Fuel consumption toyota Rav 4 VX 1999

ISO M.CodD

ISO M.CodD

JF-Expert Member
4,794
2,000
Gari ina nguvu? Kama haina cheki na upumuaji kwenye exhaust system (mufflers) .

Halafu kupima utumiaji wa mafuta kwa kuempty tank zima ni kosa. Unaweza kuingiza mafuta machafu kwenye mfumo since mafuta yanayokuwa kule chini kabisa huwa ni machafu..

Njia nzuri zaidi ni kujaza full tank, kuendesha kwa kilomita kadhaa, kisha kurudi kwenye pump ile ile uliyojaza full na kujaza full tank nyingine. Note zile lita zilizoingia ulipojaza full tank second time.

Gawanya kilomita ulizotembea kwa lita ulizojazia. Done.
 
jacobcm8

jacobcm8

Senior Member
134
225
gari inanguvu ila kuna muda inakosa nguvu unakanyaga accelerator inakuja kuchanganyaa badae sana..... ila hata nkiweka sailensa nka kanyaga accelerator inatoa sauti ya ovyo uku kwenye engine kama kuna uwazi kwenye mfumo wa exhaust...............
fuel injector walibadili ila wapi... nikimalza mitihan nataka waicheki labda engne ndio shda....
kwenye exhaust yanatokaga maji mengi nilijuaga n tatzo nkaambiwa sio. moshi siuonagi... kama upo labda navostart tu nao n kdgo..
Gari ina nguvu? Kama haina cheki na upumuaji kwenye exhaust system (mufflers) .

Halafu kupima utumiaji wa mafuta kwa kuempty tank zima ni kosa. Unaweza kuingiza mafuta machafu kwenye mfumo since mafuta yanayokuwa kule chini kabisa huwa ni machafu..

Njia nzuri zaidi ni kujaza full tank, kuendesha kwa kilomita kadhaa, kisha kurudi kwenye pump ile ile uliyojaza full na kujaza full tank nyingine. Note zile lita zilizoingia ulipojaza full tank second time.

Gawanya kilomita ulizotembea kwa lita ulizojazia. Done.
 
jacobcm8

jacobcm8

Senior Member
134
225
poa poa boss
sasa kuna starlet ilikuja hapa gereji mtaani sehemu ambayo mimi naweka mafuta ya elfu 30 arusha mjini to makumira university yeye mwenye starlet alitumia kama mafuta ya elfu 50......
walifungua engine wakakuta KUNA VITU IMEUA ikiwemo nozeli zlikufa baadhi....wamefix jamaa anakula maisha na mm naiman ntafix tuu....ngoja UE ipite.
 
C

Christel U

New Member
1
20
2000cc
kwa hiyo 1 litre km 3 plus na siyo 1 litre km 8 plus kwa hiii gari
izo km 14 inatembea hadi kuzima mafuta nloweka niya elfu 10 ambayo n kama 4.4 litres
kwa iyo 4.4 kwa 14 km ni sawa?
Sio sawa
 
jacobcm8

jacobcm8

Senior Member
134
225
Gari ipo Garage itafanyiwa Engine Overhauling kesho asubuhi.....mkuu
nlibadil pump juzi na kucheck oxygensensor leo kama ilivodai diagnosis machine naona imesogea sogea hadi 1litre per 5km.......naona improvement
kezho ovahauling maana inakosa nguvu kizembe kwenye mwinuko mdogo fundi kasema mlio wa injine sio sawa........lazima wachek cylinder head, gasket, piston na wasage valve ... tufunge thermostat maana iliungwa feni direct..
 
mng'ato

mng'ato

JF-Expert Member
23,503

Weka engine mpya tu mku Usiweke mswaki
 
J

julius milla

JF-Expert Member
634
500
Nenda N I T mtafute mhandisi Jackson Kiando ataikomesha.
 
muzi

muzi

JF-Expert Member
826
1,000
Duuuu pole sana, hilo tatizo linahitaji mafundi wazoefu na sio wale wa vijiweni wanaojifunza kazi kulingana na tatizo. Ukifanikiwa tujulishe gereji ipi waliweza kutarua tatizo na tatizo kubwa lilikuwa nini.
 
jacobcm8

jacobcm8

Senior Member
134
225
Duuuu pole sana, hilo tatizo linahitaji mafundi wazoefu na sio wale wa vijiweni wanaojifunza kazi kulingana na tatizo. Ukifanikiwa tujulishe gereji ipi waliweza kutarua tatizo na tatizo kubwa lilikuwa nini.
kweli kaka kama ulivosema gari limetoka garage juzi sasa lipo katika ubora wake lina nguvu safi.....nmezunguka sana ila tatizo limetatuliwa GARAGE YA DUTI IPO MAKUMIRA ARUSHA AISEE hawa jamaa ni mafundii watu wanatoka mjini wanaleta magari pande hizi....

