friji ya kiafrika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

friji ya kiafrika

Discussion in 'Jamii Photos' started by UncleUber, Aug 3, 2012.

 1. UncleUber

  UncleUber JF-Expert Member

  #1
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 4,945
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  ubunifu asilia, au vipi wanajamvi
   
 2. yaser

  yaser JF-Expert Member

  #2
  Aug 3, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 1,373
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  hakuna kitu hapo
   
 3. LexAid

  LexAid JF-Expert Member

  #3
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 1,950
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Sijaielewa mkuu inavyofanya kazi....

  Meng'enyua mkuu.
   
 4. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #4
  Aug 3, 2012
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,088
  Trophy Points: 280
  Kuna moja niliiona jamaa wameweka bia kwenye gunia lililowekwa mchanga halafu wakalimwagia maji! Aisee bia zinapoa vizuri sana! wakuu na wala msibishe jaribuni hiyo fomular halafu mniambie.
   
 5. m

  markj JF-Expert Member

  #5
  Aug 3, 2012
  Joined: Jul 6, 2012
  Messages: 1,756
  Likes Received: 364
  Trophy Points: 180
  na bado! tutaweka mpaka kwenye mabati ya nyumba usiku
   
 6. ndetichia

  ndetichia JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2012
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 27,641
  Likes Received: 236
  Trophy Points: 160
  inachukua muda gani kupoza hivo vinywaji..
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Aug 3, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,610
  Likes Received: 82,187
  Trophy Points: 280
  Mie nayapenda sana maji ya mtungini. Ni matamu kupita kiasi!!! Unachemsha maji yako unasubiri yapoe kisha kuyaweka mtungini. Naweza kunywa maji hata glass tano kwa wakati mmoja.
   
 8. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #8
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Humo ndani ya mtungi kulitakiwa kuwe na Togwa bana na sio hayo masoda.
   
 9. UncleUber

  UncleUber JF-Expert Member

  #9
  Aug 3, 2012
  Joined: Apr 25, 2011
  Messages: 4,945
  Likes Received: 99
  Trophy Points: 145
  mtungi hujulikana kwa uwezo wake wa kupoza maji na yakawa ya ubaridi wa wastani, sasa hawa jamaa wakaamua kutumia theory hiyo kwenye soda kwa kuziweka kwenye maji zinapoa
   
 10. princess enny

  princess enny JF-Expert Member

  #10
  Aug 4, 2012
  Joined: May 27, 2012
  Messages: 1,042
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  teh!!! hcho sasa kikokotezi
   
 11. Boflo

  Boflo JF-Expert Member

  #11
  Aug 4, 2012
  Joined: Jan 20, 2010
  Messages: 4,394
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  coooooooooooooooooooool
   
 12. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #12
  Aug 5, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  rafiki, mimi nikiendaga kijijini, hata kama sina kiu huwa naomba maji, harufu yake tu inanivutia kuyanywa................ hasa ukute maji yamechotwa kisimani halafu yakatiwa mtungini.................. na huwa hayachemshwi yale lakini hakuna cha typhoid wala nini
   
 13. Asulo

  Asulo JF-Expert Member

  #13
  Aug 5, 2012
  Joined: Jun 25, 2012
  Messages: 733
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Maji ya kwenye hii kitu ni nooouma..
  Unaweza ukanywa hata lita kwa mkupuo.
   
 14. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #14
  Aug 5, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,610
  Likes Received: 82,187
  Trophy Points: 280
  Ahsante sana FP kwa mchango wako, mie kusema kweli ni muoga sana kunywa maji ambayo hayajachemshwa. Hata nikienda nyumbani kwa mtu kama tumezoeana sana nikihitaji maji basi lazima niulize mnachemsha maji yenu ya kunywa? lakini kama hakuna mazoea ya karibu basi ni heri tu ninywe hata kinywaji baridi chochote kile lakini si maji. Nimewahi kuona watu waliopata kipindupindu jinsi walivyorudisha namba haraka sana basi nikasema kamwe mdomoni mwangu hayataingia maji ambayo hayajachemshwa. Hilo la maji ya mtungini kuwa na harufu nzuri sana ni kweli, ila nililisahau. :)


   
 15. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #15
  Aug 5, 2012
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  mimi huwa nayafanya hayo nikiwa mjini, sinywi maji kwa watu kama sina uhakika kama wanachemsha au la. kwa kijijini huwa naangalia mazingira. kabla sijaomba maji huwa naomba kwenda toilet hata kama sijabanwa. mara nyingi sana hali ya toilet huwa inakutambulisha hygiene ya mahali hapo
   
 16. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #16
  Aug 5, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  huu mtungi unafanana na ule wa pale mburahati kwa mama muuza gongo
   
 17. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #17
  Aug 5, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,841
  Trophy Points: 280
  BAK umenikumbusha mbali sana, maji yake huwa hayanuki clorine bana yanakauwa na harufu ya udongo wa mtungi lol halafu ni ya baridi ile mbaya. sasa hivi tunataka kuziadvance hizi tuziekee membrane filters zenye micropores 4mm yaani ili zitumike kuchuj maji kwa watu wa vijijini ishu imekuwa ngumu kwenye utunzaji yaani ikivunjika ndo basi tena. pia ikisha clog hiyo filter mtumiaji ataaboreka nayo so ataaidiscard despite gharama ambazo serikali imeinvest kwenye hiyo filter.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Z

  ZeMarcopolo JF-Expert Member

  #18
  Aug 5, 2012
  Joined: May 11, 2008
  Messages: 13,589
  Likes Received: 480
  Trophy Points: 180
  Haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa ila kuiita ya kiafrika naona kama unawaua waafrika. Hiyo ni ya mtu masikini tu, hakuna uafrika hapo!
   
 19. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #19
  Aug 5, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,610
  Likes Received: 82,187
  Trophy Points: 280
  lol! FP vyoo vingine hasa hivi vya kizungu unaweza kujutaaa kwa nini uliamua kuomba kwenda chooni hasa kunapokuwa na shida ya maji. Na kama uijuavyo nchi yetu shida ya maji ni ya miaka nenda miaka rudi na hakuna hata dalili za ahueni.
   
 20. gfsonwin

  gfsonwin JF-Expert Member

  #20
  Aug 5, 2012
  Joined: Apr 12, 2012
  Messages: 16,963
  Likes Received: 1,841
  Trophy Points: 280
  @fixeed point aisee hii theory yako siyo kabisa. unless kama umefanya tafiti nyingi katika vijiji vya huko tanganyika. mara nyingi sana kuna watu hasa baadhi ya waislam kwao maliwato ni priority sana ila kwingine siyo. kuna siku tulikwena singida vijijini yaani unamkuta mtu uwanja msafi na choo kizuri kweli ila mtu huyu maji anayokunywa ni machafu sana anachemsha kisha kikombe cha kunywea ndicho kinacho chota majia ndani ya water can. sasa unakuta mwingine katoka toilet anashika kata tena yenye mkono mfupi so lazima mkono utadumbukia, ananywea kikombe hicho hicho. na kaukairudisha hapo.

  kuna mwingine aliposikia kuna watafiti kwenye kata aliweka water guard so tulipopima free chlorine tukaikuta tukajua huyu anajali sana kumbe yale maji ndio anayofulia nguo kia water guard ina hypochlorite ambayo ni bleaching agent ya kunywa ni machafu kabisa yaani ukiyaangalia ni meupe ila kiafya ni full of coliforms tulipoyapanda total coliform walikuwa juu sana. so sikushauri kabisa kwa hili.
   
Loading...