Freeman Mbowe atangaza Baraza la Mawaziri Vivuli

OKW BOBAN SUNZU

Platinum Member
Aug 24, 2011
52,033
114,423
Mh.Mbowe anatarajiwa kutangaza baraza la mawiziri kivuli leo.Katika baraza hilo la nguvu linatajwa kuwa na watu makini kuliko la Magufuli linalofanya kazi kutokana na "Mizuka ya Rais".

Imedokezwa pia kuwa Mbowe amemjumuisha Zitto Kabwe mbunge pekee nje ya UKAWA, katika baraza hilo kivuli.

Updates


Mbowe atangaza baraza la mawaziri vivuli..

Wizara ya Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora.
Mawaziri – Jaffar Michael
Naibu Waziri – Joseph Nkundi na Ruth Mollel

Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira
Waziri – Ali Saleh Abdalla
Naibu Waziri – Pauline Gekul

Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu
Waziri – Esther Bulaya
Naibu – Yusuph Makame na Maftah Abdalla

Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi
Waziri – Magdalena Sakaaya Naibu
Waziri – Emmaculate Swari

Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.
Inj. James Mbatia
Naibu Waziri Willy Kombucha


Wizara ya Fedha na Mipango
Waziri – Halima Mdee
Naibu Waziri – David Silinde


Wizara ya Nishati na Madini
Waziri – John Mnyika
Naibu Waziri – John Heche

Wizara ya Katiba na Sheria Waziri
Tundu Lissu Naibu
Waziri Abdalla Mtolela

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.
Waziri – Peter Msigwa
Naibu Waziri – Riziki Shaghal

Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Waziri – Juma Omari
Naibu Waziri Mwita Waitara

Wizara ya Mambo ya Ndani
Waziri – Godbless Lema
Naibu Waziri Masoud Abdalla

Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Waziri – Wilfred Lwakatare
Naibu Waziri – Salum Mgoso

Wizara ya Maliasili na Utalii
Waziri Esther Matiko
Naibu Waziri– Cecilia Pareso

Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.
Waziri Anthony Komu
Naibu Waziri Cecil Mwambe

Wizara ya Elimu, Sayansi Teknolojia na Ufundi
Waziri – Suzan Lyimo
Naibu Waziri Dkt. Ali Suleiman Yusuph

Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Waziri – Dkt. Godwin Mollel
Naibu Waziri Zubeda Sakul

Wizara ya Habari, Utamadu, Wasanii na Michezo
Waziri – Joseph Mbilinyi
Naibu Waziri – Devotha Minja

Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Waziri – Hamidu Hassan
Naibu Waziri – Peter Lijualikali
 
UKAWA inamuhitaji zaidi Zito Kabwe kuliko yeye anavyohitaji kuwa ndani ya UKAWA. Hakuna namna nyingine ya kulikwepa hili kama wanahitaji watu wenye upeo Mkubwa wa kuisimamia Serikali.
Kwa nini wabunge wa CCM wasiisimamie serikali? Au nako hakupatikani wabunge wenye upeo kama ilivyo kwa UKAWA as you said?
 
UKAWA inamuhitaji zaidi Zito Kabwe kuliko yeye anavyohitaji kuwa ndani ya UKAWA. Hakuna namna nyingine ya kulikwepa hili kama wanahitaji watu wenye upeo Mkubwa wa kuisimamia Serikali.
Hii ni pumba.....kila mmoja anamuhitaji mwenzie.
 
UKAWA inamuhitaji zaidi Zito Kabwe kuliko yeye anavyohitaji kuwa ndani ya UKAWA. Hakuna namna nyingine ya kulikwepa hili kama wanahitaji watu wenye upeo Mkubwa wa kuisimamia Serikali.
Vyovyote iwavyo, hata kama Zito ni muhimu kuliko Watanzania wote, haijalishi. Tunahitaji umoja waksti huu kuliko wakati mwingine wowote. Hapingwi mtu au kuchukiws kwa sura yske bali kwa matendo yake.

Kama Zito baada ya kujaribu kuwa mbali na matakwa ya umma, akapata jibu. Kuna ubaya gani kwake kujirudi na kuendelea kuupigania umma?
 
No problem at all. Mbowe ataenda na zito with huge precautions like carrying a timing bomb
 
Sasa hawa ndugu zangu wa hapo ufipa sijui wataweka wapi sura zao! Maana kuanza kumwita msaliti kamanda ni ishu kubwa!

Anyway..kama waliweza kwa Luwassa naamin kwa zitto haitashindikana....ukizingatia alichoamua m/kiti hakuna wa kupinga...
 
  • Thanks
Reactions: nao
UKAWA inamuhitaji zaidi Zito Kabwe kuliko yeye anavyohitaji kuwa ndani ya UKAWA. Hakuna namna nyingine ya kulikwepa hili kama wanahitaji watu wenye upeo Mkubwa wa kuisimamia Serikali.

kwenye siasa, uwingi ni mtaji mkubwa. no numbers no power!

hata kwenye vita, jeshi la mtu mmoja haliwezi kushinda (labda iwe movie!)


nadhani umepata jibu la ni upande ugani unamuhitaji mwenziwe!!
 
Duh! Tuliambiwa Zitto ni Msaliti, Ayatollah, Mwami na majina mengineyo. Ile dhana ya kuvujisha siri kwa chama tawala imeisha? Hivi hatavujisha siri za Baraza la Mawaziri la UKAWA kweli?
 
