From the desk of the Chairman Baba v.

From the desk of the Chairman Baba v.

Baba V

JF-Expert Member
Joined
Dec 29, 2010
Posts
19,479
Reaction score
9,548
Ni matumaini yangu kuwa mu wazima wapendwa wanajamvi wenzangu, Kwa upande wangu niko poa japo ninasumbuliwa na ukurutu kidogo nilioambukizwa huko lupango ambako kwa sasa nimepewa hadi chumba maalumu kwenye server namba 3.

Nina mambo machache ambayo ningependa kuyaongea nanyi hapa.

Mosi ni kuwatangazia uteuzi wa watu8 kuwa makamu wa mwenyekiti wa Tume ya mahusiano na ndoa hapa chit chat.Nafasi hii watashirikiana na gfsonwin ambae pia ni mwenyekiti wa umoja wa wanawake na mabinti hapa chit chat. Uteuzi huu umefuatia kukosekana kwa mara kwa mara kwangu mie mwenyekiti kutokana na ban ndogondogo na kubwakubwa ambazo zimekuwa zikiniandama siku za hivi karibuni.Nimewateua hawa kwa kuzingatia busara zao na uwepo wao hapa jamvini na uzoefu wao pia. Nawaombeni wanajamvi muwape ushirikiano na ushikiriano pindi ukìitajika.

Pili, napenda kuongelea habari ya mwenzetu Ruhazwe JR ambaye hatukuwa nae kwa muda mrefu baada ya yeye kupata matatizo na kimya kikatanda kwa muda mrefu hadi ikaleta wasiwasi kwa madau hadi pale alipojitokeza mwenyewe. Napenda kuliongelea hili kwa sababu limeleta mitazamo tofauti baina ya wadau wa hapa jamvini. Kimsingi ifahamike kuwa chìt chat kwa ukaribu wetu tumekuwa kama familia moja, tatizo la mwenzetu mmoja linatugusa sote, na ndio maana huwa tunapenda kupata taarifa ili kuwa updated,kuna baadhi yetu hapa walilaumu eti kwa nini wanachit chat walimlaumu Ruhazwe JR kwa kutotoa taarifa, Mie naamini alieanzisha uzi ule alikuwa na nia njema kabisa kwani baada ya ule uzi na maoni ya wadau tumepata tumaini jipya. Tuendelee kumuombea mwenzetu ili arudi tujumuike nae hapa kama mwanzo.

Pia ningependa kuwataarifu kuwa hivi karibuni nitatangaza couple ya mfano wa kuigwa ya mwaka 2012/13. Kigezo kikubwa ni namna ilivyoweza kudumu bila mifarakano na kutengana kwa muda mrefu. Hii itakwenda sambamba na kumtangaza mwanamke na mwanaume mmoj mmoja ambao wameongoza kwa kubadilisha wenza wao.

Mwisho ingawa sio kwa umuhimu napenda tu niwaambieni wana chit chat kuwa hizi ban zilizoniandama zisiwafadhaishe kwani nimeamua kuzikubali kwa ustawi wa nchi yetu. Kule siasani kuna watu huwa inahitaji wakati flani kutumia maneno yatakayofikisha ujumbe ipasavyo hata kama yatawaumiza na ndio maana wakati flani yanakinzana na busara za mods ambao nao wananipa hifadhi kunako server za Jf . Tutaendelea kuwa pamoja wapendwa.

Wenu
Baba V
Mwenyekiti wa tume ya kudumu ya mahusiano na ndoa chit chat 2013

C.c watu8, gfsonwin, Madame B, Erickb52, Ruttashobolwa, Judgement , Filipo Arushaone Chimbuvu Arabela Slave, Dr.zero, Mpenda Yesu, Ben Saanane, Vin Diesel charminglady Slave, snowhite (Pole kwa msiba), lady furahia Passion Lady Donn, jeneneke, TANMO, ummu kulthum Ndelejha, Kaizer, Kipipi , BADILI TABIA , Kijino Mr Rocky, Nicas Mtei, Dena Amsi, Asprin, The secretary, FP , cacico, Jeska, King'asti (mwambie mumeo apunguze ban kwangu asidhani sifa), Kongosho, Mamndenyi, Sefet , Mwanyasi, IGWE, Mamzalendo , nitonye, PakaJimmy, marejesho, sweetlady amu, mimisa Tonykp sharifaa , noahism, pombekali Supu ya Jiwe Invisible na wengineo woote.....:yo::A S-heart-2::A S-heart-2:
 
Last edited by a moderator:
Hivi huko seva za JF kukoje mkuluuu....???nina wasiwasi ushapewa unyapala huko

makamu asikwambie mtu, kule hata uwe baunsa vipi unabaki mtoto, basi tu ni huu ujanja wa mjini unatusaidia:A S shade:
 
kwa hiyo nikatafute chuo wanachosomea hiyo nikajiunge?
short course inatosha au mpaka nisome degree?

eeeeerr mnh eeeh kwa apiarens unaonekana huitaji kuisomea, wewe utafaa hivyohivyo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom