Furahi panapofurahisha

ladyfurahia

JF-Expert Member
Joined
May 10, 2011
Posts
14,758
Reaction score
9,592
Hay wanajamvi wenzangu

Leo mwenzenu nimeona nifurahi zaidi ya kfurahi kwa jambo ambalo Mungu
amenitendea leo mwenzenu,nimebahatika kukutana au kuona jambo langu
ambalo nilimwomba Mungu kwa muda mrefu naye ametenda? wewe je
rafiki yangu ukiona umetendewa utafurahi zaidi pale panapokufurahisha?


Naomba mjumuike pamoja nami kufurahi panapofurahishwa zaidi kwangu
kwani muolmba kwa mola hakosi dua yake kusikilizwa na kutendewa.
Sitaki niingie ndani zaidi kujua nn nimetendewa kwa muda wake kila
mwana MMU aingie kule aniulize nami nitamjibu bila woga au mnataka
kukua hapa hapa. Acha niwamegee kidogo vile Mungu alivyonitendea
NilimwombaMungu anipe uzima, afya njema, na hekima toka kwake nae
leo kanijibu kwa maombi yangu kwani nimemuona Mungu kwangu akifungua
madirisha yake, na kuanzia April naenda soma chuo, nawasihi wale wote
wanaomwomba Mungu wasikate tamaa kwani yuko yeye aonaye taabu
yao naye atakwenda kutenda kwa wakati wake msipozimia mioyo yenu
kwani yeye anajua taabu , mazito, na magumu, majaribu, na mateso
mnayopitia naye ndiye anayetuwezesha na kutushindia
Rafiki yangu mara upatapo muda soma hapa Jeremiah 32:27 'Behold, I'm
the LORD, the GOD of all flesh; is there any things too hard for me?
Hakuna jambo linaloweza kumshinda Mungu, hebu mtumaini, mtegemee
naye atafanya njia na mlango wakutokea katika taabu yako

Mbona amefanya kwangu na nimepata kicheko na furaha iweje kwako
mpenzi wangu rafiki yangu ukate tamaa kwa jambo upitalo.
naomba usikate tamaa hata kama unaona kiza leo, kesho yako nzuri inakujilia
JIFUNZE KUMTEGEMEA, KUMTUMAINI MUNGU NYAKATI ZOTE NAYE ATAFANYA
NA KUKUPA KICHEKO NA FURAHA NAWE UTAFURAHI KAMA MM NINAVYOFURAHIA
PANAPOFURAHISHA.

COPY: @
nicas mtei, The hammer, Bakulutu, Madame B, gfsonwin, sweetlady, Bujibuji (vipi mbona lile kongamano la PRAISE NA WORSHIP la CC umeshasahau au alipo ), Zion Daughter, Mamndenyi, watu8, my beloved bro Erickb52, Arushaone, Excellent, sokwe, (my cousin) charminglady , Mr. Rocky Sean Ruttashobolwa, ruttashubanyuma, manoah (mtukuttu) Bishanga, Baba V, Von Mol, Mentor (my husband to be), Roullete na wote marafiki zangu wa jf cc, na kuleeeeee

Nawatakia pasaka njema pokea hiyo kagift kadogo sana hako
na lingine la upendo zaidi kwenu wote marafiki zangu hilo pokea
 
Last edited by a moderator:
Hongera sana. Asante kwa kunipa moyo manake na mie nna hitaji moja namuomba Mungu afanye muujiza hapa. Najua sistahili, lakini Yesu si alikufa msalabani tena kifo cha aibu ili tusiostahili tustahilishwe?

Im happy for you. When you are blessed i feel double blessed. Sasa huyo mchumba ungempa kichumba cha hapo kando kabisa akae hapo hadi umalize chuo. Ukimaliza chuo kama bado hajawa kibabu (ama kawa kibabu handsome aka mwenye mahela) tunawaozesha.
 
Hongera sana.
kumbuka kumshukuru Mungu wako kwa kila jambo,
si kwa kupata tu hata kwa kukosa pia kwani inawezekana
umekosa ili utukufu wake uonekane.
 
Hongera sana ladyfurahia! Mungu ni mwema na ujibu kwa wakati! Hongera sana!

Asante pia kwa wishes za pasaka, nawe uwe na pasaka njema!
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…