Freeman Mbowe, halipwi mshahara wowote na chama wala posho

Oct 7, 2015
86
108
Baada ya wengi sana jana kuhoji mshahara wa mwenyekiti wa chadema .mh freeman mbowe kufuati mh rais kutaja mshara wake. HILI NDIO JIBU LAKE

Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe halipwi mshahara wowote na Chama. Amekitumikia Chama kwa kujitolea kwa zaidi ya miaka 20 akiwa Mjumbe wa Kamati Kuu tangu aliposhiriki kuasisi Chama 1992, Mwenyekiti wa Vijana Taifa na baadaye Mwenyekiti wa Taifa kuanzia mwaka 2004.
Mbali na mshahara, Mbowe halipwi posho wala stahiki ya aina yeyote kama gari, nyumba, mawasiliano n.k na Chama. Utendaji wake ndani ya Chama ni wa kujitolea na kutoa.

Utamaduni huu umejengwa na viongozi wengi ndani ya Chadema kuanzia ngazi ya juu hadi chini.

Wanaolipwa posho ni watendaji wachache wanaofanya kazi full time katika ngazi ya Taifa na Kanda. Wabunge na madiwani wote walio na wadhifa wowote ndani ya Chama au katika Mabaraza yake nao hujitolea kwa asilimia 100 kwa kila namna watendapo majukumu yao ndani ya Chama. Hawapokei mishahara wala posho mbili mbili.

Hivyo Mbowe na viongozi wenzake wengi wa ngazi mbalimbali hawalipwi na Chama bali wao hukigharamia Chama kiweze kukua na kutekeleza majukumu yake kadiri iwezekanavyo.

Chanzo : Afisa habari Chadema
: Tumaini Makene
 
nimeandika mara nyingi sana humu kwamba bilionea mbowe ambaye ni Tajiri halali wa kutupwa ni kama zawadi kwa watanzania kutoka kwa Mungu , anatumia utajiri wake kugharamia uhuru wa nchi yake aliyozaliwa badala kuutumia kupora mali za nchi kama wafanyavyo matajiri wengi wa kiafrica , Mungu mbariki Mbowe , mpe maisha marefu .
 
Kwa hiyo lowassa alipowaahidi kuwalipa wenyevit wa mitaa posho ilikuwa ni changa la macho...kama chama kina spirit ya kujitolea kwa nini wasijitolee hadi kwenye serikali za mitaa??

Halafu Chadema iache ulaghai...kwa nini spirit ya kujitolea isiende hadi bungeni??mbona posho za bunge hamziachi na kuamua kujitolea???

Jingine ni hili...kama anajitolea ni vipi tunasikia anakidai chama fedha za magari ya kampeni??

Kuna wakati ni heri kukaa kimya kuliko kuibua maswali zaidi.
 
Watapinga tu hii taarifa kwa maneno bila ushahidi.

Of course, hii habari itapingwa kimantiki...Leteni matumizi ya chama na vouchers za waliosaini kuchukua fedha kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Hivi kama wewe una kampuni kwani ni lazima ujilipe mshahara? Lakini hii haimananishi kwamba hutumii fedha za kampuni hiyo.
 
CHADEMA wajitahidi kutoa habari zenye mantiki. Hivi inaingia akilini kwamba Freeman Mbowe tangu ajiunge na CHADEMA miaka ishirini yote amekuwa anajitolea? Kwamba hata posho ya kununua maji ya kunywa hajawahi kulipwa na Chama chake kwa miaka yote 20?

Halafu wanasema hata viongozi wengine nao hawalipwi chochote kwa miaka yote hiyo? Sasa kama ndivyo hela za CHADEMA zinafanya kazi gani maana hata jengo la ofisi hakuna!
 
Kwa hiyo lowassa alipowaahidi kuwalipa wenyevit wa mitaa posho ilikuwa ni changa la macho...kama chama kina spirit ya kujitolea kwa nini wasijitolee hadi kwenye serikali za mitaa??

Halafu Chadema iache ulaghai...kwa nini spirit ya kujitolea isiende hadi bungeni??mbona posho za bunge hamziachi na kuamua kujitolea???

Jingine ni hili...kama anajitolea ni vipi tunasikia anakidai chama fedha za magari ya kampeni??

