FT: Ligi Kuu Bara | Simba SC 3-0 Dodoma Jiji FC | Uwanja wa Mkapa 02/10/2022

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea kupigwa leo Oktoba 2, 2022, ambapo Mnyama Mkali Mwituni Simba SC, atakwaruzana na Walima Zabibu Dodoma Jiji FC kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mechi huenda ukawa ngumu kwa pande zote mbili, hasa ukizingatia kwa kila timu kujipanga ili kupata matokeo ya ushindi.

Kocha Msaidizi wa Simba SC amesema kuwa, wamepata muda wa siku mbili kufanya mazoezi baada ya kurudi Zanzibar na wanajua utakuwa mchezo mgumu licha ya Dodoma Jiji kuanza vibaya Ligi, lakini wamejipanga kuhakikisha wanashinda.

Naye Kocha Msaidizi wa Dodoma Jiji FC amesema kuwa, watapambana kulingana na Simba anavyocheza na watahakikisha kwenye mchezo wa leo wanakwenda kucheza kwa ushindani ili wapate ushindi mwingine wa pili kwenye Ligi Kuu.

Je nani atakubali kupigwa mweleka? Ngoja Tusubiri Kuona Ndani ya Dakika 90.. Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1:00 Usiku.. Usikose Ukapata Simulizi.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana

================

Timu zinaingia uwanjani kufanyiwa ukaguzi pamoja na kupiga picha za kumbukumbu kuashiria kuanza kwa mchezo.

Refa wa katikati ni Ramadhan Kayoko

Naaam mpira umeanza Uwanja wa Mkapa | Simba SC 0-0 Dodoma Jiji FC

04' Goooooooooooooaaal gooal
Abdallah Shaibu anajifunga baada ya kupiga kichwa cha nyuma kuelekea lango lake | Simba SC 1-0 Dodoma Jiji FC

10' Mkude anaonyeshwa KADI ya Njano baada kuchezea vibaya Ngalema.

Opare anapiga shutii lakini linapaa nje ya lango la Simba SC.

Mwana Kibuta anaonyeshwa KADI ya Njano baada kuchezea vibaya Israel

20' Chama kwake Kibuuuuu, lakini mpira unatoka sentimita chache ya lango la Dodoma Jiji

Israel anapoteza mpira, Kwake Martin anapiga shutii lakini linatoka nje na kuwa goal kick

28' Phiri upo chini akipatiwa matibabu baada ya kupata rabsha, mpira umesimama, amerudi uwanjani mpira unaendelea

Wanakwenda sasa Dodoma Jiji, kwake Martin kwake Mwaterema Offside.

32' Wanamiliki Simba kwake Chama anapiga shutii looo njee, ilikuwa nafasi nzuri ya kufunga

Nafasi kwa Dodoma Jiji nao wanashambulia lango la Simba, Opare anapiga njeee.

35' Phiri anapiga shutii lakini mpira unatoka sentimita chache ya lango la Dodoma Jiji, ilikuwa nafasi ya dhahabu

Kasi ya mpira imepungua huku kila timu ikipoteza nafasi kadhaa za kufunga mabao.

Kwake Chama pasi murua lakini Kibu anachelewa kuwahi mpira, namna gani Kibu

41' Simba SC wamenapata Kona ambayo haikuzaa bao, mpira wanao Dodoma Jiji

Justine Bilaly anaonyeshwa KADI ya Njano kwa kumchezea madhambi Phiri

Phiri Goooooooooooooaaal gooal

Moses Phiri anahesabu bao la pili akipiga shuti kali la chini chini na kumuacha golikipa Aron akiruka bila mafaniko | Simba SC 2-0 Dodoma Jiji FC.

45+2' Kuelekea kuwa mapumziko ambapo Simba wapo mbele ya mabao mawili.

Naaam mpira ni mapumziko

Kipindi cha pili kimeanza uwanja wa Mkapa

Ametoka Justine Bilaly na ameingia Karihe upande wa Dodoma Jiji

SIMBA wamepata Kona mbili mfululizo ambazo hazikuzaa bao, mipira yote ya Kona imeokolewa.

