajili ya kutengenezea Krips, Chips ama kuchemshwa kawaida au kukaangwa na kuliwa kama vitafunwa asubuhi wakati wa kupata stafutahi.

Kwa jinsi viazi hivi vilivyo na matumizi mapana, hatunabudi kukiinua zaidi kilimo hiki ili kiwe dira na mkombozi kwa mkulima katika kuinua kipato chake binafsi, kaya na taifa kwa ujumla. Kupitia viazi lishe maisha ya mkulima yanaweza kuboreka sana.

Katika jitihada zetu za muda mefu, Kinasoru East Africa Tanzania Ltd, imefanikiwa kupata soko la uhakika la kuuzia viazi lishe. Soko hilo linahitaji tani 300 sawa kilo 300,000 kwa mwezi. Soko tulilopata ni soko endelevu na ni kubwa. Mkulima mmoja au kikundi cha wakulima wachache hawawezi kumudu kutoa kiasi cha viazi kinachotakiwa.

Kwahiyo, tunahitaji wakulima wengi zaidi ambao tutaingia nao mkataba kwa ajili ya kuzalisha viazi hivyo. Na kwamba mara baada ya viazi kukomaa, mkulima atapaswa kuvipeleka viazi hivyo Dar es salaam katika ghala maalum liloandaliwa kwa ajili ya kufanya ukusanyaji wa viazi hivyo. Kama itapatikana njia nyingine bora ya kukusanya viazi hivyo kutoka kwenye mashamba ya wakulima moja kwa moja ili kurahisisha usafirishaji, basi wakati utakapofika tutawajulisha njia hiyo.

Kwa kuzingatia mzigo mkubwa unahitajika, kinasoru East Africa Tanzania Ltd, imeshindwa kuingia mkataba wa jumla na mteja wetu anaohitaji viazi hivyo kutokana na kampuni yetu kushindwa kumudu kuzalisha kiasi cha viazi kinachohitajika. Lakini hata hivyo, hadi sasa bado hatuna wakulima wa uhakika tunaowafahamu wanajishughulisha na uzalishaji wa zao hilo na wenye uwezo wa kutoa tani 300 kwa mwezi.

Ikiwa ndivyo, tukaona si vyema tukaingia tamaa kwa kujifanya tunamudu kuzalisha viazi hivyo ilihali uwezo wetu ni mdogo, ndio maana tukaamua, kwa makusudi kabisa, fursa hii muhimu tuilete kwenu wakulima wenye utayari wa kufanya kazi hii ili tuweze kunufaika kwa pamoja kupitia soko hili muhimu.

Kwa upande wetu sisi kama Kinasoru East Africa Tanzania Ltd, tutabaki kwenye kusambaza mbegu bora za F1 zenye kumhakikishia mkulima mavuno mengi kwa ekari lakini vilevile tutahakikisha kuwa kila mkulima ambaye ataingia katika programu yetu hii anapata usaidizi wa kutosha wa kiufundi katika uendeshaji wa mradi wake wa kilimo ili kuhakikisha kuwa viazi vinavyozalishwa vinakidhi ubora unaotakiwa katika soko.

Mkulima anayehitaji kujiunga katika programu hii, atapaswa kulipia ada kwenye kampuni yetu ya Kinasoru East Africa Tanzania Ltd, kwa ajili ya kugharamia ushauri wa kiufundi pamoja na kuunganishwa kwenye soko. Ushauri wa kiufundi unalenga kuhakikisha kuwa mkulima wetu anazalisha viazi bora vyenye kukidhi viwango kwa soko la kimataifa.

Aina viazi lishe vinavyohitajika kwa sasa katika soko tulilonalo ni Kabode, Mataya, Ijumla na Jewery. Na kwa bahati nzuri sana mbegu zote hizi tunazo shambani kwa hivyo ni jukumu lako sasa wewe mkulima kuhakikisha kuwa unapata moja kati ya mbegu hizo ili uendane na mahitaji ya soko.

Aidha, kama wewe ni mkulima wa siku nyingi wa viazi lishe na katika miezi mitatu uliyopita uliweza kupanda aina moja wapo kati ya aina nilizotaja hapo juu na kwamba viazi vyako kwa sasa vimekomaa na viko tayari kwenda sokoni lakini kwa bahati mbaya sana, huna soko na una ekari kuanzia mbili na kuendelea, tafadhali usikae kimya, wasiliana nasi haraka ili tuweze kuunganisha kwenye soko letu.