Kuna wakati ni heri kukaa kimya kuliko kuibua maswali zaidi.
Kwani wenyeviti wa serikali za mitaa ni viongozi wa chama ? umekurupuka sana !
 
CHADEMA wajitahidi kutoa habari zenye mantiki. Hivi inaingia akilini kwamba Freeman Mbowe tangu ajiunge na CHADEMA miaka ishirini yote amekuwa anajitolea? Kwamba hata posho ya kununua maji ya kunywa hajawahi kulipwa na Chama chake kwa miaka yote 20?
sasa kama hutaki tukusaidieje ?
 
Halipwi mshahara,maana ruzuku zote anakamata yeye,yeye ndo anaepanga zitumikaje,hahahaha mpaka leo anakidai chama;chezea Mangi wewe pesa mbele ,mengine ndo yanafuata
 
nimeandika mara nyingi sana humu kwamba bilionea mbowe ambaye ni Tajiri halali wa kutupwa ni kama zawadi kwa watanzania kutoka kwa Mungu , anatumia utajiri wake kugharamia uhuru wa nchi yake aliyozaliwa badala kuutumia kupora mali za nchi kama wafanyavyo matajiri wengi wa kiafrica , Mungu mbariki Mbowe , mpe maisha marefu .
Mungu amwongezee neema na utashi na pia awasaidie marafiki zake kama alivyomsaidia Dr. Slaa kununua nyumba
 
Baada ya wengi sana jana kuhoji mshahara wa mwenyekiti wa chadema .mh freeman mbowe kufuati mh rais kutaja mshara wake. HILI NDIO JIBU LAKE

Mwenyekiti wa CHADEMA Mhe. Freeman Mbowe halipwi mshahara wowote na Chama. Amekitumikia Chama kwa kujitolea kwa zaidi ya miaka 20 akiwa Mjumbe wa Kamati Kuu tangu aliposhiriki kuasisi Chama 1992, Mwenyekiti wa Vijana Taifa na baadaye Mwenyekiti wa Taifa kuanzia mwaka 2004.
Mbali na mshahara, Mbowe halipwi posho wala stahiki ya aina yeyote kama gari, nyumba, mawasiliano n.k na Chama. Utendaji wake ndani ya Chama ni wa kujitolea na kutoa.

Utamaduni huu umejengwa na viongozi wengi ndani ya Chadema kuanzia ngazi ya juu hadi chini.

Wanaolipwa posho ni watendaji wachache wanaofanya kazi full time katika ngazi ya Taifa na Kanda. Wabunge na madiwani wote walio na wadhifa wowote ndani ya Chama au katika Mabaraza yake nao hujitolea kwa asilimia 100 kwa kila namna watendapo majukumu yao ndani ya Chama. Hawapokei mishahara wala posho mbili mbili.

Hivyo Mbowe na viongozi wenzake wengi wa ngazi mbalimbali hawalipwi na Chama bali wao hukigharamia Chama kiweze kukua na kutekeleza majukumu yake kadiri iwezekanavyo.

Chanzo : Afisa habari Chadema
. Tumaini Makene
Hakuna mchaga anaeweza kufanya biashr kama hyo! huu ni uongo uliopita kiwango.. ni Kubenea pekee ndo anaweza kuukubali, ila Tundu na Msigwa na yule wa kibamba.. hawawezi kuukubali, Makene umedanganya..
 
Of course, hii habari itapingwa kimantiki...Leteni matumizi ya chama na vouchers za waliosaini kuchukua fedha kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Hivi kama wewe una kampuni kwani ni lazima ujilipe mshahara? Lakini hii haimananishi kwamba hutumii fedha za kampuni hiyo.
Nenda kwa mkaguzi wa chama na msajili wa vyama utavikuta vyote hivyo
 
hakuna mchaga anaeweza kufanya biashr kama hyo! huu ni uongo uliopita kiwango.. ni kubenea pekee ndo anaweza kuukubali, ila tundu na msigwa na yule wa kibamba.. hawawezi kuukubali, makene umedanganya..
Mbona Baba yake Mbowe alimfadhili Nyerere kwenda kwa malkia kudai, uhuru jee Nyerere alimlipa nini?
 
Back
Top Bottom