Freemasonry Wametushika kila kona

Freemasonry Wametushika kila kona

NAMTUMBA

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2014
Posts
1,939
Reaction score
600
Tafadhali kama una msimamo mkali wa dini ishia hapa usiendelee kusoma.

Nilikuwa kijiweni muda mfupi uliopita nacheza mchezo wa Draft. Kaja jamaa mmoja baada ya salamu jamaa mungine akauliza muda ili awahi kuondoka, akajibiwa kwamba ni saa moja na robo.
Sasa shida ikaanza kwa yule mgeni wetu, akatuuliza munawajua Freemasons? Nikajibu nawasikia kwamba ni mtandao wa matajiri wakubwa duniani. Jamaa akanicheka akasema umepotea kaka, hao ni waabudu shetani na wametushika kila kona. Nikambishia nikasema si kweli. Ndipo akaja na somo la saa au mfumo wa kusoma saa.

Akaanza kwa kuuliza sasa ni saa ngapi? nikamjibu saa moja. Akaniuliza hapo kwenye saa yako imeandikwa ngapi? Nikamjibu saba. Akasema emheeee hapahapo ndipo wametushika. Akauliza munajua kwa nini saa moja iandikwe saba? Nikajibu sijui. Akauliza munajua 666 alama ya mpinga kristo? Nikamjibu nasikiaga. Ndo sasa akaanza hesabu zake kama ifuatavyo.

1. Saa moja inaandikwa saba: 7-1= 6
2. Saa mbili inaandikwa nane: 8-2= 6
3. Saa tatu „ Tisa: 9-3= 6
4. Saa nne „ kumi: 10-4=6
5. Saa tano „ 11: 11-5 =6
6. Saa sita „ 12: 12-6= 6
7. Saa saba „ 13: 13-7=6
8. Saa nane „ 14: 14-8=6
9. Saa tisa „ 15: 15-9= 6
10. Saa kumi „ 16: 16-10=6
11. Saa kumi na moja „ 17: 17-11=6
12. Saa kumi na mbili „ 18: 18-12=6
Hapo akauliza mumenisoma? Wote tukajibu ndio mzeee.
Akasema kwa masaa 12 mengine Freemason wamefanya kama ifuatavyo.
1. Saa moja inaandikwa 19: 19-1=18=6+6+6
2. Saa mbili „ 20: 20-2=18=6+6+6
3. Saa tatu „ 21: 21-3=18=6+6+6
4. Saa nne „ 22: 22-4= 18=6+6+6
5. Saa tano. „ 23: 23-5= 18=6+6+6
6. Saa sita „ 24: 24-6= 18= 6+6+6
Hivyo kuanzia saa saba usiku inarudia tena kama hapo juu kabisa kuanzia namba 1-6. Hivyo tukabaki kimyaaa. Akasema ndo maana yeye hatumii mfumo wa 24hrs anatumia 12hrs system.

Sasa niwaulize wanajamvi kuna ukweli wowote hapa? Je nikweli Freemasons walivuruga saa makusudi? Je kuna ubaya kutumia 24hrs system?.
 
Embu kamuulize tena ni kwanini hao Freemason wameamuamua kutumia no 6 (666)...
Naomba jibu..
 
Ni upumba.vu wa hali ya juu...Hapa Tanzania na East Africa tunatumia mifumo miwili ya majira...Ule wa kiingereza na kiswahili....Saa na majira yake yapo kwa Kingereza na Tunasoma kwa kiswahili...

Hawa Freemason nafikiri watakuwa wanajuta kufahamika Tanzania.....

Anyway fanya uchunguzi wako uangalie ni watu wa imani/dhehebu gani hupendelea sana kijadili haya mambo....Ukimaliza hapo angalia hali zao za kimaisha...?? Kuna kitu utajifunza kikubwa...

Kwa mtu aliyefika darasa la saba na kusoma majira ya saa kwa akili ya kawaida hawezi fikiria upuuzi wa namna hii...

Kuna watu wametuloga Watanzania..
 
Kuna mtu aliwahi kuniambia namba 333 pia ni freemansons. Sasa mwandishi naomba nisaidie hiyo naipataje kwenye mambo ya wkt km somo lako linavyoeleza
 
Ni ujinga kujaribu kuaminisha watu mambo yasiyo thibitika.
 
Unapoingia Net Unaanza Na WWW HIYO NI 666
Kilakitu Unachotumia Ni Cha Kwao Kuanzia
Chakula
Mitandao Ya Simu
International Networking Ya Intarnet
Vipodozi Vyote Unavyovifahamu
Muvi Zote Za Hollwood
Mabenk Yote Ya Kwao
KWA HIYO HUWEZI KUWAKWEPA POPOTE ULIPO WAPO

Masikini ya Mungu sijui nani katuloga....Dahhh....Wanasayansi na wenzetu wanakaa kucha kutwa wakiumiza vichwa kitumia akili Mungu alizowapa kivimbua vitu mbalimbali...

Kumbe kuna ma mbumbumbu yapo Tanzania yamedumaza akili zao na kufikiri kila kitu ni Freemason...

Hivi mtu kama wewe wanao watakuja kuwaje...Tutakuwa watumwa wa Mataifa ya nje mpka lini...leo mpaka toothpick zinatoka China...

Hivi tunaweza kuja tengeneza hata simu ya hapa Tz na watoto wetu...

Nani katulogaaaaaa!!!!
 
Unapoingia Net Unaanza Na WWW HIYO NI 666 Kilakitu Unachotumia Ni Cha Kwao KuanziaChakulaMitandao Ya SimuInternational Networking Ya IntarnetVipodozi Vyote UnavyovifahamuMuvi Zote Za HollwoodMabenk Yote Ya KwaoKWA HIYO HUWEZI KUWAKWEPA POPOTE ULIPO WAPO
hiyo ndiyo Roman Empire hutaki unaacha
 
Kuna mtu aliwahi kuniambia namba 333 pia ni freemansons. Sasa mwandishi naomba nisaidie hiyo naipataje kwenye mambo ya wkt km somo lako linavyoeleza

333 ni nusu ya 666.
 
Back
Top Bottom