FT: Chelsea FC 3-0 Paris Saint-Germain | FIFA Club World Cup | Final Match | MetLife Stadium | July 13, 2025.

FT: Chelsea FC 3-0 Paris Saint-Germain | FIFA Club World Cup | Final Match | MetLife Stadium | July 13, 2025.

kiwatengu

Platinum Member
Joined
Apr 6, 2012
Posts
19,225
Reaction score
17,649
images.jpeg

Mambo vipi wadau! Leo ni siku ya kipekee kwani tunasubiri fainali ya FIFA Club World Cup 2025 kati ya Chelsea na Paris Saint-Germain (PSG) itakayochezwa saa nne usiku (10:00pm EAT) kwenye dimba la MetLife Stadium, New Jersey.

Hii ni mechi ya kihistoria, kwani ni fainali ya kwanza kati ya timu mbili za Ulaya katika toleo hili lililopanuliwa la michuano hii.

Nitakuwa hapa kuwapa updates za hii game.

Najua kuna uzi generally kwa mechi hizi ila kwa upekee wa fainali tuwe na uzi separate.

VIKOSI VYA LEO.
1. CHELSEA
20250713_210150.jpg


2. PARIS SAINT-GERMAIN
20250713_210135.jpg


22'
Chelsea wanapata goli safi sana kupitia kwa Cole Palmer.
1-0

30'
Cole Palmer goli la 2.
2-0
1752435206853.gif

42'
Pedro anaipatia Chelsea Goli 3.
3-0
downloadfile.gif

IMG-20250714-WA0000.jpg
 
Historia ya Mchuano

Chelsea wana nafasi ya kufanya historia kwa kuwa timu ya kwanza ya Kiingereza kushinda Kombe la Dunia la Vilabu mara mbili, baada ya ushindi wao wa 2021 dhidi ya Palmeiras.

Kwa upande mwingine, PSG wako kwenye michuano yao ya kwanza na wana hamu ya kuongeza kombe la dunia kwenye kabati lao baada ya kushinda UEFA Champions League msimu huu.

Mechi za awali kati ya timu hizi mbili zimekuwa za ushindani mkubwa, na kila timu ikishinda mara mbili katika mechi nane zilizopita, huku tatu zikiwa sare.
 
Ngoja tuone, Chelsea wakikaa vibaya kiungo chake chote kitamezwa, watapitia pembeni kuabsorb zile loopholes lakini si rahisi kihivyo maana hata Neto pia atakuwa na kazi ya kukaba na upande huo wa Neto ndo PSG wata overload huko, mmoja lazima atoe kilio cha mbwa Leo.
 
Mwenendo wa Timu

Paris Saint-Germain:

Wameonyesha nguvu za ajabu katika michuano hii, wakisonga mbele bila kushindwa katika raundi za mtoano, wakiwafunga
Inter Miami (4-0),
Bayern Munich (2-0),
Real Madrid (4-0)

Kwa ustadi wa hali ya juu. Wachezaji kama Ousmane Dembélé, Khvicha Kvaratskhelia, na Désiré Doué wamechangia mabao 16, huku Gianluigi Donnarumma akiwa imara langoni, akiruhusu bao moja tu katika mechi sita. PSG wana safu ya ushambuliaji inayoweza kushambulia kutoka kila pembe, pamoja na kiungo imara cha Joao Neves, Vitinha, na Fabian Ruiz. Hata hivyo, wanakosa walinzi Willian Pacho na Lucas Hernandez kutokana na kusimamishwa.(Red Card)
 
Mwenendo wa Timu

Chelsea:

Wameimarika kadri michuano inavyosonga, wakiwafunga
Benfica (4-1)
Palmeiras (2-1)
Fluminense (2-0)
Katika raundi za mtoano. João Pedro, ambaye ni mchezaji mpya, amekuwa nyota, akifunga mabao mawili dhidi ya Fluminense. Kocha Enzo Maresca ameweka mkazo kwenye kumudu mpira kwa ustadi, na Chelsea wamefunga mabao 14, sita yakiwa ya koni za haraka. Hata hivyo, wanakabiliwa na changamoto ya jeraha la Moises Caicedo, ingawa anaweza kuwa fit kwa mechi ya leo.
 
Chelsea wakiwa na game approach nzuri kama walivyofanya Bayern(japo baadae walitoka kwenye mkakati wao) wanaweza wakatoa ushindani wa hali ya juu sana pengine hata kushinda.
Kama Caicedo hatakuwepo Chelsea wajiandae kwa milio ya kutosha.

Binafsi nina shauku ya kuona Chelsea watakuja na mbinu gani dhidi ya hii PSG ambayo ipo kwenye fomu vibaya mno
 
Back
Top Bottom