luisajr
JF-Expert Member
- May 31, 2014
- 270
- 85
Tafadhali kama una msimamo mkali wa dini ishia hapa usiendelee kusoma.
Nilikuwa kijiweni muda mfupi uliopita nacheza mchezo wa Draft. Kaja jamaa mmoja baada ya salamu jamaa mungine akauliza muda ili awahi kuondoka, akajibiwa kwamba ni saa moja na robo.
Sasa shida ikaanza kwa yule mgeni wetu, akatuuliza munawajua Freemasons? Nikajibu nawasikia kwamba ni mtandao wa matajiri wakubwa duniani. Jamaa akanicheka akasema umepotea kaka, hao ni waabudu shetani na wametushika kila kona. Nikambishia nikasema si kweli. Ndipo akaja na somo la saa au mfumo wa kusoma saa.
Akaanza kwa kuuliza sasa ni saa ngapi? nikamjibu saa moja. Akaniuliza hapo kwenye saa yako imeandikwa ngapi? Nikamjibu saba. Akasema emheeee hapahapo ndipo wametushika. Akauliza munajua kwa nini saa moja iandikwe saba? Nikajibu sijui. Akauliza munajua 666 alama ya mpinga kristo? Nikamjibu nasikiaga. Ndo sasa akaanza hesabu zake kama ifuatavyo.
1. Saa moja inaandikwa saba: 7-1= 6
2. Saa mbili inaandikwa nane: 8-2= 6
3. Saa tatu Tisa: 9-3= 6
4. Saa nne kumi: 10-4=6
5. Saa tano 11: 11-5 =6
6. Saa sita 12: 12-6= 6
7. Saa saba 13: 13-7=6
8. Saa nane 14: 14-8=6
9. Saa tisa 15: 15-9= 6
10. Saa kumi 16: 16-10=6
11. Saa kumi na moja 17: 17-11=6
12. Saa kumi na mbili 18: 18-12=6
Hapo akauliza mumenisoma? Wote tukajibu ndio mzeee.
Akasema kwa masaa 12 mengine Freemason wamefanya kama ifuatavyo.
1. Saa moja inaandikwa 19: 19-1=18=6+6+6
2. Saa mbili 20: 20-2=18=6+6+6
3. Saa tatu 21: 21-3=18=6+6+6
4. Saa nne 22: 22-4= 18=6+6+6
5. Saa tano. 23: 23-5= 18=6+6+6
6. Saa sita 24: 24-6= 18= 6+6+6
Hivyo kuanzia saa saba usiku inarudia tena kama hapo juu kabisa kuanzia namba 1-6. Hivyo tukabaki kimyaaa. Akasema ndo maana yeye hatumii mfumo wa 24hrs anatumia 12hrs system.
Sasa niwaulize wanajamvi kuna ukweli wowote hapa? Je nikweli Freemasons walivuruga saa makusudi? Je kuna ubaya kutumia 24hrs system?.
Ni kweli wamevuruga wao ....kuna cku jmaa mmoja alielezea clouds tv
lkn kwa kingereza