Bei ya jumla ya kununulia viazi vilivyokomaa ni tsh 800 kwa kilo moja na kwa gunia lenye ujazo wa kilo 100 litachukuliwa kwa tsh elfu 80. Katika mradi huu mkulima hatakopwa. Mzigo utakapofikishwa katika kituo kikuu kilichoandaliwa cha ukusanyaji, utakaguliwa kuona kama uko sawa kiubora, utapimwa uzito wake na mwisho mkulima ataweza kulipwa kadiri ya kilo alizoleta.

Tunafahamu kuwa kuna maeneo ya nchi yetu kwasasa bado kuna mvua za masika zinaendelea kunyesha lakini kuna maeneo mengine mvua hizo zimeishia. Kwa watu wanaoishi katika maeneo ambayo bado mvua za masika zinaendelea kunyesha na kuna wale ambao wako katika maeneo ambayo mvua za masika zimeishia lakini wanamudu kuendesha kilimo kwa njia ya umwagiliaji, na wangependa kuingia katika programu hii, milango iko wazi. Kila mtu anakaribishwa kuweza kushiriki katika mradi huu wenye manufaa makubwa.

Kinasoru East Africa Tanzania Ltd inatamani kuona mkulima akinufaika kupitia kilimo chake. Kama utahitaji maelezo zaidi ya ufafanuzi tafadhali usisite kuwasiliana nasi kupita anuani zetu hapo chini. Hima hima wakulima! Twende pamoja, twende shambani tukalime.

Aman Ng’oma
Mkurugenzi Mtendaji
Kinasoru East Africa Tanzania Ltd
New office location: Msalato Bible
Te: +255767989713, +255715989713 & +255786989713
Email: amanngoma@gmail.com
Facebook Page: Kinasoru East Africa Tanzania Ltd
DODOMA, TANZANIA.
 
Ada ya kiingilio kwny hiyo program ni bei ngapi? Bei ya mbegu kwa sasa ni ngapi? Na je, kama shamba lipo inagharimu bei gani kwa ekari moja kulima hadi kuvuna?
 
Ada ya kiingi
Ada ya kiingilio kwny hiyo program ni bei ngapi? Bei ya mbegu kwa sasa ni ngapi? Na je, kama shamba lipo inagharimu bei gani kwa ekari moja kulima hadi kuvuna?
Ada ya kiingilia kwa mtu binafsi ni tsh 250,000 haijalishi unalima ekari ngapi, kikundi tsh 500,000/= na kampuni au Ushirika 750,000. Lakini hizi ada siyo za kiingilio bali za kukutafutia soko, kukupa ushauri wa kiufundi pamoja na kupata mkataba wa kisheria utakaokulinda wewe mkulima na vilevile kukupa uhakika wa kazi unayoifanya.

Ada hiyo siyo lazima uilipe mwanzo, unaweza kuilipa mwishoni baada ya kuuza zao lako.
 
'SOKO LA UHAKIKA LA VIAZI LISHE, CHANGAMKIA UPESI, LISIKUPITE!'
(1)"Katika kuwajali wakulima wetu na kutambua mahangaiko yao kwenye masoko ya mazao wanayoyazalisha, kampuni ya kinasoru East Africa Tanzania Ltd imepata soko la uhakika la kuuza viazi lishe nje ya nchi kupitia wakala wao aliyepo hapa nchini."
(2)'Ada ya kuingilia kwa mtu binafsi ni tsh 250,000 haijalishi unalima ekari ngapi, kikundi tsh 500,000/= na kampuni au Ushirika 750,000. Lakini hizi ada siyo za kiingilio bali za kukutafutia soko, kukupa ushauri wa kiufundi pamoja na kupata mkataba wa kisheria utakaokulinda wewe mkulima na vilevile kukupa uhakika wa kazi unayoifanya.

Ada hiyo siyo lazima uilipe mwanzo, unaweza kuilipa mwishoni baada ya kuuza zao lako'.
Swali/maswali ya msingi.
Soko la uhakika la viazi lishe mnalo, mwanzoni mlianza kulima nyie Kinasoru East Africa Tanzania Ltd, ila mkashindwa ku.supply viazi kutokana na demand kubwa. Sasa mmerudi kuhimiza wakulima wa kawaida walime kuongeza uzalishaji, ni kwa sbb zipi mnataka ada kubwa za kutafuta masoko, ilhali soko mnalo, ushauri wa kiufundi na mkataba wa kisheria wa kumlinda mkulima kama vile sasa mmekuwa serikali au mungu tunayemtegemea ili kupata mvua au mazao mengi?
Kuwajali wakulima wetu kunaanzia wapi hasa?
 
'SOKO LA UHAKIKA LA VIAZI LISHE, CHANGAMKIA UPESI, LISIKUPITE!'
(1)"Katika kuwajali wakulima wetu na kutambua mahangaiko yao kwenye masoko ya mazao wanayoyazalisha, kampuni ya kinasoru East Africa Tanzania Ltd imepata soko la uhakika la kuuza viazi lishe nje ya nchi kupitia wakala wao aliyepo hapa nchini."
(2)'Ada ya kuingilia kwa mtu binafsi ni tsh 250,000 haijalishi unalima ekari ngapi, kikundi tsh 500,000/= na kampuni au Ushirika 750,000. Lakini hizi ada siyo za kiingilio bali za kukutafutia soko, kukupa ushauri wa kiufundi pamoja na kupata mkataba wa kisheria utakaokulinda wewe mkulima na vilevile kukupa uhakika wa kazi unayoifanya.

Ada hiyo siyo lazima uilipe mwanzo, unaweza kuilipa mwishoni baada ya kuuza zao lako'.
Swali/maswali ya msingi.
Soko la uhakika la viazi lishe mnalo, mwanzoni mlianza kulima nyie Kinasoru East Africa Tanzania Ltd, ila mkashindwa ku.supply viazi kutokana na demand kubwa. Sasa mmerudi kuhimiza wakulima wa kawaida walime kuongeza uzalishaji, ni kwa sbb zipi mnataka ada kubwa za kutafuta masoko, ilhali soko mnalo, ushauri wa kiufundi na mkataba wa kisheria wa kumlinda mkulima kama vile sasa mmekuwa serikali au mungu tunayemtegemea ili kupata mvua au mazao mengi?
Kuwajali wakulima wetu kunaanzia wapi hasa?
Ndugu yangu kampuni yetu ya Kinasoru East Africa ni kampuni inayojihusisha na kilimo biashara kupitia outgrowers. Sisi zaidi tunazalisha mbegu. Hilo ni suala la kwanza lakini suala la pili Kinasoru East Africa tunatafuta changamoto za wakulima na kuzitafutia ufumbuzi tukiwa kama wataalam wa kilimo biashara na moja ya ya changamoto kubwa inayowakabili wakulima ni masoko. Kwahiyo tunachokifanya ni kutafuta masoko kisha tunawaletea wakulima mezani mwenye uwezo wa kulima na alime. Sisi watu wa kinasoru siyo madalali bei ya soko tunayoipata ndiyo tunayoiweka wazi kwa mkulima. Kwahiyo tunacharge ada kwa kazi ya kukutafutia soko wewe mkulima. Kutafuta soko nako ni kazi ambayo siyo wakulima wote wanaweza

Kwahiyo kifupi sisi si wanunuaji wa viazi hivyo.
 
Mimi ninahiyo elimu muda mrefu kitu nilichogundua hakuna soko kwasababu watu wengi hawajui uzuri na faida ya viazi hivyo
 
Soko la hivyo viazi ni wapi?!! Hakuna soko la uhakika, hakuna muamko waw watu kusisitiza kiazi lishe anapokwenda sokoni, utalima kiazi lishe lakini utauza kama kiazi cha kawaida!
Huu ndio ukweli.binafsi nilishawishika sana lkn watu hawana elimu yoyote kuhusu viazi hivi
 
Kama kawaida upepo unahamia kwenye viazi lishe.Ndugu zangu kilimo cha kupata milioni 20 kwa heka kwa mvuno mmoja hakipo hata utambike,najua kuna watu watabisha ila watakaoamua wajaribu halafu watuletee mrejesho.Ukiamua kulima usiwe MTU wa kufuata upepo kwani ni lazima upotee
Labda kilimo cha mitiki
 
Hivi viazi ni kweli vina bei nzuri na mimi.ni mtumiaji mmoja nyumbani kwangu. Tatizo moja ni kuwa endapo supply itakuwa kubwa considering hii sio.high usage item, bei itaanguka mpaka 200-500.kwa kilo. Kwa hiyo unapoamua kuinvest kwenye hii kitu mkulima uwe cautious!
 
Haya maswala ya fursa nilishayapiga stop akilini mwangu, kilichobaki ni kutengeneza fursa za kwangu mwenyewe toka akilini
 
Viazi lishe ni aina ya viazi vitamu vyenye mwonekano wa rangi ya njano kwa ndani vikimenywa. Viazi lishe ni biashara mpya katika kilimo biashara ambacho hakijamulikwa vyema na wakulima wetu. Hii ni fursa muhimu na ya kipekee kwa wakulima wanaolenga utajiri kutokana na kilimo. Kwa kifupi huku kuna pesa kuliko kawaida. Ni muhimu tukaichangamkia fursa hii. Kilimo cha viazi lishe ni kama ilivyo kwa viazi vingine vitamu ni rahisi sana ukilinganisha na aina nyingine ya kilimo.

