Fredrick Lowassa, mbona kimya Bungeni?

malang0

JF-Expert Member
Apr 7, 2021
440
518
Ni takriban miezi saba sasa tangu uwepo wa bunge hili, Mbunge wa Monduli Mh. Fredrick Lowassa hatujamsikia akichangia chochote kama alivyokuwa mtangulizi wake, Mh. Julius Kallanga aliyekuwa na makeke sana?

Au naye kajiunga kwenye kundi la Mh. Abood yule wa Morogoro asiyechangia bungeni?
 
Mkuu ukiiangalia tu ' Body Language ' ya Fredy Lowassa huhitaji ' IQ ' kubwa kugundua kuwa huo Ubunge alionao sasa Yeye hakuutaka ila 'alishinikizwa' na 'kulazimishwa' na Hayati Mwendazake ili tu 'Kumfurahisha' na hata 'Kumpoza' Baba yake na 'Maumivu' pamoja na 'Mateso' ambayo CCM na Serikali yake walimpatia Mzee wa Watu ili tu 'Kumkomoa' na arejee rasmi Chamani ( CCM ) na akarudi kweli.
 
Kwa Monduli huyo ni mbunge-hasara tosha. Kwanza inasemwa ni chapombe wa kukata na shoka. Pili, huyo alibebwa na baba yake, hivyo maendeleo ya jimbo hilo yataendelea kutegemea ushawishi wa mzee huyo kwa watawala walio madarakani.

Wenye Monduli yao wanasema yule aliyeshika nafasi ya tatu kwenye maoni ndiye angetoa utumishi bora, lakini shida yake hakuwa na pesa za kuhonga.

Hasara nyingine ya Monduli ni baraza bovu la madiwani wanaoongzwa na mla rushwa aliyekubuhu. Huyo yuko hapo kushibisha tumbo lake huku halmashauri hiyo ikiendelea kuoza.

Sasa: Mbunge Bomu + Mwenyekiti wa Halmashauri Bomu = HASARA KWA MONDULI
 
Ni takriban miezi saba sasa tangu uwepo wa bunge hili, Mbunge wa Monduli Mh. Fredrick Lowassa hatujamsikia akichangia chochote kama alivyokuwa mtangulizi wake, Mh. Julius Kallanga aliyekuwa na makeke sana?

Au naye kajiunga kwenye kundi la Mh. Abood yule wa Morogoro asiyechangia bungeni?
Unataka aongee nini wakati Jimboni kwake anafanya mambo? Halafu hatafuti uteuzi tofauti na yule kichaa msukuma sijui anauwaza uwaziri tu. Akasome kwanza
 
Hivi kuwa mbunge mzuri lazima uwe unaongea ongea sana bungeni? Mbona wapo wanaongea mara kwa mara lakini michango yao inakuwa pumba tu.
Mnakumbuka yule aliyeongelea nguvu za kiume? Mwingine akataka kupanda juu ya meza!
 
Hao hawajengi hoja zenye mantiki na ni viti maalum hawana majimbo, ukiwa bubu wananchi wako hupeleki hoja zao kwa serikali, wananchi wamechagua mtu wa kwenda kuwasemea hoja zao
 
Ni takriban miezi saba sasa tangu uwepo wa bunge hili, Mbunge wa Monduli Mh. Fredrick Lowassa hatujamsikia akichangia chochote kama alivyokuwa mtangulizi wake, Mh. Julius Kallanga aliyekuwa na makeke sana?

Au naye kajiunga kwenye kundi la Mh. Abood yule wa Morogoro asiyechangia bungeni?
Wabunge wote wa ccm wako kma wamekaa wodi ya mirembe wakisubiria dawa
 
Sasa mtu amezaliwa
Amelelewa hajui wala hajawahi kuona shida

Sasa aanze kuzungumzia matatizo ya matundu ya vyoo,shida ya maji etc wakati shida hazijui

Ova
 
Hebu watafute wabunge wanaochonga sanaaaaa mfano Kibajaj, Msukuma n.k...

Halafu rudi kutazama maendeleo katika majimbo yao na uyalinganishe na majimbo ya wabunge watulivu bungeni...

Baada ya hapo tutaweza discuss hili la mwana wa Lowassa kuwa 'bubu bungeni'
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom