Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 124,399
- 236,026
Leo Jumapili Freeman Mbowe amefika kwenye kanisa la KKKT Azania Front na kufanya maombi maalum yakiambatana na Sadaka, kwa lengo la Kumshukuru Mungu.
=========
Freeman Mbowe: Leo nimewaona wakristo wenzangu, sikusudii kuzungumza mengi zaidi ya shukrani. Nimepata hofu sana na hofu kubwa inayonikabili sio mimi kuishi gerezani ila Mungu atanipa uwezo gani wa kulipa mapenzi, sala na misaada mbalimbali ya dunia ambayo iliniandama nikiwa gerezani.
Watu wengi wamelia na mimi, watu wengi wamelia na familia yangu, watu wengi wa vyama vyote, wa Serikali wamefanya sala, wamefunga kwaajili yangu.
Nimeshtakiwa kwa kosa zito sana, ambalo inawezekana wengine wanaona tu ni ugaini lakini hawajui tafsiri ya neno gaidi. Shtaka lolote chini ya ugaidi lina kifungo cha miaka 15 kwa uchache hadi miaka 30 na hakuna faini.
Watu wengi na watu wote walikuwa wanaomba mara kwa mara mtoeni Mbowe, futeni mashtaka ya Mbowe. Mimi nilikuwa naomba msifute mashtaka haya hadi ukweli udhihirike, nilitamani nisikie hao walionituhumu kwa ugaidi watatoa huo ushahidi upi ili dunia ielewe.
Kulikuwa na mahakama ya mahakamani na kulikuwa na mahakama ya umma, sasa hayo yote tuyaache. Nilishukuru sana niliposikia upande wa Jamhuri umefunga ushahidi wake, nikasema Mungu asante iache dunia iamue kwa ushahidi huu kama kweli nilikuwa gaidi, watu wamenipa upendo wa ajabu sijui nitawalipa nini.
Magereza wananiambia tangu tumeanza magereza hii kwa umri wetu wa utumishi hatujawahi kuona mfungwa anayepata wageni wengi kama wewe. Siku ambayo nimepata wageni wengi walikuwa 214, nikalazimika kuweka register ya wageni wote wanaokuja kunipa pole lakini miezi nane haikupotea bure, nimepata muda wa kusoma, kuandika.