Ukimbie uende wapi huku mechi ikipangwa tarehe fulani inapigwa tarehe hiyo hiyo, Barca alikuwa na mechi kumi mfululizo anapumzika siku mbili mechi mbili mechi, akaomba baadhi ya mechi zisogezwe mbele La Liga wakakataa. Madrid mechi ya Marudiano na Arsenal baada ya kupigwa mechi ya kwanza akaomba, mechi yake ya ligi ambayo iliyo pangwa na Laliga ichezwe Jumapili ,akaomba ichezwe jumamosi Laliga wakakataa na Madrid akacheza siku ile ile ya Jumapili iliyo pangwa. Mechi ya Jana Madrid walikuwa wanalamikia marefa wabadilishwe Laliga wakakomaa kwamba marefa hawa hawa tulio wapanga ndio watachezesha hiyo mechi.
Kwa kifupi vyama vya wenzetu ulaya vina nguvu halafu cha pili kule kuhairisha mechi kwa sababu za kipuuzi ni hasara,kwani wanao simamia production wanaweza wakadai fidia kubwa sana, sababu set up ya mechi moja gharama yake ni kubwa.Hiyo May 11 hamna kukimbia.