Fredwaa (Fredi Fidelis) forgive, forget and move on? PB imepoaaa

Mara zote naitamani Kiss Fm ya 2010 kurudi nyuma

Asubuhi unaanza na John Karani JK na mwanadada fulani simkumbuki. Baada ya hapo ni Kiss Prime Time
The Big Fuse na Captain JML Joachim Munga Luguru (alikua anasema "keep on your inner ear and get terrifying"). Alikua na DJ Jeff Jerry...noma sana

Baadaye hii show alirithiwa na Ezden The Rocker,akaibadili jina na ikaitwa Bongo Collabo Mix Show. Hakuiharibu sana

Saa tano kamili tunapata News from the BBC na show inaendelea mpaka saa sita. Hapo tunapata show ya afternoon mpaka saa nane

Kuanzia saa nane ni Kiss Hot Wire na Dj Chriss...we acha kabisa

Saa kumi ni Kiss Drive. Ilikua na mtangazaji bonge moja la vocalist Dunia nzima Tobby The Splash! Huyu jamaa sijaona mfano wake mpaka sasa.

Show ya Tobby iliisha saa kumi na mbili jioni. Hapo aliingia Dee Seven na African Beat...mitamboni alikuwepo DJ Maliz..kulikua na jingle ya miluzo...fyuu fyuuuuuu...! acha kabisa Mangi. Hii ilikua ndio show pekee ya kiswahili kwa hii redio. Ilisimamisha mitaa yote na daladala zote Dodoma enzi hizo. Mji mzima iliskika sauti moja tu ya Kiss FM

Saa mbili kamili show iliisha. Aliingia mwanamama Sharbano Aboubakar "Sherry" na Kiss Comfort Zone. Ilikua hatari nyingine

Kuazia saa tatu kulikua na habari za BBC na sports kama sikosei. Saa nne kamili alichukua usukani jamaa mmoja mlavidavi aliitwa Gody B The Pilot na show iliitwa Love Zone! Acha kabisa arif...

Weekends waliungana na redio za marekani. Show ya Ryan Seacrest ya American Top 40 ilirushwa Mubashara. Kulikua pia na Weekend Top 30. Jumamosi kulikua na sebene mix za kufa mtu kuanzia saa tisa mchana

Walikua na best DJ's...Dj Maliz,DJ Devi,DJ Jeff Jerry,DJ Chriss na wengine

Kiss FM ilivyoharibika na watangazaji wote kutimkia kusikojulikana basi nilipatwa na msongo wa mawazo!

Aliyeiloga Kiss FM alaaniwe sana! Sasa hivi redio zote zinatengeneza programu sawa tu na Clouds. Hakuna ubunifu wowote utakaomfanya msikilizaji awe na choice ya program za redio tofauti. Program za asubuhi,mchana,jioni na usiku ni zilezile kwa redio zote. Ovyo kabisa!

Fredwaa pale RFA alikua na show ya tofauti sana na ubunifu wa kipekee nje ya huu mfumo wa ki-clouds. Sasa alipoenda clouds pale alikosa kabisa emotional freedom ya kufanya makeke yake! Natamani kumwona jamaa akiwa na show yake mwenyewe kwenye redio kubwa. Energy Man is very talented! Mashabiki wake tutakua naye mpaka mwisho!



Sent using Jamii Forums mobile app
Kiongozi Asante Sana..umetisha Sana..umenikumbusha mbali Sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe Bwana Mdogo umemaliza kila neno langu

Umenigusa moyo wangu na hii ni comment bora sana kwa mtu anayejua Kiss Fm unayoiongelea

Wakati ule Dee Seven na DJ Maliz walikua kama vichaa kuna wakati wanapiga Hip Hop kipindi kizima na kuna wakati RnB tu.

Nakumbuka sana dogo Yaki, Producer Amber wamepigwa sana kwenye African Beat kwa mara ya kwanza nimemsikia Joh Makini na River Camp Soldiers wakat ule tu.

Jumapili Ryan Seacrest na Amercan Top 40 ndio mara ya kwanza nilisikia Beautiful Girl ya Sean Kingston

Kila ikianza See it started at the park
Used to chill after dark
Oh when you took my heart
That's when we fell apart

Nakumbuka ile Kiss Fm times 3!






Sent using Jamii Forums mobile app
Umenikumbusha YAKI..2007 alikuwa noma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mwambie wewe, vijiwe vyote vya kahawa vina redio, kwa shoe shine, muuza matunda wanasikiliza redio hata walinzi wako lindo wanasukuma muda kwa kusikiliza redio
Hata kwenye hizi smart phones kuna redion......huyo muhuni aache mbwembwe
 
Yupo na Coy ya Caltex wewe

Sent using, Mashikoro Mageni
Umeelewa alichouliza na nilichojibu..?
Ndio tunajua yuko na kampuni ya ORION ananadi bidhaa ya Caltex, swali lilikuwa ni kwa nini hasikiki redioni, kufanya kazi Clouda na kufanya kazi Orion vitu viwili tofauti
 
Kukua Kwa social network na kuongezeka Kwa watumiaji wa smartphone ndo kumeiua amplifaya mana vtu vingi jamaa ana Google , sasa watu wanavipata fasta tuu bila kumsubir yeye tofaut na zaman, kama website yake ndo kabisaaa .... Ni kama zaman watu wakisikia Nyerere anahutubia wote wanajikusanya kwenye redio ya kijiji ...na walimwaminia kuwa anajua vitu vingi kumbe jamaa naye alikuwa na access ya news from abroad af anakuja kuwaringishia wabongo
kazee sikapendi kale. ndiyo chanzo ya kuua elimu yetu na maujinga mengine.
 
Back
Top Bottom