From Jambo to Jamii Forum... Ni kweli?

Mtego wa Noti

JF-Expert Member
Nov 27, 2010
2,591
1,599
Habari wanaJF, nimeambiwa kuwa zamani Forum hii ilikuwa inaitwa Jambo forum na ikafungwa na serikali na ikabadilishwa kuwa Jamii forum ambayo mpaka sasa tunatoa mawazo yetu tukiwa huru. Hii ni kweli jamani? naomba mawazo yenu mnipe historia ya JF. Nawasilisha!!
 
Umetumwa ili muifungie na hii? Mshindwa kwa jina la Jamii forums!
 
Umetumwa ili muifungie na hii? Mshindwa kwa jina la Jamii forums!

Hapana kaka sijatumwa, nimeona niulizie historia tu ili niifahamu. sina mpango wa kuchochea ifungwe.. Ingekuwa ni suala la kufungwa, basi Wikileaks ingefungwa haraka sana.... maana imekuwa mwiba kwa wakuu wa dunia.
Lengo langu ni kujua background tu ya hii formu na si vinginevyo...
 
Ni kweli ilikuwa inaitwa jamboforums, kulikuwa na dispute kuhusu domain name mpaka ikabadilishwa as far as I know, sasa hii habari ya serikali kuwa chanzo ni mpya kwangu. Labda wenye kuendesha mambo watuarifu rasmi.
 
Ni kweli ilikuwa inaitwa jamboforums, kulikuwa na dispute kuhusu domain name mpaka ikabadilishwa as far as I know, sasa hii habari ya serikali kuwa chanzo ni mpya kwangu. Labda wenye kuendesha mambo watuarifu rasmi.

Asante Kiranga kwa huo ufafanuzi. angalau napata mwanga kiasi kuhusu JF.. nadhani na wegine wataweka mawazo yao ili tujue uwazi zaidi ya huu
 
as far as i am concerned, kufukua maiti hakumrudishii uhai marehemu
 
Una maana gani aise!! kwani kuna ubaya kufahamu background ya kitu? si ndiyo maana ya historia?
niko very clear mkuu, unless unasoma post nyingine.......... BTW, did you hvae to be enrolled to search for history?
 
Ugaidi? magidi? hili nalo ni jipya, unaweza kutuelezea ilikuwaje ikahusishwa na mambo ya ugaidi? Ila sishangai, hapa Africa mtu ukiwa na mawazo ya ukombozi utapata majina mengi...mara haini na mengine kama gaidi... please more infos. ninahofu sana na hilo swala la ugaidi..
 

Max na invisible wanaweza kukupa ukweli kamili.

Ni kweli, ilikuwa inaitwa Jambo Forums, ikiwa kama sehemu ya jambo networks. Kulingana na kumbukumbu zangu, matatizo halisi ya Jambo Forums yalianzia kwenye bomu lililolipuliwa hapa kuhusu mafisadi mbalimbali wakiwemo wa EPA na Richmond ambayo yalipelekea Lowasa kufukuzwa kazi au kujiuzulu uwaziri mkuu. Max na Mushi walishikwa na kuwekwa ndani kutokana na tukio hilo, halafu kwa vile Jamboforums ilikuwa imeandikiswa kwa kutumia credit card ya Mushi mkubwa (siyo Mike Mushi) ambaye nadhani alikuwa na maslahi fulani kwa Lowasa, basi akaamua kuvuruga Jambo Forums kipindi hicho hicho, kwanza kwa kuwa anafuta mafaili ya post zote, lakini Mods walikuwa wanaweza kuyarecover tena kwa kutumia njia ambalimbali. Baada ya kuona ameshindwa kuizuia Jambo Forums kwa njia hiyo ya kufuta mafaili, Mushi akaamua kuzuia malipo ya server na hivyo baadaye kuifungia Jambo Forums kabisa.

Baada ya jamboforums kufungwa, viongozi mbalimbali wa Jamii Forums kwa pamoja walichukua hatua madhubuti ya kuanzisha domain nyingine kwa jina la Jamii Forums ikiwa kwenye server tofauti na ilikokuwa Jamboforums; wakahamisha mafaili yote yaliyokuwa jamboforums na baada ya wiki moja hivi forum ikawa imesimama tena. Mushi mkubwa alifungua kesi dhidi ya Jamii Forums lakini alishindwa katika kesi ile, na leo Jamii forums imeendelea kukua na kubadilika sura kuwa ya kisasa zaidi kama uionavyo.
 
 

This is great. nimefurahi sana kwa huo ufafanuzi. Kumbe Lissu kaanza harakati long time sana. Sasa tunajiandaaje kama ikitokea mafisadi wakiingilia huu mtandao na kutaka kuufunga? si mnakumbuka jinsi walivyofanya mpakq magazet yaliyokuwa moto kwao kama MwanaHalisi mpaka yakafungwa?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…