Viazi lishe hutumia muda wa miezi mitatu toka kupandwa hadi kuvunwa. Na kama vikilimwa kwa ajili ya mbegu, vyazi hivyo hutumia miezi miwili tu na vinakuwa tayari kuvunwa na kupelekwa shambani.

Viazi lishe vina beta karotini ambayo ni chanzo muhimu cha vitamini A. Viazi lishe vinatengeneza bidhaa mbalimbali zikiwemo Chipsi, Kripsi pamoja na Unga ambao hutumika kutengenezea bidhaa mbalimbali kama vile Mikate, Keki, Maandazi, chapati, Biskuti na vitafunwa vinginevyo. Kwa kifupi, kwa kutumia viazi lishe, tunaweza kutengeza bedhaa zote ambazo unga wa ngano unatengeneza. Majani ya viazi lishe hutumika kama mboga.

Ekari moja huitaji mbegu elfu 12 na kila mbegu moja tunaiuza kwa tsh 60/= kwa mteja anayechukua mbegu kuanzia elfu 12 na kuendelea lakini chini ya hapo mbegu moja inauzwa kwa tsh 100/=. Tunatoa huduma ya kukusafirishia hadi ulipo kwa kukupostia mzigo kwenye gari na huduma yetu ni bora sana .

Katika ekari moja una uwezo wa kuvuna tani 19 hadi 24 kutegemeana na matunzo yako. Kwa kawaida mbegu moja ya viazi lishe iliyopandwa inatoa kilo 2 za viazi. Kadiri unavyoweka matuta makubwa ndivyo unatakavyovuna viazi vikubwa zaidi. Upandaji wa viazi lishe kati ya shina moja na jingine ni futi moja moja na kati ya tuta moja na tuta jingine pia ni futi moja.

Viazi lishe ni vitamu sana. Vina unga wa kutosha na mwonekano wake huwavutia wateja wengi sokoni ukilininganisha na viazi vitamu vya kawaidi. Lakini vilevile viazi hivi vimepewa chapuo kubwa na wenzetu wataalam wa lishe kwa ajili kuboresha afya ya watoto, akina mama wajawazito pamoja na wazee.

Kilo moja ya viazi lishe inakwenda kwa tsh 1000/= sokoni. Na shina moja linatoa wastani wa kilo mbili na ekari moja ina mashina 12,000. Kwa haraka haraka ekari moja ikiwa utafuata na kuzingatia masharti yote muhimu utaweza kuvuna tani hadi 24. Sasa wewe rudisha nyuma hiyo hesabu, fanya utavuna tani 20 tu ambayo ni sawa na kilogramu 20,000. Je wajua kwa hiyo ekari moja utaweza kutengeneza tsh ngapi? Hapa utachukua 1000/= X 20,000KGS itakuwa sawasawa na tsh. 20 milioni. Hebu niambie kuna biashara gani unaweza kufanya kwa miezi michache tu ukaibuka na kiwango hicho cha pesa. Fursa ni nyingi mtaani tuzichangamkieni.

Hapo hatujaongealea biashara ya mbegu za viazi hivyo. Navyo ni hela pia. Ukiamua kuzalisha mbegu za viazi lishe kama nilivyosema hapo awali vyenyewe huchukua miezi miwili tu hadi kuvunwa. Katika ekari moja inatoa mbegu laki moja 1,046,000 na kila mbegu kwa bei inauzwa kwa tsh 30/= na sokoni kwa wale wateja wakubwa kabisa wanaochukua kuanzia mbegu 360,000 zinauzwa kwa tsh 50/=. Sasa ukichukua mbegu 1,046,000 x 30/= mkulima ataweza kupata jumla ya tsh 31,380,000/= . Je kuna biashara yeyote unayoweza kufananisha na kilimo hiki cha uzalishaji wa mbegu na viazi vyake?

Ni muhimu kukumbuka viazi ni miongoni mwa mazao yanayostahimili sana ukame hivyo vinamuhakikishia mkulima chakula cha uhakika. Vilevile kilimo hiki cha viazi lishe, hakina usumbufu kama ilivyo kwa aina nyingine ya kilimo. Ukipitisha trakta likavuruga ardhi, ukapanda mbegu kitakachofuata ni palizi tu. Kwa baadhi ya maeneo huhitaji mbolea lakini kuna baadhi ya maeneo mengine kama vile Morogoro hayahitaji hata mbolea, ukivichomeka tu basi utasubiri palizi kisha kuvuna.

