From Jambo to Jamii Forum... Ni kweli?

Mtego wa Noti

JF-Expert Member
Nov 27, 2010
2,590
1,614
Habari wanaJF, nimeambiwa kuwa zamani Forum hii ilikuwa inaitwa Jambo forum na ikafungwa na serikali na ikabadilishwa kuwa Jamii forum ambayo mpaka sasa tunatoa mawazo yetu tukiwa huru. Hii ni kweli jamani? naomba mawazo yenu mnipe historia ya JF. Nawasilisha!!
 
Umetumwa ili muifungie na hii? Mshindwa kwa jina la Jamii forums!
 
Umetumwa ili muifungie na hii? Mshindwa kwa jina la Jamii forums!

Hapana kaka sijatumwa, nimeona niulizie historia tu ili niifahamu. sina mpango wa kuchochea ifungwe.. Ingekuwa ni suala la kufungwa, basi Wikileaks ingefungwa haraka sana.... maana imekuwa mwiba kwa wakuu wa dunia.
Lengo langu ni kujua background tu ya hii formu na si vinginevyo...
 
Ni kweli ilikuwa inaitwa jamboforums, kulikuwa na dispute kuhusu domain name mpaka ikabadilishwa as far as I know, sasa hii habari ya serikali kuwa chanzo ni mpya kwangu. Labda wenye kuendesha mambo watuarifu rasmi.
 
Asante Kiranga kwa huo ufafanuzi. angalau napata mwanga kiasi kuhusu JF.. nadhani na wegine wataweka mawazo yao ili tujue uwazi zaidi ya huu
 
as far as i am concerned, kufukua maiti hakumrudishii uhai marehemu
 
Una maana gani aise!! kwani kuna ubaya kufahamu background ya kitu? si ndiyo maana ya historia?
niko very clear mkuu, unless unasoma post nyingine.......... BTW, did you hvae to be enrolled to search for history?
 
Ugaidi? magidi? hili nalo ni jipya, unaweza kutuelezea ilikuwaje ikahusishwa na mambo ya ugaidi? Ila sishangai, hapa Africa mtu ukiwa na mawazo ya ukombozi utapata majina mengi...mara haini na mengine kama gaidi... please more infos. ninahofu sana na hilo swala la ugaidi..
 
Habari wanaJF, nimeambiwa kuwa zamani Forum hii ilikuwa inaitwa Jambo forum na ikafungwa na serikali na ikabadilishwa kuwa Jamii forum ambayo mpaka sasa tunatoa mawazo yetu tukiwa huru. Hii ni kweli jamani? naomba mawazo yenu mnipe historia ya JF. Nawasilisha!!

Max na invisible wanaweza kukupa ukweli kamili.

Ni kweli, ilikuwa inaitwa Jambo Forums, ikiwa kama sehemu ya jambo networks. Kulingana na kumbukumbu zangu, matatizo halisi ya Jambo Forums yalianzia kwenye bomu lililolipuliwa hapa kuhusu mafisadi mbalimbali wakiwemo wa EPA na Richmond ambayo yalipelekea Lowasa kufukuzwa kazi au kujiuzulu uwaziri mkuu. Max na Mushi walishikwa na kuwekwa ndani kutokana na tukio hilo, halafu kwa vile Jamboforums ilikuwa imeandikiswa kwa kutumia credit card ya Mushi mkubwa (siyo Mike Mushi) ambaye nadhani alikuwa na maslahi fulani kwa Lowasa, basi akaamua kuvuruga Jambo Forums kipindi hicho hicho, kwanza kwa kuwa anafuta mafaili ya post zote, lakini Mods walikuwa wanaweza kuyarecover tena kwa kutumia njia ambalimbali. Baada ya kuona ameshindwa kuizuia Jambo Forums kwa njia hiyo ya kufuta mafaili, Mushi akaamua kuzuia malipo ya server na hivyo baadaye kuifungia Jambo Forums kabisa.

