Naomba taarifa na uzoefu kuhusu kilimo cha viazi mviringo Sumbawanga na Mbeya

maslulkat

Senior Member
Feb 17, 2013
107
32
Wadau ambaye anauzoefu wa Zao hili la VIAZI MVIRINGO tafadhali nisaidie kujibu na kunipatia taarifa zaidi kutokana na maswali yangu nitakayouliza hapa chini, lengo niweze kufahamu nini kinahitajika na nianzie wapi.

1. Baada ya kuandaa shamba, Ni mbegu gani nzuri zaidi?

2. Je, hekari moja inahitaji Mbegu kiasi gani?

3. Je, hekari moja inahitaji Mbolea kiasi gani wakati wa kupanda?

4. Je, ni mbolea gani nzuri sana kwa ustawi bora wa zao la viazi mviringo?

5. Je, viazi mviringo vinahitaji muda gani tena baada ya kuvipanda ili uweze kuweka mbolea nyingine na kupulizia dawa?

6. Je, mbolea hiyo bei yake ipoje?

7. Mbegu nzuri ya viazi bei yake ipoje? Hususani sumbawanga.

Tafadhali nisaidie kupata taarifa hizi au zaidi.

images%20(31).jpg
 
Kidinya, heka moja wastani wa debe 35 mpaka 40 kutegemea na ukubwa wa mbegu, mbolea ya kupandia DAP
 
Wadau ambaye anauzoefu wa Zao hili la VIAZI MVIRINGO tafadhali nisaidie kujibu na kunipatia taarifa zaidi kutokana na maswali yangu nitakayouliza hapa chini, lengo niweze kufahamu nini kinahitajika na nianzie wapi.

1. Baada ya kuandaa shamba, Ni mbegu gani nzuri zaidi?

2. Je, hekari moja inahitaji Mbegu kiasi gani?

3. Je, hekari moja inahitaji Mbolea kiasi gani wakati wa kupanda?

4. Je, ni mbolea gani nzuri sana kwa ustawi bora wa zao la viazi mviringo?

5. Je, viazi mviringo vinahitaji muda gani tena baada ya kuvipanda ili uweze kuweka mbolea nyingine na kupulizia dawa?

6. Je, mbolea hiyo bei yake ipoje?

7. Mbegu nzuri ya viazi bei yake ipoje? Hususani sumbawanga.

Tafadhali nisaidie kupata taarifa hizi au zaidi.

View attachment 2566750
Viazi Mviringo hulimwa zaidi sehemu zenye miinuko, mfano; Mbeya, Njombe, Rukwa, Kilimanjaro, Arusha n.k. Mbegu nzuri kwa maana ya kwamba inayopendwa na walaji ni Obama. Kwa wastani mbolea inayotumika kwa ekari 1 ni mifuko 3 kwa mkoa wa Njombe na Mifuko 6-10 kwa mikoa mingine. Aina za mbolea zipo nyingi ingawa kuna CAN n.k. Ukishapanda viazi huhitaji tena kuweka mbolea bali kuna zoezi la kuinua matuta na kupulizia dawa ya kuua wadudu waharibifu. Bei za mbolea ni sh. 120,000 kwa mfuko kwa mbolea ambayo si ya ruzuku wakati ya ruzuku ni sh. 70,000 kwa mfuko. Bei ya mbegu hutofautiana kulingana na upatikanaji wake, Kwa mkoa wa Njombe na Mbeya ni kuanzia sh. 50,000 - sh. 70,000 kwa kiroba kimoja cha mbegu. Nawasilisha.
 
Hiyo mbolea ya ruzuku utaratibu wake upoje, na maana yake ni nini?
 
Back
Top Bottom