UKAWA inamuhitaji zaidi Zito Kabwe kuliko yeye anavyohitaji kuwa ndani ya UKAWA. Hakuna namna nyingine ya kulikwepa hili kama wanahitaji watu wenye upeo Mkubwa wa kuisimamia Serikali.
Nyumba inayojengwa ni moja na fito ni zile zile. Hakuna anayemhitaji mwingine zaidi. Wote wanategemeana. Acha ushabiki usiokuwa na tija!
 
Kama ni kweli basi ni jambo zuri sana,tukumbuke kuwa umoja ni nguvu...................
 
Cdm kuwaamini unatakiwa uwe na akiri ya kushikiwa baada ya kutwambia ni msaliti leo wanataka wamjulishe kwenye baraza la mawaziri kivuri. Toka leo sitowaamini kwa lolote ni watu waongo, wagombanishi, wachochezi,
 
Huku ndio pia kuta leta Msisimko ndani ya Bunge, Of cause huwezi mwacha zito Kabwe katika hilo jamani hapo ni kuwaunganisha wapinzani ipasavyo
 
Mkutano wa pili wa Bunge la 11 la jamhuri ya Muungano wa Tanzania unamalizika leo mjini Dodoma.

Kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Aikaeli Mbowe anatarajiwa kutangaza Baraza Kivuli la Mawaziri litakalosimamia Baraza la Mawaziri la Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dr. John Pombe Magufuli(TINGATINGA).

Tayari zipo tetesi kuwa Mbunge wa Kigoma mjini kwa kupitia chama cha ACT-WAZALENDO, Zitto ZUberi Kabwe atajumuishwa kwenye baraza hilo kivuli. Huu ni mwendelezo uleule wa Mbowe wa kutafuta namna ya kujiokoa kila pale alipoona anaelekea kudondoka. Ni bahati mbaya kabisa kwamba miti yote anayoishikilia asidondoke ni ile aliyoikata kwa sababu ya kutofaa.

Zitto Kabwe alipofukuzwa Chadema na kutimkia ACT-WAZALENDO, CHADEMA ilibaki HOI BIN TAABAN. Wanachama, washabiki na wapenzi wa Chadema wakakata tamaa hadi kutamani kuona Mbowe anaachia ngazi.

MBOWE akaangukia kwenye mti alioukata na pale na kujikuta anaungana na vyama vya CUF na NCCR na kuunda Umoja wa Katiba ya Wananchi(UKAWA). Akaenda mbali na kuvunja Baraza Kivuli la Mawaziri lililokuwa na Wabunge wa Chadema pekee na kuliunda jipya lililoshirikisha Wabunge kutoka CUF na NCCR.

Mwanzoni CHADEMA waliwaita CUF na NCCR kuwa ni CCMB kwa vile CUF walikuwa wameunda serikali ya Umoja wa Kitaifa na CCM kule Zanzibar na NCCR kwa vile Mwenyekiti wake, James Mbatia aliteuliwa kuwa Mbunge na Rais ambaye ni Mwenyekiti wa CCM. Aidha waliwaita CUF MALIBERALI. CUF na NCCR ni miti ilikwisha katwa na MBOWE na chama chake.

Kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2015, CHADEMA hawakuwa na mtu mwenye sifa ya mgombea urais kupitia chama hicho. Hali ilikuwa mbaya zaidi pale bila matarajio, CCM walipomteua JOHN POMBE MAGUFULI kuwa Mgombea wao. Mbowe kwa maslahi yake binafsi tena bila ajizi akampokea LOWASSA kuwa Mgombea Urais kupitia Chadema.

CHADEMA ndiyo waliotumia zaidi ya miaka mitatu KUUJULISHA UMMA WA WATANZANIA UFISADI WA LOWASSA kupitia majukwaa ya siasa, vyombo vya habari, Midahalo na Makongamano. LOWASSA ni mti uliokatwa na MBOWE na Chama chake cha CHADEMA.

Leo kiongozi wa ACT-WAZALENDO, ZITTO KABWE akiteuliwa kwenye Baraza kivuli la Mawaziri atakuwa ni MTI wa TATU kumuokoa MBOWE asidondoke. Mbowe anajua mziki wa Rais wa John Pombe Magufuli. Ni lazima awe na mtu mwenye uwezo kujenga hoja vizuri Bungeni la sivyo yeye na chama chake atajikuta anaangukia pua.

MBOWE anamuona Zitto kama Kimbilio lake. Sote tunakumbuka chanzo cha Zitto Kabwe kufukuzwa chadema ni mgogoro kati yake na Mbowe. Mbowe mwenyewe amekiri alimkosea ZITTO juzi Bungeni wakati akitoa mwelekeo wa jinsi Baraza lake kivuli litakavyokuwa.

TAFAKURI:

1.Tabia hii ya MBOWE kukimbilia kuegemea kwenye miti ambayo kwake ilikuwa ni kikwazo ni dalili za kuchoka. Anahatarisha uhai wa Chama kwani kuna siku ataugemea mti wa aina hiyohiyo na ataanguka nao.

2. Wanachama na Wapenzi wa Chadema na Watanzania kwa ujumla tunakosa imani na Mbowe, tunamuona kama mtu anayeangalia maslahi binafsi na siyo maslahi ya Chama na Wananchi kwa ujumla.
 
Back
Top Bottom