Freeman Mbowe, kwanini maridhiano sasa?

Kaka tunazungumzia situation iliyopo Rais aliyepo madarakani hataki kuishi kwa mazoea mwisho, Sasa njia nyingine ni nguvu ya bunge ambayo obviously haipo, ya pili ni Maandamano ambayo sioni hilo likitokea, na la mwisho ni kwenye sanduku la kura (labda hapa)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kula tano kaka

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Na Chama chake kinakuwa wapi? Haiwezekani chama kikakubali kukasimu madaraka yake yote kwa mtu mmoja!
 
Nyie tunawajua sana uvccm, mlitaka uhasama wa cdm na ccm uendelee ili mpate kazi ya kupeleka majungu kwa mwenyekiti wenu na hivyo kujipatia viposho.

Sasa lazima nanyinyi mwende mkalime maana hakuna pa kupeleka majungu yenu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hata kuandika habari za cdm unatetemeka kudadeeeeekiiiii, Njaaaa hiyo sasa huna tena sehemu ya kupeleka hayo majungu yenu.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitaturu,
Mkuu hizo tatu alijipa mwenyewe ila nilisikia Magu kwa masikio yangu akimpa sekunde. Sasa sijui sekunde angeongea nini
 
Watanzania wengi hatuna uwezo wa kuangalia mambo critically .hawa makamanda si wajinga kuna kitu wanakinyatia .si bahati mbaya ati kuwakuta wote wamejipanga kwenye sherehe ni issue walipanga. Ramli moja inasema kuwa wanataka Lissu aridhiwe nami naona kama ramli iko sawa. Janja yao iko jikoni soon tutawagundua
 
Hata kuandika habari za cdm unatetemeka kudadeeeeekiiiii, Njaaaa hiyo sasa huna tena sehemu ya kupeleka hayo majungu yenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Rais aliishasema, anayefikiri atamkwamisha, atakwama yeye. Akina Mbowe na washauri wake wakafikiri anatania. Mara UKUTA, mara Mange Kimambi, mara kususia chaguzi ndogo, mara kususia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Na sasa eti mnaomba maridhiano. Halafu mmeshupaza shingo kweri kweri, maridhiano, maridhiano!
 
Kwanza sitaki kuamini kuwa Mbowe alishiriki katika lile tukio hivi hivi tu bali kushawishiwa na watu wa sytem na wasaidi wengine wa Bwana mkubwa na pia sitaki kuamini kuwa alikwenda kushirikia bila kushirikisha viongozi wenzake ndani ya chama(teyari Lissu katetea kauli ya Mbowe kwa mujibu wa gazeti moja la leo) hivyo kuna uwekano mkubwa Mbowe alitoa kauli ile akijua kinachoendelea ingawa pia inawezekana kaingia katika mtego kwa faida ya Bwana yule asietaka kuonekana kuwa anaweza kushindwa katika misimamo yake(nitaeleza huko mbele).

Kosa alilolifanya Mbowe na chama chake kwa ujumla, ni kushiriki tukio lile bila kushauriana na viongozi wengine wa upinzani ambao naamini wangeshirikishwa,basi aliyoyasema Zitto yasingetokea hata kama wasingefikia muafaka wa pamoja kuwa Mbowe ashiriki.

Nikirudi kwenye mada,nitakuwa wa mwisho kuamini kuwa Bwana yule alikuwa hajui Mbowe ataongea alichoongea bali alitaka tu Mbowe ndio aonekana mtafuta suluhu kwanini yeye siku zote hataki kuonekane ameshindwa(hataki kupangiwa).

Na ndio maana baada tu ya Mbowe kuongea,vijana wa Lumumba wakaanza propaganda za kusema Mbowe kaomba suluhu na maneno mengine mengi ili mwisho wa siku wapinzani ndio waonekane wameshindwa katika mapambano ya kudai haki na sasa wanategemea huruma ya Bwana yule kumbe Bwana yule nae anabanwa na pressure ya ndani na nje ya nchi kutokana na aina ya uongozi wake hasa uminyaji wa demokrasia na unyanyasaji kwa wapinzani.

Naamini katika kujisafisha na ili asiendelee kuvurugana na Bwana wakubwa wa hii dunia,Bwana yule ameona kuna umuhimu wa kujirudi japo kidogo, hivyo anaweza kuja kufanyia kazi wazo la Mbowe ingawa anaweza kufanya hivyo kwa kuwazuga tu mabeberu kwahiyo wawe makini nae.

Ni imani yangu pia, Mbowe kwa upande wake, aliamua kujishusha ili atumie fursa iliojitokeza(akijua kinachoendelea) hivyo akaongea alichoongea ikiwa ni utekelezaji wa kinachoendelea chini ya kapaeti.

Inawezekana kabisa watu wa system hawakumshirikisha Zitto na chama chake hasa kutokana na Zitto kwa sasa kuonekana ni mtu anaemkosoa na kumpinga vibaya sana Bwana yule na pia wakiamini chama cha Zitto hakina wafuasi wengi kama CHADEMA hivyo impact yake haitokuwa kubwa ingawa kwa hili wanaweza kuwa hawakuwaza sawaswa.

Huu ni mtazamo wangu ila muda ndio msema kweli.
 
Miaka minne mmemtukana kila aina ya Matusi Rais Magufuli

Leo mnaomba maridhiano ya nini?
 
Yule bwana mkubwa hawezi kufanya maridhiano na wapinzani. Kwasabb makungwi wake (M7 na PK) hawajawahi kukaa meza moja na wapinzani mpk leo. Na hawa ndiyo wamempa mbinu zote za kuukandamiza upinzani.

Mbowe amejaribu kutafuta namna ya kumteka huyu jamaa kwa kujishusha lkn roho na dhamira ya huyu jamaa havimruhusu kufanya maridhiano na wapinzani. PK and M7 will hit him!
 
Muda utasema ila nina wasiwasi kuna jambo linaendelea.
 
Ulichokiongea kama hisia zako ndiyo ukweli wenyewe haujakosea chochot, ila kwa muhtasari wa nchi binafsi naliona hilo ni jambo jema kwa namna yoyote ile.
Kwa sisi ambao hatuna minyororo ya Vyama na ambao Tanzania ndiyo kila kitu kwetu na tupo tayari kwa lolote kwa ajili ya nchi hii, miaka hii minne ilikua ni miaka ya giza nene na mkwamo mkubwa.
Hata kama Mbowe ameagizwa kwenda kuyaongea aliyoyaongea ma kama dhamira ya liyemtuma hivyo ni kurudisha umoja wa kitaifa, hili kwangu hilu ni zaidi ya ushindi na ni heshima kubwa sana kwa nchi. Ila kama lengo ni kutumia kauli zile kisiasa ili kumdharirisha Mbowe basi bado tutakuwa na tatizo kubwa na zaidi tutakuwa tumeongeza ukubwa wake.
 
Kalazimishwa na wastaafu alete mshikamano wa kitaifa lasivyo wenye chama wampoke tiketi ya kugombea 2020.

So tegemeeni ushirikiano wa kutosha kati yake na wapinzani kuelekea uchaguzi 2020 na baada ya uchaguzi.
 
Kalazimishwa na wastaafu alete mshikamano wa kitaifa lasivyo wenye chama wampoke tiketi ya kugombea 2020 so tegemeeni ushirikiano wa kutosha kati yake na wapinzani kuelekea uchaguzi 2020 na baada ya uchaguzi.
Inawezekana kwa kujua hili,ndio maana hata Mbowe alikubali kushiriki tukio lile.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…