- Source #1
- View Source #1
- Tunachokijua
- Madai
Agosti 17, 2025 imeibuka taarifa kwa umma iliyoambatanishwa kwenye grafiki zenye utambulisho wa baadhi ya vyombo vya habari ikieleza kuwa aliyekuwa mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe ametimuliwa uanachama na chama hicho.
Barua hiyo imeeleza sababu mbalimbali ikiwemo Mbowe kutokuhudhuria kesi ya mwenyekiti wa sasa Tundu Lissu, Mbowe kuhudhuria uzinduzi wa dira ya Taifa na mambo mengine.
Uhalisia wa Taarifa hiyo
JamiiCheck imefuatilia na kujiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli.
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck kupitia nyenzo za kidigitali imebaini kuwa taarifa hiyo ya haijachapishwa katika kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA).
Aidha grafiki zilizotumika kusambaza taarifa hiyo ni za kughushi na hazijachapishwa na Mwananchi na Jambo Tv kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii.
Grafiki hizo zina makosa za kiuandishi matahalani rejelea grafiki yenye utambulisho wa Jambo Tv imetumia neno ‘uwanachama’ badala ya ‘uanachama’, pia zimetumia fonts tofauti huku zikiwa na mpangilio tofauti ukilinganisha na grafiki halisi za vyanzo hivyo rejelea grafiki ya Mwananchi.