Freeman Mbowe: Kiongozi wa Chama cha siasa kutokea Afrika anayeheshimika zaidi Duniani

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,752
218,339


Taarifa za Kidunia zinaonyesha kwamba huyu ndiye kiongozi wa kisiasa mwenye kuheshimika zaidi duniani kwa sasa , ndiye mwanasiasa anayeongoza kwa siasa za kistaarabu , ni mvumilivu asiye na kisasi hata kwa watesaji wake waliojiapiza hadharani na gizani kumshughulikia.

Huyu ndio Mwanasiasa aliyefirisiwa na kudhulumiwa kuliko yeyote barani Africa , ambapo wote waliosaidia kudhulumiwa kwake ama wamepandishwa cheo au wamefutiwa mashitaka yao ya ufisadi , RC wa Mtwara na Mh Mchechu ni miongoni mwa wanufaikaji wa mateso ya Mbowe , Huyu Mbowe Taarifa mpya zinaonyesha kwamba ndiye mwanasiasa aliyetukanwa zaidi katika historia ya siasa za Tanzania , huyu ametukanwa hata na watu waliokuwa hohehahe aliowaokota majalalani na kuwapa maisha akiwemo Mwita Waitara aliyeokotwa na Chadema baada ya kukimbia UVCCM alikopangiwa kuwa mpika chai wa Nchimbi aliyekuwa mwenyekiti wa UVCCM Taifa ( hii ni kwa mujibu wa kauli ya Waitara mwenyewe )

Ni mwanasiasa wa kizazi kipya asiyetishwa wala kuyumbishwa na wenye mamlaka , ni miongoni mwa wanasiasa wachache wa Tanzania WANAOFAHAMISHWA MAPEMA JUU YA NJAMA DHIDI YAO , lakini haogopi , hii imejidhihirisha hata alipofungwa jela miezi minne bila hata kuhukumiwa kifungo na Mahakama , ni miongoni mwa Magwiji wa siasa nchini Tanzania na sasa Africa na duniani , wengi wanamfananisha na kizazi cha akina Nelson Mandela na Kwame Nkurumah .

Hii ni tunu ya Dunia

 
Hakika kwa ujasiri wake, anastahili kuingia kwenye Guiness World Records
 
Kutunga uzushi dhidi ya Mh Mbowe hakutakuondoa kwenye maisha magumu yanayokukabili
 
Hah hah hah hah sio kwa kupaka ranging huko.

Mkuu asante kwa kutujuza.
 
Kama alizomewa na wapiga kura wake unadiriki kusifia uongo? Kama alikopesha Chadema deni la uongo mpaka sasa analipwa mil 50 kila mwezi unamfananisha na akina Nkurumah! Labda umemix mbege na K vant.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…