Fuga nguruwe wako kisasa uwaepushe na magonjwa, jipatie automatic drinker

zinaitwa nipple drinker .... zinahitaji uwe umefanya plumbing installation kwa ajili ya mzunguko Wa maji
 
Unapomuwekea maji nguruwe kwenye beseni/sehemu iliyojengewa kwa sementi kuna wakati nguruwe huyo huingiza miguu yake ndani ya hayo maji na kuendelea kuyanywa hivyo humuweka nguruwe katika hati hati ya kupata minyoo.

Suluhisho, kuna automatic drinker za nguruwe ambazo unaweza kuzifunga katika chumba cha nguruwe hivyo nguruwe akitaka kunywa anaenda moja kwa moja kunywa.

Kifaa hicho ni kama koki ya maji tu (mfano) ambayo nguruwe anaenda kunyonya akitosheka anaacha, maji yanakuwa yanatoka kwenye tank yanafikia.

Ndani ya chumba kimoja cha nguruwe unaweza kuweka mbili au tatu, ukihitaji wasiliana nami. Nauza 9,500 tu kwa pisi moja.

Angali Picha
Mimi nahitaji sana. Nipe mawasiliano nikutafute.
 
Swali zuri sana na mimi mwenyewe ndo nililojiuliza la kwanza

ni rahisi sana ..... baada ya ku-install nipple drinkers unawapa nguruwe wako chakula cha pumba kikavu wanakula kwa muda ..... halafu watasikia kiu sana ..... utaingia kwenye banda lao na kuibonyeza we we hiyo nipple drinker kwa kidole Maji yatatiririka halafu nguruwe wataona Maji yanatokea wapi ..... na hapo nipo mwanzo wa nguruwe kwenda kwenye Nipple drinker na kuibonyeza kwa meno na hatimaye kufanikiwa kunywa maji
 
Back
Top Bottom