Viazi lishe hustawi katika maeneo mengi ya nchi yetu lakini hustawi zaidi katika maeneo ya joto kwa mfano maeneo yote ya mikoa ya Pwani na Morogoro, maeneo yote ya Kanda ya ziwa na mikoa ya magharibi kama vile Tabora na Kigoma, Mikoa ya Kanda ya kati Singida na Dodoma pamoja na mikoa ya nyanda za juu kusini hasa Ruvuma, Rukwa na Katavi. Kwahiyo wakulima waliyo kwenye maeneo hayo wana fursa zaidi ya kuendesha kilimo hiki cha viazi lishe pamoja na mbegu zake.

Hii ndiyo fursa niliyoona niwashirikishe siku ya leo.
Kwa mahitaji yako ya Viazi lishe au Mbegu zake tafadhali wasiliana nami

Aman Ng'oma
Mkurugenzi Mtendaji
Kinasoru East Africa Tanzania Ltd
0767989713/0786989713
amanngoma@gmail.com
Dodoma.
View attachment 486804 View attachment 486805View attachment 486806View attachment 486807View attachment 486810View attachment 486811
Umewahi tengeneza hiyo 20m au mahesabu tu?
 
VIAZI LISHE SASA KUTAJIRISHA WAKULIMA

Kwa miaka mingi wakulima wa viazi lishe wamekuwa wakihangaika kupata masoko ya uhakika ya kuuzia viazi vyao na hivyo kuwakatisha tamaa katika juhudi za kuongeza uzalishaji. Kwa kuliona hilo, Kampuni ya Kinasoru East Africa Tanzania Ltd iliamua kwa makusudi kusaidia juhudi za wakulima kwenye upande wa masoko ili kuwawezesha kuuza mazao yao kirahisi.

Hadi sasa tuna soko kubwa la viazi lishe hakuna mfano wake. Kama wakulima wataamua kulichangamkia ipasavyo soko hilo, itakuwa ni fursa muhimu kwao. Wataweza kuuza viazi vyao kwa njia rahisi na kujipatia kipato.

Habari hii si hadithi, ni habari ya uhakika kabisa. Ukiwekeza kwenye kilimo cha viazi lishe lazima utajirike kwa kuwa, kwa sasa kilimo hicho si tena cha kubahatisha. Wazungu wanahitaji tuwalishe. Na Tanzania tuna ardhi kubwa yenye mabonde na mito inayotiririsha maji kwa muda wa mwaka mzima hivyo kuruhusu kuendesha kilimo wakati wote, iwe kiangazi au masika. Mungu atume nini tena.

Mkulima changamkia fursa hii, huna haja ya kuogopa kuingia kwenye hili soko. Tutakupa mkataba wako kamili huku vigezo na masharti vikizingatiwa.

Mbegu tunazo nyingi sana, bora na za uhakika. Zinatoka kwetu, Kinasoru East Africa Ltd na kwa wadau wetu tunaowaamini kama vile Taasisi ya utafiti Kibaha pamoja na SUGECO. Tuna mbegu za aina mbalimbali. Tuna Jewel, Mataya, Kabode, Kakamega, Kiyegeya, Ijumla nk. Ikiwa mabonde yetu tutweza kuyatumia ipasavyo, Tanzania itaweza kuilisha dunia yenye njaa na kutuingizia pesa nyingi za kigeni.

Wakulima tuichangamkie fursa hii ili itusaidie kujikomboa kiuchumi. Kilimo ni Biashara.

Kokote uliko kama una viazi lishe na viko tayari kwenda sokoni tafadhali wasiliana nasi kwa namba zetu hapo chini. Ni kwa viazi hivi hivi vinaweza kuwa sababu ya kukutoa kwenye umasikini. Usisubiri muujiza, ichukue hii fursa na uifanyie kazi.

Utajiri huja kwa watu wanaojishughulisha na kujihangaisha.

Aman Ng'oma
Mkurugenzi Mtendaji
Kinasoru East Africa (T) Ltd
Office location, Msalato Bible
Email: amanngoma@gmail.com
+255767989713, +255715989713 or +255786989713
Dodoma, Tanzania.
 
Aman, hebu fafanua hili. Kwenye andiko la kwanza kuhusu upandaji wa mbegu shambani ulisema kutoka tuta hadi tuta ni FUTI MOJA; katika andiko hili la pili unasema ni MITA MOJA! Which is which, FAFANUA TAFADHALI.
Andiko la kwanza nilikosea kidogo typing error lakini nilikusudia kuwaupandaji kati ya tuta na tuta ni mita moja na shina kwa shina futi moja.
 
Back
Top Bottom