Jeshi la Kuezeka

Jeshi la Kuezeka

RRONDO

Platinum Member
Joined
Jan 3, 2010
Posts
58,243
Reaction score
131,047
Kuna kajumba ka kupangisha nimekajenga sehemu. Nyumba hii ni vyumba vitatu vya kulala,sebule,jiko na vyoo viwil kama kawaida.

Sasa wakati wa kuezeka kama kawaida nilivyozoea najua ni kazi ya siku 3-5. Fundi alienijengea akaniambia ana watu wake wa kuezeka wanaezeka kwa siku moja tu yaani wanakuja asubuhi 0600 jioni 1800 wanakabidhi kazi! Nikamuuliza mara mbili mbili akaniambia wanaweza na kazi ni kiwango.

Akaniunganisha na hawa mafundi. Wakanipa list ya material na wakasema wanaweza kulala site ili waanze saa 0600 nikawaambia site hairuhusu kulala au kutumza vifaa basibwakasema watakuja asubuhi.

Asubuhi wakafika pale saa 0600 mpaka vifaa kufika site wakaanza kazi 0800. Mimi nilifika site around 1600 hivi na nilikuta wanamalizia kuweka mabati sehemu iliobaki kama robo tu ya nyumba nzima. Na kazi ilikuwa kiwango cha juu. Kufika 1830 wamemaliza na wakasema kama vifaa vingewahi ningekuta kazi imeisha.

Kwa kweli nilishazoea kuezeka ni kazi ya siku tatu na kuendelea. Nyumba ilitumia mabati 95, mbao 2*2 100pcs na 2*4 150pcs. Mafundi walikuwa 8. Wote mafundi hakuna kibarua.
 
Nje ya mada; wameezeka vizuri sana na kitaalamu. Kitaalamu mlingoti wa paa "King Post" haitakiwi kuwa ndefu zaidi ya nusu ya ukuta wote.

Ukizidisha hapo unakuwa mshamba, paa linakuwa mara mbili ya urefubwa nyumba. Ni ushamba. 😊
 
RR hakuna nyumba ya kuezeka siku tatu, mafundi nane hapo. 😁
Hata hivyo hongera kwa mjengo mkuu.
Kawaida huwa anakuja fundi mmoja au wawili na vibarua. Hawa huwa wanatumia siku 3-4 wakijitahidi siku 2. Hawa jamaa wanakuja kulingana na ukubwa wa nyumba na wanamaliza siku moja tu.
 
Hata mbili ni nyingi sana kwa mafundi nane Mbaga. Watu wawili wanabaki chini, watu sita wapo juu.
Wanagawana mapande, nyumba ya kukata iyo, huyu anashika upande huu, huyu anashika huku. Ni nyundo tuu. 😁
Kwa idadi ya watu 8 tena hawa n mafundi kabisa sio saidia fundi n sahihi kumaliza kwa siku moja, mafundi hawa hawa wakiwa wanne siku mbili wanamaliza
 
Hujaelewa mkuu. Hawa 8 ni siku moja tu. Kawaida huwa natumiabfundi wawili vibarua wawili ndio wanatumia siku 3 au 4
 
Kawaida huwa anakuja fundi mmoja au wawili na vibarua. Hawa huwa wanatumia siku 3-4 wakijitahidi siku 2. Hawa jamaa wanakuja kulingana na ukubwa wa nyumba na wanamaliza siku moja tu.

Hao ni mafundi wazoefu na wanajua maana ya muda, ndio maana wameji organize, bora wafanye kazi moja watu wengi iishe wagawane, kuliko wakae hapo siku tatu! Akili mtu wangu.

Maana yake hizo siku tatu wanafanya kazi ndogo ndogo kama hizo nyingi.
Hapo wenda kesho wataamkia kwingine kupiga kazi.
 
Kwa idadi ya watu 8 tena hawa n mafundi kabisa sio saidia fundi n sahihi kumaliza kwa siku moja, mafundi hawa hawa wakiwa wanne siku mbili wanamaliza
Na ndio nilichosema. Kawaida huwa natumia mafundi wawili na vibarua wawili wanachukua siku 3-4. Hawa jamaa nyumba yoyote wanafanya siku moja ndio utaratibu wao. Wanakuja idadi fulani kulingana na ukubwa wa jengo.
 
Hao ni mafundi wazoefu na wanajua maana ya muda, ndio maana wameji organize, bora wafanye kazi moja watu wengi iishe wagawane, kuliko wakae hapo siku tatu! Akili mtu wangu.

Maana yake hizo siku tatu wanafanya kazi ndogo ndogo kama hizo nyingi.
Hapo wenda kesho wataamkia kwingine kupiga kazi.
Na ndio utaratibu wao. Mjmi niliwazoea wa siku 3-4
 
Hujaelewa mkuu. Hawa 8 ni siku moja tu. Kawaida huwa natumiabfundi wawili vibarua wawili ndio wanatumia siku 3 au 4

Ukitumia mafundi wawili, vibarua wawili ni lazima wafanye kazi hiyo siku nne. Watu 8 mafundi, nyumba kama hiyo siku moja tuu, ndio maana yangu.
 
Back
Top Bottom