48' Golikipa Aron Karambo yupo chini akipatiwa matibabu ameinuka mpira unaendelea.

Nkosi anapiga shutii lakini golikipa Manula anadaka huku akiwaambia wachezaji wake watulie.

Kibu anapangua mabeki lakini anapoteza mpira kizembe kabisa namna gani Kibu

Hassan Kessy anaonywa na mwamuzi baada ya kumuingia vibaya Chama

58' Bocco anakosa nafasi nzuri ya kufunga ilikuwa Shambulizi kali kuelekea lango la Dodoma Jiji lakini golikipa Aron anadaka shuti lile.

Ametoka Mwaterema na ameingia Chambo upande wa Dodoma Jiji

Phiri anachambua Beki kwake Bocco lakini anachelewa kuwahi mpira

Haya kwake Bocco, pasi murua kutoka kwa Chama anapiga Bocco lakini mpira unagonga Mlingoti

67' Mashambulizi yanazidi kuelekea Dodoma Jiji sasa, Simba wanakosa nafasi nyingine kupitia kwa Chama

Karihe anapiga Krosi lakini hakuna MTU na anauwahi mpira Israel anaondosha

Collins Opare anajaribu kumtingisha Hussein lakini anakataa

Dodoma Jiji wamefanya Shambulizi kali mno, Almanusura wapate bao.

Wachezaji watatu wa Dodoma Jiji FC wameingia kuchukua nafasi za wengine akiwemo Hoza

Bocco anaunyanyua mpira na kumpita golikipa Aron, lakini unatoka nje na kuambaa ambaa kule.

81' Ametoka Kibu na Bocco na nafasi zao zimechukuliwa na Okwa na Kyombo

Simba wanapata Kona ambayo haikuzaa bao huku Dodoma Jiji wakishindwa kabisa kupata nafasi

85' Kyombo Goooooooooooooaaal gooal

Habibu Kyombo anaandika bao la tatu kwa kichwa akipokea Krosi ya Hussein | Simba SC 3-0 Dodoma Jiji FC.

Mzamiru anaonyeshwa KADI ya Njano kwa mchezo mbaya huku Simba wakifanya mabadiliko

88' Ametoka Phiri na ameingia Nyoni

90+3' Kuelekea kumalizika kwa mchezo wa Ligi Kuu

Opare anapiga shutii lakini golikipa Manula anadaka na unamtoka, Beki Hussein anaondosha hatari ile.

Okwa anakosa nafasi ya wazi hapa

Naaam mpira umekwishaaaaaa ambapo Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao matatu kwa bila dhidi ya Dodoma Jiji FC.

FT; Simba SC 3-0 Dodoma Jiji FC

..... Ghazwat...
 
Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea kupigwa leo Oktoba 2, 2022, ambapo Mnyama Mkali Mwituni Simba SC, atakwaruzana na Walima Zabibu Dodoma Jiji FC kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.

Mechi huenda ukawa ngumu kwa pande zote mbili, hasa ukizingatia kwa kila timu kujipanga ili kupata matokeo ya ushindi.

Kocha Msaidizi wa Simba SC amesema kuwa, wamepata muda wa siku mbili kufanya mazoezi baada ya kurudi Zanzibar na wanajua utakuwa mchezo mgumu licha ya Dodoma Jiji kuanza vibaya Ligi, lakini wamejipanga kuhakikisha wanashinda.

Naye Kocha Msaidizi wa Dodoma Jiji FC amesema kuwa, watapambana kulingana na Simba anavyocheza na watahakikisha kwenye mchezo wa leo wanakwenda kucheza kwa ushindani ili wapate ushindi mwingine wa pili kwenye Ligi Kuu.

Je nani atakubali kupigwa mweleka? Ngoja Tusubiri Kuona Ndani ya Dakika 90.. Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1:00 Usiku.. Usikose Ukapata Simulizi.

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana
Itoshe kusema kuwa Phiri anaenda kuandika hat trick yake ya kwanza NBCPL
 
Hii hapa ni ratiba ya Simba SC kwenye michezo yake ya mwezi wa Oktoba
20221002_151120~3.jpg
 
Back
Top Bottom