Tanzania detains popular Web site editors

New York, February 29, 2008 – CPJ condemns the arbitrary arrest of two popular online editors without charge. The two were detained and interrogated for 24 hours in Dar es Salaam, Tanzania, on February 18, in what observers of the case say was a politically motivated attempt to shutter the site.
The two young editors, Maxence Mello and Mike Mushi, aged 21 and 18 respectively, host the extremely popular Jambo Forums, a public discussion site with more than 2,000 members and 6 million hits in February alone. Topics on the site cover everything from politics to culture to entertainment. Police confiscated three computers used to host their Web site, shutting down the site for five days while the equipment remained under police custody, Mello told CPJ.
According to Mello's defense lawyer, Tundu Lissu, the police had no official charges against the editors and said the orders to arrest them had come from the president's office. The Inspector General of Police, Said Mwema, stated in a press conference on February 20 in Dar es Salaam that they were arrested because they were suspected of criminal activity – which may include the "dissemination of wrong information" through the Jambo Forums Web site.
"The Tanzanian government must refrain from arresting journalists in an attempt to silence public dialogue," said CPJ's Executive Director Joel Simon. "Such arbitrary arrests set a dangerous precedent for the free dissemination of information online."
Maxence Mello told CPJ that police arrested him at his college, the Dar es Salaam Institute of Technology, at 4 p.m. and then took him to his house where they lured then arrested his colleague, Mike Mushi. They were interrogated throughout the night over several postings on the site that criticized the government, and released at 5 p.m. the following day.
Local journalists said the forum had played a major role in exposing a suspect energy contract the former Prime Minister Edward Lowassa made with an American energy firm. The contract was published in full on the Jambo Forums site, Mello said. The former minister resigned on February 7 after a parliamentary probe into the incident. Four other suspected fraudulent contracts between the government and foreign companies are also currently posted on the Web site, Mello told CPJ.
Lissu said the two moderators were questioned specifically on this matter, and he as well as local journalists say they suspect the detention was directly tied to the posting of the contested energy contract. This kind of interrogation of journalists is part of a pattern of ongoing harassment of the local media, Lissu added.
Baada ya jamboforums kufungwa, viongozi mbalimbali wa Jamii Forums kwa pamoja walichukua hatua madhubuti ya kuanzisha domain nyingine kwa jina la Jamii Forums ikiwa kwenye server tofauti na ilikokuwa Jamboforums; wakahamisha mafaili yote yaliyokuwa jamboforums na baada ya wiki moja hivi forum ikawa imesimama tena. Mushi mkubwa alifungua kesi dhidi ya Jamii Forums lakini alishindwa katika kesi ile, na leo Jamii forums imeendelea kukua na kubadilika sura kuwa ya kisasa zaidi kama uionavyo.
 
Max na invisible wanaweza kukupa ukweli kamili. Ni kweli, ilikuwa inaitwa Jambo Forums, ikiwa kama sehemu ya jambo networks. Kulingana na kumbukumbu zangu, matatizo halisi ya Jambo Forums yalianzia kwenye bomu lililolipuliwa hapa kuhusu mafisadi mbalimbali wakiwemo wa EPA na Richmond ambayo yalipelekea Lowasa kufukuzwa kazi au kujiuzulu uwaziri mkuu. Max na Mushi walishikwa na kuwekwa ndani kutokana na tukio hilo, halafu kwa vile Jamboforums ilikuwa imeandikiswa kwa kutumia credit card ya Mushi mkubwa (siyo Mike Mushi) ambaye nadhani alikuwa na maslahi fulani kwa Lowasa, basi akaamua kuvuruga Jambo Forums kipindi hicho hicho, kwanza kwa kuwa anafuta mafaili ya post zote, lakini Mods walikuwa wanaweza kuyarecover tena kwa kutumia nji ambalimbali. Baada ya kuona ameshindwa kuizuia Jambo Forums kwa njia hiyo ua kufuta mafaili, Mushi akaamua kuzibia malipo ya server na hivyo baadaye kuifungia Jambo Forums kabisa. Baada ya jamboforums kufungwa, viongozi mbalimbali wa Jamii Forums kwa pamoja
 
Max na invisible wanaweza kukupa ukweli kamili.

Ni kweli, ilikuwa inaitwa Jambo Forums, ikiwa kama sehemu ya jambo networks. Kulingana na kumbukumbu zangu, matatizo halisi ya Jambo Forums yalianzia kwenye bomu lililolipuliwa hapa kuhusu mafisadi mbalimbali wakiwemo wa EPA na Richmond ambayo yalipelekea Lowasa kufukuzwa kazi au kujiuzulu uwaziri mkuu. Max na Mushi walishikwa na kuwekwa ndani kutokana na tukio hilo, halafu kwa vile Jamboforums ilikuwa imeandikiswa kwa kutumia credit card ya Mushi mkubwa (siyo Mike Mushi) ambaye nadhani alikuwa na maslahi fulani kwa Lowasa, basi akaamua kuvuruga Jambo Forums kipindi hicho hicho, kwanza kwa kuwa anafuta mafaili ya post zote, lakini Mods walikuwa wanaweza kuyarecover tena kwa kutumia njia ambalimbali. Baada ya kuona ameshindwa kuizuia Jambo Forums kwa njia hiyo ya kufuta mafaili, Mushi akaamua kuzuia malipo ya server na hivyo baadaye kuifungia Jambo Forums kabisa.

Baada ya jamboforums kufungwa, viongozi mbalimbali wa Jamii Forums kwa pamoja walichukua hatua madhubuti ya kuanzisha domain nyingine kwa jina la Jamii Forums ikiwa kwenye server tofauti na ilikokuwa Jamboforums; wakahamisha mafaili yote yaliyokuwa jamboforums na baada ya wiki moja hivi forum ikawa imesimama tena. Mushi mkubwa alifungua kesi dhidi ya Jamii Forums lakini alishindwa katika kesi ile, na leo Jamii forums imeendelea kukua na kubadilika sura kuwa ya kisasa zaidi kama uionavyo.

This is great. nimefurahi sana kwa huo ufafanuzi. Kumbe Lissu kaanza harakati long time sana. Sasa tunajiandaaje kama ikitokea mafisadi wakiingilia huu mtandao na kutaka kuufunga? si mnakumbuka jinsi walivyofanya mpakq magazet yaliyokuwa moto kwao kama MwanaHalisi mpaka yakafungwa?
 
Back
Top Bottom