FT: Ligi Kuu Bara | Dodoma Jiji FC 0-1 Simba SC | Jamhuri Stadium 22/01/2023

Ghazwat

JF-Expert Member
Oct 4, 2015
23,718
66,262
Baada ya kuachia kipigo cha 3-2 dhidi ya Mbeya City🟣 katika ile Patashika ya Ligi Kuu Tanzania Bara, leo January 22, 2023 Wataalamu wa kusakata kabumbu ukanda huu EAC na COSAFA Wekundu wa Msimbazi Simba SC wapo ugenini kuwakabili Wenyeji Walima Zabibu Dodoma Jiji FC kwenye mchezo utakao vurumishwa Dimba la Jamhuri Makao Makuu ya Nchi Jijini Dodoma.

Kocha Msaidizi wa Dodoma Jiji FC Kassim Liogope amesema kuwa " Tupo Nyumbani tunakabiliana na mechi ngumu, lakini sisi kama Dodoma Jiji tumejipanga vizuri na kukabiliana na Simba, moja timu bora Afrika" amesema Kocha Liogope.

Kocha Mkuu wa Simba SC Robertinho Mbrazil, amesema kuwa "Tuna nafasi ya kuonyesha Simba SC ni Timu Kubwa, baada ya Kambi ya wiki moja Dubai kufanikiwa tunahitaji kushinda na kuonyesha soka safi, ili kuwa bingwa lazima kuchukua alama tatu". Amesema Kocha Robertinho.

Je Robertinho ambapo ni mechi yake ya pili kwenye Ligi Kuu ataendeleza moto ule ule wa mchezo uliopita kwa Simba SC ambayo huenda ikakosa huduma kutoka kwa nyota wake kadhaa wenye viwango vya juu, kwasababu ya Majeruhi na Kadi za Njano🟨?

Yote ni dakika 90 Kuamua..Kumbuka mchezo ni kuanzia saa 1:00 Usiku

Kulitaka Mwana Kulipewa Mwana

..... Ghazwat...


=============================

Timu zote mbili zipo uwanjani zikipasha misuli moto tayari kwa mchezo.

00' Naaam mpira umeanza Uwanja wa Jamhuri | Dodoma Jiji 0-0 Simba SC

05' mchezo umeanza kwa kasi huku Simba SC wakifanya mashambulizi mawili, kupitia kwa Baleke na Ntibazonkiza kwa mpira wa faulo ambao haujuzaa bao.

10' Kibu anakosa nafasi nzuri ya kufunga, mpira unaokolewa na mabeki wa Dodoma Jiji.

12' Dodoma Jiji, wanajaribu kulifikia lango la Simba, lakini Opare ni Offside.

17' Bocco anapoteza nafasi ya kufunga baada kupiga shutii hafifu lango la Dodoma Jiji

19' Ntibazonkiza anaonyeshwa Kadi ya Njano kwa kumchezea madhambi mchezaji wa Dodoma Jiji

25' Mwaterema anakosa nafasi nzuri ya kufunga, golikipa Manula anadaka shutii dhaifu bila wasiwasi ilikuwa nafasi bomba.

30' Kennedy anaonyeshwa Kadi ya Njano kwa mchezo mbaya, ni free kick kuelekea Simba, inapigwa kulee lakini mpira unababatiza mabeki wa Simba.

32' Kibuta anaonyeshwa Kadi ya Njano kwa kumchezea madhambi Ntibazonkiza

35' Ntibazonkiza anawekwa chini eneo la 18 lakini Refa anakataa anasema cheza mpira hizo ni shida zako TU

Muhsin anapiga shutii lakini linapaa nje ya lango la Simba SC.

41' Opare anapiga shutii lakini Refa anasema kabla hujapiga uliunawa kwahivyo ni faulo.

45+2' Kuelekea kuwa mapumziko

Unapigwa mpira mrefu kwake Kibu anagonga kichwa cha mparazao kwake Balekeeeee

Baleke Goooooooooooooaaal gooal

Jean Beleke anaweka kambani bao la kwanza | Dodoma Jiji FC 0-1 Simba SC

HT: Dodoma Jiji FC 0-1 Simba SC

Kipindi cha pili kimeanza huku Nsata akionyeshwa Kadi ya Njano kwa kumchezea madhambi Baleke

50' Bilary anaonyeshwa Kadi ya Njano kwa kumchezea madhambi Kibu, ni faulo inapigwa kulee kwake Sawadogo anapiga kichwa lakini mpira unatoka nje.

53' Dodoma Jiji wanapata Free Kick inapigwa kulee lakini wanaokoa hatari ile Simba SC

57' Kibuyu kinalia, na Kadi ya Njano inatoka kwa upande wake Opare baada ya kuchelewa faulo Hussein

60' Wachezaji wa timu zote wanajaribu kufikia eneo la upinzani lakini umaliziaji si nzuri.

Sawadogo anaonyeshwa Kadi ya Njano kwa kumchezea madhambi mchezaji wa Dodoma Jiji

Sereri ameingia kuchukua nafasi ya MTU upande wa Dodoma Jiji, huku wakipata kona ambayo haikuzaa bao

71' Kapama ameingia kuchukua nafasi ya Sawadogo, upande wa Simba

Umiliki wa Dodoma Jiji sasa, lakini wanashindwa kutumia nafasi wanazopata

83' Ametoka Bocco na Baleke na wameingia Okrah na Kyombo upande wa Simba

Raizin ameingia kuchukua nafasi ya Muhsin na ameingia Karihe badala ya Opare

88' Karihe anaonyeshwa Kadi ya Njano, Kumbuka ameingia hivi punde katika dakika hizi za lala salama.

99+2' Kuelekea kumalizika kwa mchezo, Dodoma Jiji wanapata Kona, inapigwa kulee lakini golikipa Manula anadaka

Naaam mpira umekwishaaaaaa ambapo Simba SC wanaibuka na ushindi wa bao moja kwa bila dhidi ya Dodoma Jiji FC.

FT: Dodoma Jiji FC 0-1 Simba SC

.... Ghazwat..
 
20230122_150821.jpg
 
NUKUU:

Mwanzo niliwaambia nina vitu viwili akilini kwangu nataka kuviingiza hapa Simba, moja ni timu kushinda kila mechi, mbili ni kucheza vizuri kwa kasi.

Kwa maana hiyo kila mchezaji anaweza kuwa bora kama atavitambua hivyo na kuvifanyia kazi.

-Kocha Robertinho.
 
Kocha anawapa morari sana wachezaji na mashabiki pia,si mgunda kila siku ooh dodoma ni timu nzuri tunawajua ,tunaheshimu na blabla kibao zinazojirudia
Alikuwa anajiona bado yupo katika timu ndogo Coastal Union kumbe ni Timu Kubwa Simba SC, ndo maana alikuwa akisema hayo.

Mkuu hyperkid kumbe ulikuwa unamfuatilia sana kwenye mikutano yake na waandishi wa habari.
 
Back
Top Bottom