Alisikiliza mlio akanambia Engine yakufungua
TUKAFUNGUA akabaini vitu vifuatavyo
1. Cylinderhead inashida tukaenda kuifanyia clearance mm na yy mpaka mjini nikanunua na OVERHAUL
2. Ring piston zmeisha
3. Main and CONe zliisha
4. kuna kama vicoin vya sh 500 ya nchi yetu sjui vnaitwaje ila vilibadilishwa pia kwenye cylinder head maaana aliyeniuzia gari alifanya modifikesheni ya kijinga aliongezea spacer ( vibati vya duara kama coin ya 500) kwenye hzo coin baada ya kuona zmeisha ntatuma picha badae...
5. Walisaga Valve
6. kwenye piston waliakikisha zile tundu za kupitisha oil zote ziko waz nyingi ziliziba hivo oil ilikua haipiti kupelekea ring kulika....
7. nimefunga thermostat mafeni yanavofunguka automatic had raha .... mwanzoni engine ilikua inapozwa muda wote hivo kupoteza ufanisi...

oVERHAUL imenisaidia sana mana gari saiv haina leakage yoyote gasket zote mpya...

Wasingekkua hwa jamaa nilitaka kuuza hii gar manaa nligive up mana mafundi wengi ni wa kuuunga unga ....na nmepoteza kwel ela ... fundi ananibadlishia OIL natembea hata km 100 hazfiki oil nziiiito kumbe imeunguzwa .......
again GARI IPO MKAO SASA .....

pichani n vitu nlivokuta kwenye en gine havitakiwi kuwa na spacer
hizo coin inabd ziwe nene..

sakasaka

sakasaka

Senior Member
188
225
Mkuu kwa zoezi hili lote umetumia kama shiling ngapi?
 
jacobcm8

jacobcm8

Senior Member
134
225
Almost laki 9 hv kuanzia kubadil nozeli hadi engne overhauling.. Na ufundi. Pamoja na vifaa vidogo kama thermostat. Etc
 
mng'ato

mng'ato

JF-Expert Member
23,503
2,000
Almost laki 9 hv kuanzia kubadil nozeli hadi engne overhauling.. Na ufundi. Pamoja na vifaa vidogo kama thermostat. Etc
Hongera mkuu kwa machine kurudi road,sa hivi consumption imekaaje kwa lita?
 
jacobcm8

jacobcm8

Senior Member
134
225
Hongera mkuu kwa machine kurudi road,sa hivi consumption imekaaje kwa lita?
NMETOKA MAKUMIRA ARUMERU TO MOSHI (PASUA] KWENDA KURUDI NILIWEKA MAFUTA YA 30 elfu = 13.2 litres nmetembea zaid ya kilomita 160 (kwenda moshi na kurudi] speed 80-100 inapobidi 50 nmetumia online calculator inaonesha gari inaenda 12 KM PER LITRE.... Kama ifuatavyo View attachment 737967
 
Extrovert

Extrovert

JF-Expert Member
22,264
2,000
hapo umeweza kuo reset engine haswa. Hio ndio Rav 4 sasa ile ya mwanzo ilikuwa scania mende
NMETOKA MAKUMIRA ARUMERU TO MOSHI (PASUA] KWENDA KURUDI NILIWEKA MAFUTA YA 30 elfu = 13.2 litres nmetembea zaid ya kilomita 160 (kwenda moshi na kurudi] speed 80-100 inapobidi 50 nmetumia online calculator inaonesha gari inaenda 12 KM PER LITRE.... Kama ifuatavyo View attachment 737965 View attachment 737967
 
Jephta2003

Jephta2003

JF-Expert Member
5,107
2,000
Jaman msaada gari yngu toyota rav 4 vx old model 1999 naona haipo sawa kwenye ulaji mafuta

Nikashauriwa niendeshe izime then niweke mafuta kidogo kwa ajili ya testing
Nikaweka mafuta ya 10,000 ambayo ni kama 4.4 litres hivi distance covered 13kilometers

Lilipozima nilirudia tena kuweka petrol ya 10,000 distance covered ikawa around 14 kilometers licha ya

1.Kubadili fuel filter

2.Kuweka sparking plugs mpya zote nzima

3.Nyaya za plugs mpya zote nzima

4.Fuel system throttle body ( regulate the amount of air that flows into the

Engine more details on - what is a fuel system 'throttle body'?)
Icho kifaa kilikua checked pia kiko freshi

Gari imetembea kilometers kama laki na arobaini tu [140,000]

Nimeuliza maana naambiwa atleast itembee 10 upto 14 kilometers per litre kwa hii gari

Wataalamu naombeni ushauri shida inaweza kuwa nini
Kama ulikua unatestia kwenye barabara ya foleni kubwa unategemea matokeo gani?
 
Forum statistics

Threads
1,424,986

Messages
35,078,036

Members
538,184
Top Bottom